AL HABIB MICHUZI

Sabal Khayr.

Mimi naomba nishauri kuwa kama mtu anatuma shairi basi iwe kwa maximum beti ziwe 3  ili iwe rahisi kwa msomaji  .Pia sharti lingine Shairi shurti liwe ni kiswahili sanifu ili kuondoa wanaoharibu lugha (lisiwe na kiingereza). Muhimu pia mtu aelezee kwa nini anaandika hilo shairi.Mimi bado nasubiri majibu toka kwa huyo niliyemwomba Mkopo kwenye shairi la MKOPAJI

Na kama ni swali limeulizwa basi si haba shairi likawa juu ya habari kwa masaa 24 kama hakuna majibu basi habari zingine zifuate lakini majibu yakitolewa basi si haba kama yakawa juu


Natumai Malenga wenzangu wataunga mkono hoja







-Wimbi la mbele


 Hili nalo ni shairi la Muyaka bin Hahi al Ghassay wa Voi Kenya na aliliandika kwenye karne ya 18. Kwa sasa nitatoa beti 2 tu lakini mshairi anazungumzia kutendeana wema:

Akutendeae Mema
Kumsuhuru ni lazima
Jaza ya mema ni mema
Maovu Umeyatia

Mbona umeghafilika?
Kwa jambo lisilo na shaka?
Shetani umemshika
Umemwacha nabia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2012

    mashallah shairi zuri na limepoa na ni kweli wengi wetu tumeshika shetani tumemuacha rababa na nabiya

    ReplyDelete
  2. bashir omarJune 19, 2012

    bwana michuzi, habari navutiwa na uwanja wako ni mpana na wenye njia nyingi za kupitia ahsante kwa kuwapa watu sehemu ya kukutana na kuzungumzia yao na yetu pia. mimi nimpenzi wa blog hii nataka kutoa ushauri kwa mshairi aliyeomba mkopo,amejieleza vyema ila tena aliporudi akishauri watungaki watunge alau beti mbili au tatu na pia waelezee maudhuina dhamira hakisi za tungo zao, hapo aaaah, sikumuelewa ushairi wa sasa ndiyo unaojifunua hadi kujua mradi wa mtunzi.Si dhamira yangu kumuumiza mtoa maoni la hasha,tunafurahishwa na mashairi ya watunzi wa njia za kizamani,ukune kichwa hadi upate maudhui ya mtunzi.Shairi la juzi hapa linalohusu sensa mbona lilikuwa zurisana je lingekuwa beti tatu lingejitosheleza kweli? hamu isingekwisha,lakini maoni yangu angalau basi beti nane hadi kumi zitatosha.Huu si ugonvi ni maoni yangu tu sikusudii kumkwaza yoyote.Nawatakieni kila la kheri.
    mdau
    Bashir kigamboni

    ReplyDelete
  3. Kila mema anotenda, thawabuze azichuma,
    Dini zote hebu randa, wema himizwa lazima,
    Tenda wema kisha nenda, shukurani si lazima,
    Kinyume anaekwenda, anamuudhi KARIMA,

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2012

    Mkopaji:

    Ni muhimu ukajibiwa kwa misitari mirefu ili upashwe ukorofi wako wakati ukidaiwa kulipa deni la Mkopo.

    1.Kumbuka ya kuwa Kukopa kutamu kama asali kulipa kuhcungu kama Shubiri !!!

    2.Kumbuka kuwa wewe Mkopaji unakmfuata Mkopeshaji ukiwa Mstaarabu lakini wakati ukitakiwa malipo unakuwa mbogo na mkorofi !

    3.Kumbuka kuwa ewe Mkopaji unamfuata Mkopeshaji ukiwa Bwege mtozeni, ukifanikisha kupewa mkopo wakati wa kudaiwa unakuwa unaijua sana Sheria ya Mikataba !!!

    Ahhh, Ubinaadamu Kazi !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...