Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi  akibandika stika hizo.
 Mmoja wa Madereva waliokabidhiwa Stika hizo kwaajili ya kuzibandika kwenye magari.
 Kamanda Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua kampeni ya kubandika stika zenye namba za simu za vituo mbalimbali ambazo abiria watazitumia kwaajili ya kutoa taarifa za usalama na matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani. Kampeni hiyo inadhaminiwa na benki ya posta (TPB).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2012

    Hilo ni swala muhimu kwa usalama wa raia.JE POLISI WATAITIKIA WITO WAKATI WA KUITWA KUKITOKEA UHALIFU ISIJE IKAWA KITUO KINA WATU WACHACHE,GARI HALINA MAFUTA etc hii ni Tanxania

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2012

    mimi kusema kweli as much as naunga mkono hili suala nashangaa kwanini hizo tarakimu zenyewe ziko complicated namna hiyo mbona namba hizi huwa zinakuwa rahisi universally? sasa ni kivipi mtu anaweza kunakili hizi namba zenye tarakimu nyingi namna hii?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2012

    Binafsi kwa kweli sitapenda kubandika stika kwenye gari yangu maana zimekuwa nyingi mno hata zinaweza zenyewe kuhatarisha usalama barabarani. Toeni vikaratasi tu au mtu binafsi ajitume kuzisevu hizo namba kwenye simu yake.

    Ila wazo kuu ni zuri sana i.e. wazo la kuwaripoti madereva wasiofaa japo sijui ni asilimia ngapi tu ndio watakaofikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2012

    polisi wanafiki hawafatilii haya mambo wao wanaangalia maslahi tu waliwahi kutoa namba za kila mkubwa kama kakitabu kadogo kukiwa na tatizo unawapigia hawapokei simu. Trafiki anaambiwa gari linakimbizwa anazunguka na konda au dereva anawekewa hela kwenye kadi yanaisha hawana msaada wowote hao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...