Meneja wa kinywaji cha Konyagi Martha Bangu na Mwnyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikunai Zena Khamisi wakifungua bomba la maji kuashiria uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji ambacho kimechimbwa na kampuni hiyo Mbagala Vikunai,jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kinywaji cha Konyagi Martha Bangu akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Vikunai kilichopo eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua kisima cha maji kilichochimbwa na kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Maji ni kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa eneo hili. Naishukuru kampuni ya Konyagi kwa msaada huu.

    Dkt Faustine Ndugulile
    Mbunge Kigamboni

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2012

    Hiyou sarawili ikilowana je? (kati ya mvua na jua unapenda nini?)

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2012

    Hiki isima kingependeza kama kingekuwa kinatoa kinatoa konyagi badala ya maji.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2012

    Ndo maana serikali yetu legelege kwa "wawekezaji". Kwa misaada midogomidogo kama hii basi tunabweteka. hivi kweli serikali inashindwaje kuchimba visima vidogovidogo kama hivi? Unaenda wilayani unakuta Mwenyekiti wa halmashauri na mkurugenzi wanatembelea magari kuanzia sh. 200 milioni kwenda mbele,bei ya kisima kimoja ni sh.20 milioni au chini zaidi lakini wilaya ina shida ya maji kuliko jangwani. Sasa hapo tunasema ni ukosefu wa uwezo kwa serikali kweli? Wananchi inatakiwa sasa tuwawajibishe viongozi wetu,wanatutesa sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...