Kwako Anko Michuzi,

Nakupongeza kwa kutuhabarisha.

Napenda kutoa hoja yangu hapo juu ambayo imenikwaza kwa muda sasa.

Watanzania wengi hasa tuishio mijini tumekuwa tunatoa pesa nyingi kuchangia harusi za kifahari. Watu wenye uwezo wa kawaida wanapanga harusi zenye bajeti za mamilioni wakitegemea michango wapitishie ndugu na marafiki. Na mchango wenyewe sio wa alfu kumi au ishirini, wanataka laki kwenda juu, ukitoa chini ya hapo unanuniwa. 

Kwa mfano mme mtarajiwa mshahara wake laki mbili mke mtarajiwa laki mbili - bajeti ya harusi milioni ishirini - wanandoa wanachangia nini - ziro- ukiweka vikao, nauli kumleta bibi kutoka kijijini, chakula cha wageni -kabla ya harusi yenyewe -baada ya harusi kila ndugu na jamaa amefilisika, wanabadili njia kukwepa madeni, furaha iko wapi?

Kama harusi ni upendo na kujenga familia kwa nini isiwe chai maandazi au biskuti kila mwalikwa alete sinia la chakula tule pamoja tuwapongeze maharusi - viongozi wa dini husika watoe nasaha zao, -wazazi wapongezwe kwa vifijo na vigelegele - halafu maharusi waende kijijini kumsalimia bibi na babu - wapeleke pea ya kanga na kilo ya sukari. Waishi raha mstarehe?

Kwanini tunataka makubwa tusiyoyaweza? ninapokuchangia laki mbili kwenye harusi yako halafu mkaachana baada ya mwaka hela yangu mtarudisha? Ukioa tena nichange?

Harusi ukianzia maandalizi, sare, kitcheni party, vikao, sendi ofu, ndoa, honey muni na mengine kibao yanafanya harusi kuwa kikwazo kwa wengi na maharusi kuwa omba omba.

Niliwahi kualikwa kwenye harusi ya wenzetu ulaya - dress code casual, chakula snacks and drinks - time 6-8PM, usafiri jitegemee, picha na video -rafiki wa maharusi kajitolea. Zawadi ukipenda toa donation kwa WFP au UNICEF. 

Jumla ya gharama ya harusi Euro 1000 kipato cha maharusi jumla Euro 6000 kila mwezi.

Baada ya sherehe familia ilikwenda kwa chakula cha jioni marafiki - KWA HERI.
Nimeamua kuanzia mwaka jana nitakuwa nachangia elimu, matibabu na mambo ya manufaa. Ndugu na marafiki TUBADILIKE.

KWANINI TUSICHANGIANE GHARAMA ZA ELIMU ? MILIONI ISHIRINI HAIMSOGEZI WANAFUNZI WA CHUO?

Nawasilisha,

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2012

    Kiongozi hii nakuunga mkono mia kwa mia.Hata mimi inaniboa sana.Maelezo yako yanajitosheleza sina zaidi.Kweli inabidi tubadilike.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2012

    Ya Mungu mpe Mungu na ya Kaisari mpe KAISARI. Mchango wa HARUSI uko kivyake, kadhalika na wa masuala mengine kama vile elimu uko kivyake. Kwa hiyo wewe ukitaka kuchangia changia, lakini usipotaka kula pini.

    Usifananishe Tanzania na nchi za Europe. Kila nchi ina utamaduni wake. Kwa nchi ninayoishi mimi watoto wakifikisha miaka 18 mara nyingi wanaondoka kwa wazazi, wanaenda kujitegemea! Mfano mwingine ni pale wanapofanya mapenzi hadharani kama vile wapo kitandani, isipokuwa hawatiani tu. Je, na sisi tufanye hivyo?

    Waache wale waendelee na utamaduni wetu. Na sisi tuendelee na utamaduni wetu. Ukiwa na uwezo uandae harusi kubwa tu, na utoe mchango mkubwa sana, wengine wachangie kidogo. Lakini kama uwezo hauna uchange kidogo, wenye uwezo wataongezea zaidi.

    Hakuna ambaye huwa anachukua pesa ya mtu kutoka mfukoni mwa mtu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2012

    tunakuunga mkono kabisa. hii tabia ife hizo milioni ishirini ishirini zingeesha jenga mashule kibao au kununua madawati kwa shule nyingi nchini. Watu waamke waache umaarfu. Bwana mmoja namfahamu alifaniwa harusi kubwa siyo yeye alitaka lakini wapambe na baada ya mwaka ndoa hakuna. Na mimi kuanzia leo sichangii hayo malaki hela zinaenda kwa mama!

    Mdau Marekani!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2012

    UMENENA MDAU

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2012

    umenena vya kutosha MDAU

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2012

    Mdau hapo nakuunga mkono kwa 100%. Harusi ni kitu ambacho mtu unakipanga mapema, sasa kama unajua in advance kwa nini usipange budget inayoenda na kipato chako? Kwani lazima watu waone umefnaya sherehe ndo wajue umeoa? Huu ni upuuzi kabisa. Mishahara yetu hii ilivyo midogo unakuta 40% imeenda kwenye michango ya harusi bila kujijua.
    Misiba tunawezq kuchangia maana ni kitu mtu hutegemei kinakuja bila ya kuwa umejipanga lakini sio harusi.
    Watanzania tubasilike jamani

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2012

    SAFI SANA MDAU, watanzania tunapenda maisha ya kujionyesha makuu kwa kutumia migongo ya wengine na dhuluma.
    Tatizo kubwa ni UBINAFSI na UNAFIKI.
    Mtu unajua hali ya maisha ya wengine ilivyo kisha unajipangia harusi kwa mifuko ya wengine, hiyo ni haki kweli?
    Tunajifikiria sisi wenyewe ubinafsi, hatufikirii hao wachangiaji wana kipato gani, wana majukumu gani katika familia zao, watoto kwenda shuleni, matibabu, nk, tunapokonya hata kidogo walichonacho eti kushibisha matumbo yetu kwa sherehe, tukiwaacha wakisoto na familia zao.
    Hii ni DHULUMA kubwa sana na ni DHAMBI kwa mwenyezi MUNGU.
    Bongo kuna watu kibao wanahitaji misaada, walemavu nk, watu hawachangii, lakini wanafikiriia kuchangia minuso tu.
    Wenzetu ulaya hata baadhi ya nchi za Afrika hawana haya mambo ya kipuuzi, kama mtu una sherehe yako, utaandaa mwenyewe ukiweza kualika watu, sawa, kama huwezi hakuna mtu wa kukulaumu, hawana maisha ya kujionyesha au kutaka makuu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2012

    Kaka nimependezewa sana na mswada wako, wewe ni mmoja wa watu ambao umelengwa na hili swala. Kwa ujumla michango ni sawa bali mtu asitegemee au asiweke kiwango maana mchango uunaouomba unamuomba hata mtu mwenye hali ya chini kimaisha otherwise uandae arusi ya kawaida isiyokuwa na gharama kubwa kuliko uwezo wako.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2012

    Nakuunga mkono mdau uliyetoa maada hii. Mimi pia hii kitu imekuwa inanisumbua sana. watoto wengi wanamaliza shule za msingi wanashindwa kuendelea kusoma sekondari sababu familia zao hazijiwezi, husikii watu wakisema jamani tuchangie mtoto wa fulani aendelee na shule ila kila siku utasikia ni michango ya sherehe tu. Kweli inabidi tubadilike tuchangie na mambo ya maana. wenzetu wakenya wanafanya harambee kuchangiana kwenye mambo ya kuleta maendeleo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2012

    Mdau hayo uliyoyasema ni kweli kabisa, watanzania wengi wanaendekeza sana starehe isiyokuwa na maana yeyote,yaani harusi ya siku moja inagharimu mamilioni ya pesa,ukiangalia bwana na bibi harusi wanakaa nyumba ya kupanga, lakini kwa ujinga wa watu wapo tayari kutumia mamilioni ya pesa ktk shughuli ya harusi ya siku moja!Jamani tuache ujinga na tujaribu kusonga mbele,tufanye kitu cha maana chenye faida kwa binaadam,kwa mfano tuwachangie wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kusoma,tuwachangie wagonjwa wasioweza kupata matibabu, vitengo vya watoto yatima,walemavu n.k ili tupate thawabu na kuleta maendeleo, lakini sio kuchangia maharusi,hayo mambo ya kitchen party,vinywaji,keki,chakula,pombe n.k yote ni ufahari na hanasa zisizokuwa na faida yeyote,kwa wanaooana na kwetu sisi tunaowachangia,Ulaya hawana mambo ya kijinga kama hayo ya bongo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2012

    Hapo ulipogusa mdau..weeeee.Heri mimi sijasema.Ila Dar imezidi kwa michango ya harusi tuseme ukweli.

    David V

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2012

    Ndugu umewakilisha kitu cha ukweli katika jamii ya kiTZ,pia nashukuru umeiweka hewani japo nilikutangulia kiasi kuto kuchangia hivi vitu, maana kama hawawezi harusi yao na kukununia je, watakapopata mtoto? Na hawa ndio watalazimisha aende ACADEMY zilizo nje ya uwezo wao pia kwa michango/mikopo ya lazima au kununiwa.Kuna watu wengi wenye shida za kweli ktk jamii/hospital yetu n.k. hata hawapati michango wa kununua paracetamol wanaachwa wajifie, kisha mtu anakununia kisa hukuchangia harusi yake ya 20mil. Siogopi kununiwa kwa hii bali hunipa kujua upeo wenu na ni chujio zuri kwa watu nao taka jihusisha nao kwa mambo mengi zaidi.

    Ahsante.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2012

    That is logic. I support you 100%.
    I will contibute to the forgotten children to those remote areas of Tanzania who have no shoes or exercise books. We are so selfish. Only thinking to ourselves and not about others.
    God bless you.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2012

    I know this long time ago that it is a heck of stupidity to contribute money for people to drink and eat for a single day then what next the newly wed know!
    I never give money to this event! If i did not more that Tsh 50000. What a non sense! See our seniors in the villages, see those kids in the hospitals. If we could take 10% every month to these people our country will be in a better shape. IT IS ALL ABOUT PRESTIGE, SELF AND IGNORANCE.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2012

    Kuchangia harusi ni hiari ya mtu na sio lazima kama una uwezo dhangia utakachoweza na pia hiyo michango mnayotaka wachangiwe watoto yatima, wasiona uwezo wa kulipa ada za shule,kwani serikali kazi yake nini? Mambo ya kuchangia harusi yamekuwepo miaka na miaka labda ndoa ya mkeka,acheniwatu wafurahi na nafsi zao,mnaacha kuangalia mambo yanayokwamisha hali ya maisha kuwa ngumu,na nyie mnaozungumzia nchi nyingine kila nchi wanautaratibu wao na huku msitake kufananisha na huko,iba ,danganya,dhulumu ila ujue siku ukipatikana sheria inachukua mkondo wake,hakuna alio juu ya sheria,kama unaweza changia huna acha huo ndio utaratibu wetu wa maisha

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 07, 2012

    jamani mi sisemi sana mana nimetengwa mpk na marafiki kisa sijatoa mchango wa harusi... bongo kaazi kwelikweli

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2012

    mliomuunga mkono huyu mdau ,hamjui, uchumi. hizi tamasha ni mchango mkubwa sana kibiashara, kwanza kuna kukodi ukumbi, manunuzi ya vipodozi, chakula , viungo kariakoo n.k ni pesa hii hii unayochangishwa huenda mdogo wako muuza genge la nyanya ananufaika nayo au kaka yako mwenye ukumbi ataipata na ataitumia kumpeleka mtoto wake shule au kukupa wewe mlalamikaji ukalipa deni lako la Mark 2au wanakikao kuja seaboys restaurant kula na kufanya kijimkutano chao cha bajeti ya harusi-huu ndiyo mzunguko wa pesa jamani -nyie ndo muamuke. Seaboys Magomeni.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 07, 2012

    Mdau hapo umenena! Inapoboa zaidi ni pale unepomchangia mtu usiyemjua kabisa, kwa mfano binamu yake mshikaji wako anaeolewa!! Imekua too much, na watu wamefanya mtaji hii biashara ya michango..hii ni tabia mbaya sana ya watz, sio waa Africa. Mi nimeishi Rwanda, Burundi, South Africa, Namibia, Zambia, Zimbabwe..Huko mtu unaalikwa kwenye harusi sio mchango wako ndo ukuletee mwaliko. Ina maana hata kama ni rafiki usipokua na hela ya mchango hualikwi kwenye harusi..Shame!

    ReplyDelete
  19. Hili nalo neno, tubadilike wabongo.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 07, 2012

    MIMI NILISHACHUNGUZA,NIKAONA KUWA SISI WATZ TUNA ROHO YA KWA NINI!

    UNAJUWA MDAU NI KWA NINI WATU WANAONA BORA WACHANGIE HARUSI KULIKO KITU KAMA MATIBABU AU ELIMU KAMA ULIVYOSEMA?
    NAKUPA SABABU,,KAMA NILIVYOSEMA HAPO AWALI KUWA SISI WATZ TUNAROHO MBAYA,,MTU ANAMCHANGIA MWENZAKE LAKI 5,SIO KWA SABABU KAMPENDA SAAAANA,,ILA ANAJUWA HII PESA ITATUMIKA SIKU MOJA ITAISHA,,ILA KUMCHANGIA MWANAFUNZI,ASOME ILI BAADAE AWEZE KUWA NA MAISHA MAZURI,AU KUMCHANGIA MGONJWA ILI AWEZE KWENDA HOSPITAL APONE...ANAJIULIZA NI KWA NINI HUYU MTU AJE KUENDELEA KUISHI,,KUNA WANAFUNZI WANGAPI HATA HUKO KIJIJINI KWAO,,WATOTO WANGAPI WAMEPASS LA SABA NA HAWANA UWEZO WA KUENDELEA,,UNAONA BORA UTUPE PESA KATIKA HARUSI ILI ITUMIKE SIKU MOJA KISHA IISHE,,,
    MFANO NI HUU,ATOKEE MTU HUYO HUYO ALIYECHANGIWA LAKI 5 KATIKA HARUSI,AUMWE NA AANZE KUCHANGISHA PESA YA MATIBABU,,HA HA HA,,UKIFUTWA WEWE ULIYETOA LAKI 5,,KAMA UTATOA ZAIDI NI ELFU 20 NA TENA KWA KUBEMBELEZWA MNO,,HA HA HA YANGU MAMCHO,,KAMWE WABONGO HATUTOBADILIKA

    'PEPO YA MUNGU,KWETU ITAKUWA NI KIMBINDE'

    AHLAM,,,,LONDON

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 07, 2012

    Kuchangiana ni kutiana mizigo isiyo ya lazima. Sherehe ya harusi inatakiwa iandaliwe na bwana harusi na familia yake na sio kupitisha michango kwa marafiki. Inakera kwa kias fulani mtu anapokufuatilia na kukumbusha umpe pledge yako ili baadae aanze kukufuatilia ulipe. It's so boring kwa kweli.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 08, 2012

    Cha kusikitisha ni kwamba hata hiyo million 20 haendi kuwasaidia hao wanandoa. Yote inaishia kulipia vitu visivyokuwa na faida yoyote ya muda mrefu (mapambo, DJm MC, usafiri, ukumbi, you name it) Ukiangalia zawadi wanazopata hata maharusi kwa ajili ya kuwasaidia kuanza maisha (supposedly) hata laki tano inaweza isifike.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 08, 2012

    Mdau namba mbili hapo juu anasema ni utamaduni wetu harusi za kifahari!!?? How can you say that!?? Nimeshuhudia harusi nyingi za kifahari na maisha ya dhiki baada ya sherehe. Wanandoa wanarudi kwenye maisha yao halisi na unajiuliza mil20 walizozichoma kwa siku moja zingebadilisha vipi maisha yao, achilia mbali ya ndugu na watanzania wengine. Huu ni ulimbukeni wa wazi kabisa na yatupasa tubadilike Watanzania.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 08, 2012

    Tetetee..!
    Mimi tatizo langu kubwa ni kuwa hatuchangiani watoto wetu kuwapeleka shule,lakini tunachangishana harusi.

    Yalinikuta mimi hayo,ndugu walishindwa kunichangia kabisa nilipo pungukiwa ada ya kuja kusoma huku ughaibuni.

    Anyway it has been longtime but i am still thinking about it.Strange to me!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 08, 2012

    Huyo anayesema eti ni hairi wakati mwingine ni kulazimishana na kutuafuta kutengwa kama walivyoeleza wadau wengine. Wasomi wa sociology ana wansaikojia, wanauchumi andikeni makala naa vitabu mada hii watu wengi wapate kuelimika. Hapaswi kuonyesha hasira zetu hapa bloguni bali kwa jamii yetu! "Tubadilike" Wabongo tunahitaji kubadilishwa. Tulishazoea kufanyiwa kila kitu. Basi tusubiri Wazungu waje na NGO zao jinsi ya kuelimisha jamii. kwani mangapi wanatufanyia. Yaani tumekaa "Ki-lame lame" hata wenzetu wa magharibi wanajua hii ndio sifa ya WaTz. Ukikutana na Mzaungu aliyesafiri TZ anasema ooo Tzanians are so lame" Yaani eti ni kama makondoo. Wadau tusaidiane kubadilika.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 08, 2012

    du, mimi nilishaamua, sichangi zaid ya 30,000, na wakati mwingine nachanga elfu kumi tu na harusini siendi. ni ujinga, kama unazo changa, kama huna fanya kama mimi, ni maamuzi ya mtu kupanga kipi akipe kipa umbele. juzi kuna mama mmoja aliniambia yeye sasa hivi ana kadi 7, na huwa anachanga, na hajui hesabu ya michango yake, kisa eti ni mingi sana. bahati mbaya alisemea katika eneo ambalo waliopo wengine ni walala hoi, kila mtu akamuona mjinga.. sasa cha muhimu ni..AKILI KICHWANI

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 08, 2012

    Umenena!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 08, 2012

    Unakuta Harusi ya Kifahari gharama ya Milioni 20 wakati Wanandoa hali yao kimaisha duni kabisa!!!

    Hii haina Logic,Mtaji wala Mshiko kama mtu anapenda Ufahari ni bora angetafuta fedha zake hata kwa Mkopo Benki halafu akaandaa Sherehe na kuwaalika watukwa gharama zake mwenyewe!!!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 08, 2012

    Niliwahi kuelezwa na rafiki yangu kutoka Kenya kuwa WaTZ tunapenda kufanya harambee za harusi zaidi ya maswala ya elimu kama kujenga shule, kupeleka watoto shuleni na vyuoni nk. tofauti na wao wa-Kenya ambapo harambee nyingi huwa na mtizamo tofauti na kwetu. Sikuwa na la kusema kwa kweli

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 08, 2012

    Lakini msisahau kuwa tunakatwa pesa nyingi sana kila mwezi kama kodi toka kwenye vijimishahara vyetu vidogo ambazo tunaamini ndio zinachangia katika elimu, afya na maendeleo kwa ujumla. Suala la kuchangia harusi ni maamuzi binafsi. Wewe kama hutotaka kuchanga au ukachanga yote ni maamuzi binafsi.Zipo familia au koo ambazo zina mifuko ya maendeleo na huchangiana katika mambo ya elimu na afya pia. So ni suala la familia kukaa na kuongea na kupanga ni mambo gani wayape vipaumbele! Harusi zitaendelea kuwepo na watu wataendelea kuchanga. Ndio utamaduni wetu kuchangiana kunapokuwa na sherehe au misiba. Hii inaonyesha ya kwamba tupo pamoja na tunashirikiana na wenzetu! Ni mchango wangu tu!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 08, 2012

    MICHANGO YA LAZIMA NA HARUSI ZA KIFAHARI TUSIZOZIMUDU SIO UTAMADUNI WETU. KUISHI NI KUJIFUNZA KUNA MAMBO WANAFANYA ULAYA MAZURI YA KUIGWA MENGINE MABAYA TUYAEPUKE. HILI LA HARUSI ZA KUJIONYESHA NA UFAHARI USIO NA KIPIMO TUSILIFANANISHE NA TABIA MBAYA WANAZOFANYA VIJANA WA HUKO. MAZURI TUJIFUNZE MABAYA TUACHE. JAMANI TUBADILIKE!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 08, 2012

    wadau mwenzenu mimi yalinikuta,nilimkopesha rafiki yangu laki moja akaniambia atanilipa baada ya mienzi kadhaa mara ghafla akaniletea kadi ya mwaliko wa sendof ya binamu wake siku mbili kabla akiniambia kwamba kadi za mchango zilikwisha kwahiyo ame kompaset na laki moja yangu,hapa alimaanisha nisimdai tena kwasababu tayari amenipa kadi ya mwaliko.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 08, 2012

    Huu mwezi wa Juni nina kadi za michango kama 5 hivi Kitchen party, send off, Akdi, reception, mwingine anakwenda kuoa Tanga. of course na nauli yake na rafiki na ndugu, chakula cha huko. Mtu mkubwa mzito kanipigia ananihimiza mchango, siku zimekaribia.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 08, 2012

    Hii michango ni too much!
    Kwa nini mtu asifanye sherehe ndogo yeye na familia yake yakaisha. Anayejiweza aalike rafiki zake akitaka.
    Mbona huko vijijini watu wanfunga ndoa bila hizo sherehe kubwa na ndoa zao zinadumu.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 13, 2012

    KAMA ULICHANGIWA WEWE LAZIMA UCHANGE TU, USITAFUTE SABABU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...