Watanzania wengi bado hatujaweza kutambua uwezo mkubwa tuliokuwa nao katika kuchangia maendeleo yetu. Inaeleweka kwamba kumekuwa na kilio kikubwa kuhusu michango ya kila siku katika sekta ya elimu. Hatahivyo mengi ya malalamiko haya yanatokana zaidi na wasiwasi wa matumizi ya michango husika. Michango hii ikielekezwa mahala stahiki na kuhusisha wachangiaji juu ya matumizi yake ina uwezo mkubwa sana wa kubadilisha maisha ya watoto wetu walioko mashuleni.
Tatizo sio UWEZO, tatizo hasa ni NIA. Watanzania kwa kiasi kikubwa tumekuwa na utamaduni wa kuchangia zaidi shughuli zinazoshahabiana na anasa kuliko kuchangia maendeleo. Kwa wenzetu wakenya kuchangia watoto wa majirani kwenda shule ni sehemu ya utamaduni uliojikita. Mathalani kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo kuna watanzania zaidi ya milioni nne watu 100,000 huudhuria sherehe za harusi kwa mwezi kiwango cha chini cha uchangiaji kawaida ni Tshs 60,000. Kama hii ndiyo hali inamaanisha kuwa kwa mwaka sisi wakazi wa Dar es Salaam tunatumia kiasi cha shillingi 72,000,000,000,000 kiasi ambacho kingeweza kupeleka watoto 720,000 kwa gharama ya Shillingi 100,000 kwa mwaka. Kwahiyo tungetoa asilimia kumi tu ya matumizi yetu kwenye harusi tungepeleka watoto 72,000 shule kila mwaka!!!
Labda tutaulumu mfumo wetu wa ujamaa kwa kutuzoesha kwamba tungeweza kupata huduma zote toka serikalini. Serikali ikawa ndio baba ndio mama na hivyo hata wajibu wa kimsingi kama kupata elimu ya msingi tukaiachia serikali. Umiliki wetu wa jambo hili la msingi na lazima ukapotea kwa utaratibu huo. Ni rahisi kusema kuwa serikali inakusanya kodi kwahiyo ifanye kila kitu lakini ni sawa na kuomba rafiki yako amtunze mwanao wakati ukilipia gharama za matunzo hayo. Ni dhahiri bado utahitaji kuingia gharama za kuhakikisha mwanao anapata matunzo yanayokidhi mahitaji na ndipo hapo kila mara utakapomtembelea mwanao utajikuta ukiongeza kagharama kidogo ka kununua pipi, kubadili nepi, kubadili maziwa na vitu vingine vidogo vidogo ambavyo huwa haviachi kuibuka. Bila shaka wote tukichulia elimu kwa uzito tunaouchukulia watoto wetu wa kuzaa tunaweza kupiga hatua.
Natoa wito kwa kila mmoja wetu kutafakari nafasi yake katika maendeleo ya elimu nchini. Tunaweza kuendelea kukaa kimya au kuchukua hatua sasa. Nwakaribisha vile vile kuendeleza mjadala kupitia ukurasa wa faceboo @Educate the Children of Tanzania na kupitia twitter @shujaawakarne.
Mwandishi wa makala haya ni Katibu Mtendaji wa asasi ya EDUCATE THE CHILDREN; asasi ya kitanzania inayojihusisha na kuchochea upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wa kitanzania na kwa namna ya pekee watoto wanaotoka kwenye familia duni.
Umenena mpendwa,nami nashangaa sana jinsi tunavyoshobokea michango ya harusi kuanzia kwenye k/party hadi kumaliza shere ya kamati.Pia nimeona kweli wabongo tunapenda sana sherehe kuliko maendeleo mengine.Hata ughaibuni utashangaa wabongo wanafanya sherehe zingine ambazo hazina kichwa wala miguu na kutumia gharama nyingi.Ukiwaeleza kuchangia maendeleo ni kama unawatupa jehanamu.Mdau asante kwa hoja yenye maana sana kama tuna masikio ya kusikilizia tukabadili mwelekeo.
ReplyDeleteHii tabia ya kushabihisha michango ya harusi na mahitaji mengine ukome jamani. Tuache harusi ibaki na taratibu zake na mambo mengine yaanzishiwe taraitibu zake pia. Jukumu la kusomesha watoto ni la kifamilia zaidi na halistahili kiuwazi uwazi kuwa wajibu wa jamaa na marafiki. Yaani wewe uzae halafu mimi niwajibike kukusomeshea mwanao, na wa kwangu atasomeshwa na nani? Hilo ni suala la kifamilia wakati harusi ni tafrija iliyo pana zaidi. Tuache kufananisha ndizi na machungwa, japo yote ni matunda lakini hayafanani.
ReplyDeleteSuala la kusomesha linaweza kupewa hadhi ya kiukoo (kama ukoo una maelewano mazuri au kiongozi anayefaaa)na kila familia ikachangia kiasi fulani kila mwezi au miezi miwili kwa ajili ya wenzao wasiokuwa na uwezo, vivyo hivyo kwa matibabu.
Nawahakikishieni, mpende msipende, hakutakuwa na shuluhisho mnalolitaka hata siku moja, mtaishia kuongea na kulalamika tu kila siku bila matokeo. Suluhisho ni mawazo mbadala ya utatuzi na sio ya kimfumo wa vipaumbele.
Ila mie nina mtazamo tofauti, ni asilimia ngapi ya watz wanaopenda sherehe? sanasana utakuta ni wanachuo na vijana wa mjini wanaojifanya celebrity katika maeneo yao. Kuhusu harusi wengine ndio mitoko yao akichangia harusi yake moja January hutamwona kwenye ukumbi wowote mpaka May kwenye harusi nyingine ila kikubwa ni kupunguza gharama na mchakato mzima wa harusi ziwe na uhalisia maana bw ba bi.harusi hawana gari wala nyumba lakini ukiangalia harusi yao gari na ukumbi uliotumika utashangaa ukija kwenye maisha ya kawaida ukakuta wanaishi kwenye chumba na sebule.
ReplyDeletesuala la kuchangia au kutochangia harusi ni la kibinafsi but pia ni la kijamii, kuna watu wanataka hata kulazimisha kwa hiyo ni vizuri hoja kama hizi zikaletwa ili mtu usipochanga, watu wakuelewe badala ya kukushangaa. mfuko wa familia au ukoo ni jambo zuri sana. kuna wengine wanakwenda outing za hela nyingi na kuvaa vitu vya gharama kubwa, hao maisha yao ni ya juu na waachwe wachangie wanavyotaka, BUT, wale wasio nacho pia wasaidiwe na groups kama hizo za "educate children" nina uhakika hao wanaotoa michango ya harusi kila siku nao watachangia mfuko huo, maana wanazo
ReplyDeleteNaunga mkono hoja ila naomba kukusahihisha hesabu kidogo kama watu 100,000 huhudhuria harusi kwa mwezi ina maana wachangiaji ni 50,000 kwa kuwa kadi 1 huingiza couple au kwa kiswahili watu 2. Na kwa kuwa wastsni uliouweka ni 60,000 basi nikizidisha hapo napata Tzs 3,000,000,000 (yaani bilioni 3). Hii ina maana kwa mwaka unazidisha kwa 12 na utapata billioni 36 (Tzs 36,000,000,000).
ReplyDeleteHatahivyo kiwango hiki bado ni kikubwa mno kwa vyovyote vile ni aibu kutumia kiasi hiki chote kwa sherehe wakati tu maskini kiasi cha kutisha!
Naunga mkono hoja ila naomba kukusahihisha hesabu kidogo kama watu 100,000 huhudhuria harusi kwa mwezi ina maana wachangiaji ni 50,000 kwa kuwa kadi 1 huingiza couple au kwa kiswahili watu 2. Na kwa kuwa wastsni uliouweka ni 60,000 basi nikizidisha hapo napata Tzs 3,000,000,000 (yaani bilioni 3). Hii ina maana kwa mwaka unazidisha kwa 12 na utapata billioni 36 (Tzs 36,000,000,000).
ReplyDeleteHatahivyo kiwango hiki bado ni kikubwa mno kwa vyovyote vile ni aibu kutumia kiasi hiki chote kwa sherehe wakati tu maskini kiasi cha kutisha!
Naunga mkono hoja ila naomba kukusahihisha hesabu kidogo kama watu 100,000 huhudhuria harusi kwa mwezi ina maana wachangiaji ni 50,000 kwa kuwa kadi 1 huingiza couple au kwa kiswahili watu 2. Na kwa kuwa wastsni uliouweka ni 60,000 basi nikizidisha hapo napata Tzs 3,000,000,000 (yaani bilioni 3). Hii ina maana kwa mwaka unazidisha kwa 12 na utapata billioni 36 (Tzs 36,000,000,000).
ReplyDeleteHatahivyo kiwango hiki bado ni kikubwa mno kwa vyovyote vile ni aibu kutumia kiasi hiki chote kwa sherehe wakati tu maskini kiasi cha kutisha!