Manji akiwasili Makao Makuu ya Yanga.
 Saidi Motisha akimkaribisha mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuingia Makao Makuu ya klabu hiyo wakati wa usaili
 Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji akiteta jambo na mwanachama wa klabu hiyo, Bi. Rukia Mohamed Makao Makuu ya klabu Dar es Salaam,  alikokwenda kufanyiwa usaili kwa ajili ya uchaguzi mdogo.
 Manji akiwasili Makao Makuu ya Yanga.
 Manji akizungumza na waandishi wa habari
 Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga, Sarah Ramadhani naye akiingia wakati wa usaili
 Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga,  Clement Sanga (mwenye tai) akiwa na mgombea wa nafasi ya ujumbe, Peter Haule baada ya kufanyiwa usaili kwa ajili ya uchaguzi mdogo.
 Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa yanga, Clement Sanga (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wanachama wa Yanga baada ya usaili
 Manji akiondoka baada ya kufanyia usaili na kamati ya uchaguzi.
Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2012

    Haya bwana mwenye pesa mpishe....

    ReplyDelete
  2. Somebody has to care of other people!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2012

    Pesa mwanaharamu! Kwa kihaya wanasema ekyalema amahera, naga. Yaani kilichoshinda pesa, tupa mbali...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2012

    KWELI MWENYE PESA MPISHE HUYO MANJI KISHAPITA ANGALIA ALIVYO POKELEWA NA HUYO MDADA MGOMBEA MWENZA ALIVYO POKELEWA NA WATU WAMEISHA CHORA MCHONGO HUYO SAIDI MOTISHA JINA LAKE SAIDI KONGOGO ANAJUA SASA MANJI ULAJI HUO NA HUYO MDADA KAKATIWA KITU KIDOGO NA MANJI AJE ONYESHA SURA KWAMBA MGOMBEA MAMBO YAPO PALEPALE ARKKAUNUL ISLAM HAMSAT HAIFUTIKI HATA MARCIMO ANAERUDI ENDELEZA BIASHARA YA BRAZIL NA AKINA MANJI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2012

    Kaka yangu Yusuph Manji
    Nakujua wapenda sana klab yako!! Ningekushauri ungeachana na kugombea hiyo nafasi kwani kwa uelewa wangu unachokifanya ni kutafuta kushushiwa heshima tu mambo yatakapokwenda mrama! Wewe kaa nje kama mfadhili au ugombee nafasi ya kuwa mtu mashuhuri tu hapo mtaa wa Twiga vinginevyo yetu macho!! wengine hutolewa kwa bakora!!Je upo hapo!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2012

    Inasikitisha. Yaani kabisa mtu mwenye akili timamu anagombania nafasi ya kuongoza Yanga ama Simba?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2012

    Manji hagombei uenyekiti yanga, anagombea nafasi ya kuidai yanga pesa nyingi kijanjajanja halafa ainunue kwa bei ya bure! subirini muone!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2012

    Bora Yanga inunuliwe na Manji iwe Kampuni binafsi badala ya kuwa kama Tawi la Chama ambapo Wazee na watu wa njaa kali wanaitumia kama SACCOS !

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2012

    Manji umekosea kitu kimoja tu!

    Ziara yako hapo Klabuni Jangwani ungewapanga watu kwa sinia za pilau uone vile watu wangekanyagana!

    Ohoooo, hivyo Vizee na vibandiko vyao na hao Masela wangetafuta mifuko ya Rambo kuwekea ubwabwa!

    Shaba/Ubeche mchezo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...