Katika Gazeti la Mwananchi la tarehe 16/5/2012 kulikuwa na makala iliyonakili ushauri wa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Kayanza Pinda akizishauri bank zitoe mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima. Alizitaja changamoto ambazo zinawakabili wakulima kwa kusema ‘"Wakulima wadogowadogo wanashindwa kupata mikopo ya kutosha kwa sababu benki za biashara zinawatoza riba kubwa na kuhitaji dhamana (collateral) alisema Mh Pinda.
Mh Pinda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hotuba  iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Kilimo Vijijini Afrika (Afraca).
Malengo hasa ya kuandika makala hii ni kujaribu kuishauri serikali na wananchi kwa ujumla jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo kwa kutumia taasisi nyingine za fedha kama vile bank za kiIslam. Kwa upande mwingine tunapenda kuzishauri bank za kiislam kuanza kufikria uwezekano wa kutoa huduma hizo kama bado kwa sasa hazipo.

Tukianzia na tataizo la riba (interest), ni dhahiri kua riba ktk mazingira yake yote ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Matatizo ya riba yalishaelezwa na bado yanaendelea kuelezewa, na kuthibitishwa na wataalam wengi wa kiuchumi duniani, kwa mfano hivi karibuni mkuu wa shirika la fedha la kimataifa  International Monetary Fund (IMF) Christine Lagarde  aliishauri serikali ya Uingereza kupunguza  kiwango cha riba mpaka ifikie sifuri, alinukuliwa akisema “BRITAIN should consider cutting the interest rate to ZERO if the economy continues to struggle, the International Monetary Fund believes”). The Sun 23 may 2012.  Maneno ya Miss Lagarde yaliungwa mkono na wanauchumi wengi kwa kesema  “Cutting rates from 0.5 per cent won’t be the solution on its own, but would send out the right signal.”

Kwa upande wa bank za kiislam, tungezishauri zijitokeze kuwafahamisha wananchi na wadau mbali mbali kua ziko njia mbali mbali zinazoweza kutumiwa kuepuka riba, na wakati huo huo kuleta ufanisi katika nyanja mbali mbali za kiuchumi, jamii na kadhalika. Ukweli ni kwamba bank za kiIslam zina uwezo wa kuwasaidia wakulima kwa kutumia mifumo ya uchumi ambayo inakubalika kisheria kama vile murabaha, mudarabah, muzaarah, musaqaat na nyinginezo ambazo zimeelezewa kwa ufasaha kwenye www.ijuebankiyakiislam@blogspot.com.
 Tukitolea mfano kwa kutumia mfumo wa murabaha, bank inaweza kuwapatia wakulima vifaa na mahitaji mbali mbali   kwa masharti ya kulipa  hapo baadae pamoja na faida. Mrabaha maana yake ni bank au mwenye uwezo, kumnunulia asie na uwezo kitu fulani kwa masharti amlipe kwa faida maalum hapo baadae, kwa mfano bank inaweza kuwanunulia wakulima  vifaa mbali mbali vya kilimo kama vile matrector, mbegu na mbolea, kisha ikawauzia  kwa faida maalum  kwa masharti walipe hapo baadae. hapa inaonekana wazi kabisa kua murabaha unaweza kuwasaidia wakulima wakaweza kujikomboa na kujitegemea hapo baadae.

Wasi wasi mwengine ni ule unaohusiana na dhamana (collateral) kutoka kwa wakulima kutokana na uhakika kwamba wakulima wengi hawana mali ambazo wanaweza kuzitumia kama dhamana ili bank ziweze kuwapa mikopo. Hilo nalo linaufumbuzi wake, kwa mfano bank za kiislsm inaweza ikatumia kitu kinachojuikana kama ‘group-based lending approach capitalising on peer monitoring and guarantee mechanism’ ambayo ni utaratibu wa kufanya biashara kwa vikundi ambayo hiyo inaweza kuwa mbadala wa dhamana kwa mtu mmoja mmoja.
  
 Ushauri kwa serikali ya Tanzania
Kwa upande wa serikali, tunapenda kuishauri ibadilishe njia (approach) katika kilimo na wakulima kwa kuweka mipango madhubuti ya mabaliko katika maeneo mengi ya vijijini kwa kujenga miundominu. Ni ukweli usiopingika kua wakazi wengi wa vijijini wanapoteza haki zao za msingi kama vile elimu bora, matibabu ya uhakika, na kadhalika.  Ukiangalia  umuhimu na mchango wa mkulima katika mataifa yanayoendelea  utakuta kwamba wakazi hawa wanatakiwa wapatiwe mahitaji muhimu kama vile barabara safi, vituo vya elimu, afya na miondombinu mengine.  Kwa kua wakazi wengi wa vijijini ni wakulima, serikali  pia inatakiwa iweke mipango madhubuti ya kuinua kilimo  kwa kuwapatia wakazi hawa wataalam,ujuzi na mahitaji mengine.
Pamoja na mambo mengine hotuba yake Mh waziri mkuu  iliziasa bank kuwafikia wananchi huko vijijini, hili ni suala muhimu kwani mabank mengi yamejikita sana mijini na kuwasahau  kwa kiasi  kikubwa wakazi wa vijijini.  Wataalamu  wengi wa kiuchumi wanadai kwamba suala la faida kwa mabank ndio sababu ya mabank haya kutokupeleka huduma vijijini,  suala hili limesababisha wakazi wengi wa vijijini kukosa huduma za kibank mpaka waende mijini kitu ambacho kinawagharimu sana. Kwa upande mwengine uchunguzi wa mambo unaonyesha kua wakazi wengi wa vijijini hawana bank accounts, kitu ambacho kimesababisha ugumu sana kwa wakazi hao kuaminika kupata hata hiyo mikopo yenye riba nafuu.
Maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwasaidia wakulima na kupambana na changamoto zilizopo yataelezewa kwa ufasaha na kila moja itatengewa sehemu maalum kwenye www.ijuebankiyakiislam.blogspot.com  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2012

    Kaka asabte sana kwa ushauri wako mzuri.Ila subir kesho wale jamaa zetu waende kazini wakatumie computer na internet za serikali km mali zao waanze kuja kuosha vinywa hapa.Leo ni kimya kwa sababu ni weekend lkn subir kesho j3 utawaskia tu watakavyokuja na hoja za kitoto hapa.Hawa jamaa sijui kawaroga nani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2012

    Shukran sana kwa kutupatia information hizo na tutajaribu kuwasiliana na hizo bank tuone kama hizo huduma zipo

    ReplyDelete
  3. Rahim AbdulJune 24, 2012

    Very interesting and informative article thanks. I'm told there are Conference on The role of Interest free financing at Karimjee on 15th July, 2015. Someone should present this interesting news......!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2012

    Hoja ya mdau kuhusu benki za kiislam na wakulima: MICHUZI(24/06/2012°
    kwanza namshukuru mdau kwa kuelewa benki za kiislam, baada ya hapo naomba niseme kwamba benki za kiislam bado hazina uwezo Tanzania kutokana na mfumo wa kibenki uliopo, japokuwa zinapatikana baadhi ya huduma za islamic banking kupitia benki nyingine.Hii ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:
    soko la kibenki tanzania ni la riba hivyo basi benki za kiislam zitapataje Mkopo kabla hazijatoa mkopo? maana riba ni haram
    Pili ni kwamba benki za kiislam huwa zinakagua kwanza project yako kabla hazijakupa mkopo!Hii inamaanisha kwamba lazima uwe hai kabla hawajakupa pesa.
    Tatu islamic banking banking haifadhili shughuli zote zile za kilimo zinazoendana na mapato haram mfano tumbaku.
    Nne ni kwamba benki za kiislama ni benki za kugawana faida.hivyo kutokana na uwingi wa jamii yetu ni mabepari hivyo jamii nyingi hazipendi kugawana faida hasa wawekezaji wa nje walio nchini

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2012

    Mdau wa Sun 24 11:56 Nadhani bado unahitaji shule kuhusu Islamic Banking... Kugawana faida sio msingi wa Islamic Banking, Ila Islamic banking huwa wanakuuzia bidhaa kama dukani na wao huwa wameweka profit margin yao.
    Pia ishu ya lazima uwe hai ili ukope nadhani hilo halihitaji maelezo ya nguvu sana unawezaje kukopa ukiwa umeshakufa? wao lazima waangalie project husika ili wajiridhishe kuwa sio project haram ambazo madhara yake kwa jamii ni makubwa kuliko faida

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2012

    Kwa uelewa wangu benki za kiislam nazo zinaangalia zinamkopesha nani. Sasa na hiki kilimo chetu cha jembe la mkono na mvua za kupima kweli wa benki watatoa kitu kweli?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2012

    shukran kwa wote walioshiriki. Kwa wale ambao wameonyesha wasiwasi kuhusu bank za kiislam kushiriki ktk biashara haramu au kwamba lazima mshiriki awe hai, majibu ya wasiwasi huo yatajibiwa kwenye sehemu ya maswali na majibu ktk blog yetu www.ijuebankyakiislam.blogspot.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...