Mbunge wa jimbo la Ubungo,John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania mjini Dodoma leo baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya viwanja vya Bunge la Tanzania mjini Dodoma leo baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo mara baada ya kuondolewa Bungeni mjini Dodoma leo baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya viwanja vya Bunge la Tanzania mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2012

    unakoma kichwa siyo shauri yako hii ndo bongo mzee usitake umarufu wa kipuzi puzi shauri yako kwani ungemuomba samahani ungekufaaa kula nao sahani mmoja halafu wewe katika akili yako unajua nini cha kufanya ndo inavyokwenda kijana kadogo kadogo shauri yako

    ushauri wa bure kutoka kwa fisadi

    U.K

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2012

    watanzania tupo wapi hata kufikia kutokuwa na nidhamu na viongozi wetu sina la ziada kwa kuwa muheshimiwa rais umetupa uhuru kupindukia na ndugu zangu wa islamu wana msemo mmoja kuwa ukicheza na mbwa utaja ingia neye msikitini ndio haya sasa. mdau wa ughaibuni

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2012

    CHADEMA munachojua ni kutukana watu kupata umaarufu.Basi na wewe Mnyika kwa kutafuta cheap publicity unamtusi Rais wetu.Tunasema CHADEMA kimejaa watu tamaa ya ubinafsi ndio muone.Kichwani mwake alitegemea atapata umaarufu .Siasa ni busara si matusi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2012

    sasa ss tunapenda vijana sana lakin sas kwa mwendo huu wanatuibisha yeye kasema wabunge wenzake ni machizi,rais mdhaifu na mawaziri ni wajinga lakini mwisho wa yote jambo ambalo alikusudia kuongea hakuongea kushauri bajeti kwa sisi vijana tukosa pointi za mheshiwa huyu kwa lugha yake ya matusi na ukaidi usiyo wa lazima vijana wenzangu tunaitaji mawazo yenu zaidi ili bunge lipate heshima kwa mwendo sijanda hii motion.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2012

    Tafadhalini sana tunawaheshimu, uhuru wa kuongea unavuka, Rais wetu mnamtukania nini?..

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2012

    Duh, aibu gani sasa hii jamani! Wala siyo ushujaa kuwa mtovu wa nidhamu, badala yake hiyo ni ishara ya ukatili na ukosefu wa uvumilivu kwa wenzako. Hapo ni Bungeni na Kanuni zinazuia lugha ya maudhi. Rais ni Kiongozi wa nchi, sura ya nchi, utamtamkiaje hayo kisha ukumbushwe, kama ulipitiwa, ukatae hata kufuta kauli / lugha ya maudhi.
    Hata kwa mila zetu tu, huyu Mhe. Mnyika ni kijana mdogo sana hata kwa umri. Hata kama angekuwa wa umri wa Rais, hayo humtamkii Rais, tena ukiwa BUNGENI.
    Nadhani sasa isitoshe tu kumtoa Bungeni, Kanuni zianzishe FAINI kwa baadhi ya makosa ukumbini ambapo Mhe aliyekosa atalipa FAINI.
    Ah, aibu jamani!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2012

    hivi neno "dhaifu" ni tusi? unapoenda interview watu wanaulizwa weaknesses(udhaifu wao) zao, kumbe huwa wanatukanwa! Mie naamini kila mtu ana udhaifu wake, kwa nini hatupendi kuambiwa udhaifu wetu?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2012

    wote hapo juu, hakuna mwenye point-yenye kuonyesha -hata kuandikwa kwenye blog, lakini kwa vile Michuzi habagui-basi twende tu-ni msafara wa mamba huu ,konokono, kenge, vyura,kobe wote wamo !!!! Point, Mnyika hakumtukana rais,kamuita mdhaifu. Binadamu siye wote tunamapungufu,uwe rais,uwe waziri,uwe Mnyika, uwe wewe mtoa maoni. Cheyo cha kuwa raisi wa nchi,hakimbadilishi mtu kuwa tofauti na binadamu mwingine. Mnyika aligusia mapungufu ya rais au kwa kiswahili kingine madhaifu ya rais. ( weakness of our leader or leaders. Sasa jamani kosa liko wapi hapo ???? na si lazima kufuta kauli wakati ,unaona kwamba uko na haki ya kutoa maoni. Msikimbilie kuloloma tu, STOP AND THINK.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2012

    dungu zangu.
    lazima tufikirie kwa jicho la tatu, zaid wakati tunatoa maoni yetu. Japo Mnyika katoa lugha mbaya, jee mantiki yake inaukweli au la! Maoni mazuri ungeshauri kifanyike nini au kudadafua logic behind.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2012

    Inabidi wananchi wafahamu kwamba huyu kijana hajatukana ila kwa tafsiri ya CCM ambayo rais ni mweyekiti wao, mbunge wa upinzani akiongea ukweli bila kuwa mnafiki na kuuma maneno ni dhambi. Hiki ndicho kimetokea, suala la ujana halina mashiko ktk hoja ya msingi. Kwa waliofuatilia bunge maneno waliyosema wabunge ya CCM mmeyasikia na baadae wakapongezana, mbona hawajatolewa nje? kuna kudhalilisha kuliko maneno yale?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2012

    nadani hajakosea huyu kijana wa chadema, ila kasema kweli kuwa rais wetu ni dhaifu sana labda kwa maneno mengine mnyika angesema tu rais amekuwa mvumilivu kupita kias ambayo bado ni yaleyale udhaifu maana chochote kinachozidi ni hatari. uvumilivu na udhaifu huo ndio huohuo uliosababisha hadi vijana wadogo kama mnyika kumdhalilisha hadharani...
    rais anacheka na mafisadi, matajiri lakin walalahoi anawafariji kwa maneno na mafisadi anawaogopa kuwaambia warudishe mali za umma walizoiba...

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2012

    This man is out of order,suspend him for the whole week and no allowance for the whole entire month then he will learn to respect other people idiot.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 19, 2012

    Jamani, kasomeni kwenye kamusi nini maana ya neno dhaifu, kutolewa nje kwa Mnyika ni zaidi ya kutamka rais yu dhaifu, tusihukumu haraka, mpaka aamue kukataa kufuta kauli lazima anasababu za msingi, amejenga hoja yake vipi?, swala umri kwamba ni kijana mdogo sidhani kama ni sahihi, maana kuna wazee wengi tu ambao wana mawazo mgando..wasiambiwe kwa sababu ya umri tu?? cku hizi hata mzazi akikosea huambiwa tofauti na zamani, maana hata mzazi ni binadamu!!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 19, 2012

    Neno DHAIFU sio tusi, labda angeeleza udhaifu wa Rais ulipo. Pili, ni wakati muafaka kwa jamii kuona aina ya wabunge na tabia zao kwa faida ya mbeleni....!

    Lakini haitoshi tu kumnyoshea kidole Mnyika juu ya kauli hii, bali pia ni wajibu wa watu wanao mshauri Rais kutathmini kile kinachopelekea watu kusema ni mdhaifu. Ijapo siyo Mnyika tu aliyewahi kutoa kauli hii, pengine hatua MUAFAKA zisizozingatia nafasi ya mtu kifedha au kiwadhifa ktka jamii, na kwa wakati.

    Mfano; Wauza madawa ya kulevya tunawajua na majina tunayo, waache kufanya hivyo. Au, wote waliochukua fedha za EPA warudishe kwa hiari yao..na hakuna hatua za kuchukuliwa dhidi yao...! Wezi walio magerezani leo wakirudisha walivyoiba, watakuwa free?

    Kauli hizi hukanganya sana hata kama kuna hatua muafaka huchukuliwa chinichini....bora zisitamkwe.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 19, 2012

    JAMANI ALICHOTUKANA MNYIKA NI KIPI
    WATANZANIA LAZIMA TUJUE MTU AKIINGIA KWENYE SIASA LAZIMA YOTE HAYA AYAKUBALI;KWELI KABISA ALICHOSEMA MNYIKA RAIS ANAWAJIBIKA MOJA KWA MOJA ,KAMA WASAIDIZI WAKE WAZEMBE NAYE NI MZEMBE
    HONGERA MNYIKA USIOMBE MSAMAHA NGO TUKO PAMOJA NAWE

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 19, 2012

    Hawa vibaka wamesha jiona ni dola tayari ndio maana. Wataendesha nchi kweli kwa mtaji huu ? Kumtusi mkuu wa nchi ni kutusi nchi yako,dunia inatucheka watanzania.

    ReplyDelete
  17. Ukweli sasa tunaelekea kubaya dah kaka mnyika kaa chini uangalie sii vizuri jaman

    ReplyDelete
  18. Acheni mambo ya ajabu nyinyi, Rais kuambiwa mdhaifu nalo ni tusi??hivi mnafatilia bunge au mnalopoka na maneno aliyoandika michuzi, Michuzi mbona wabunge wa CCM wanawatukana Wabunge wa Chdema na huweki?Fanya kazi yako na acha mambo ya kishamba michuzi, najuwa hii comment utaiweka kapuni lakini uwe unaandika kila kitu na sio kushobokea sehemu yenye maslahi yako, Rais kuambiwaa mdhaifu leo imekuwa kosa neno mdhaifu ni la kudhalilisha?Watu wengine bana, Makinda subiri tu endelea kufanya mambo ya ajabu ajabu 2015 sio mbali.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 19, 2012

    JAMANI NDUGU ZANGU MIMI NACHUKULIA KAULI HII YA MNYIKA KWA MTIZAMO MDOGO TU NAFIKIRI NI JAZBA LILIMJAA HUYU KIJANA MPAKA AKAFIKIA KAULI YA KISEMA VILE NA KWA AKILI YA KAWAIDA TU UKIWAZA NI KWAMBA KILA MWANADAMU HAPA DUNIANI ANA UZAIFU WAKE HAIJALISHI NI NANI HIVYO KWA KWELI KAMA MNAKUMBUKA KUNA KAULI INAYOSEMA HAKUNA ALIYE MKAMILIFU INA MAANA KWAMBA KILA MTU ANA MAPUNGUFU YAKE NAOMBA SANA MUELEWE MSIPENDE KUONGEA MANENO MENGI AMBAYO YATAMFANYA KUMKASIRISHA MUESHMIWA RAIS, KWANZA MIMI KAMA MIMI NAMUONA MUHESHMIWA ANATUMIA HEKIMA ZA HALI YA HALI YA JUU SANA NA NDIO MAANA HATA DOGO JANJA ALIPOSEMA ANADAI NCHI YA MERU MUHESHMIWA RAISI ALIKAA KIMYA KWA SABABU YA UELEWA WAKE KUNA WATU WANAWEZA KUTUMWA KUKUCHOZA ILI ULIPUKE NA UKISHALIPUKA SASA HAPO NDIO WANAANZA KULETA YALE WALIOYATAKA MIMI BINAFSI NAMPONGEZA SANA MUHESMIWA RAIS KWA HEKIMA ZAKE ZA UTULIVU HASA KATIKA VUGU VUGU HILI LA UHURU WA VYAMA VYA SIASA KAMA BWANA MNYIKA KAMUITA MHESHMIWA RAIS ANA MAPUNGUFU KWA KAULI HIYO TU INATOSHA KABISA PIA KWA MNYIKA KUONEKANA ANA MAPUNGUFU BIBLIA INASEMA TOA KWANZA BORITI KWENYE KIBANZI CHA USO WAKO KABLA KUONA CHA MWENZAKO,NDUGU ZANGU WANASIASA TUACHENI MATUSI TUJITAHIDI SANA KUJENGA NCHI NA KUWAPA WANANCHI MAENDELEO, SWALA LA BAJETI LIMEZUA MJADALA MKUBWA SANA NCHINI KULIKO BAJETI ZILIZOPITA MIMI KWA MAWAZO YANGU NINGESHAURI BAJETI YA NCHI IHUSISHE WACHUMI WA NCHI HII NA BAADHI YA WACHUMI HAO WATOKE KWENYE VYAMA VYOTE VYA SIASA NA WAWE NA KIKAO MAALUM AMBACHO KITAFANYIKA KWA MANUFAA YA NCHI HII NA WANANCHI WAKE LAKINI KWA KWELI MAAUMUZI MAZITO KAMA YA BAJETI KUFANYIKA TOKA KWA CHOMBO KIMOJA CHA SIASA KINAWEZA KIKAWA NA MAPUNGUFU YA KIBINADAMU MTU MMOJA AU WAWILI KUAMUA BAJETI YA NCHI NZIMA SIO KAZI NDOGO JAMANI,
    KWA MAONI YANGU KWENYE BAJETI HII MISAMAHA YA KODI INGELENGA KWA TAASISI MUHIMU KAMA VILE SHULE, MISIKITI , KANISA, MAKAMPUNI YA UTALII PIA YANGEENDELEA KUPATA MISAMAHA HII YA KODI KWANI WANAPOKWENDA NJE YA NCHI MARA NYINGI HUWA WANAITANGAZA NCHI HII NA FAIDA INALETWA NCHINI HAPA TOFAUTI NA IDARA ZINGINE HILO WANGELIANGALIA KWA MAPANA ZAIDI,UKIJA KUANGALIA KWENYE UPANDE WA MATUMIZI SERIKALI INGEZUNGUMZIA PIA NAMNA YA KUBANA MATUMIZI KWA IDARA ZA SERIKALI NA TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA, SEHEMU YEYYOTE DUNIANI UKITAKA KUJENGA UCHUMI LAZIMA KUZALISHA SANA NA KUTUMIA KIDOGO , PIA KUANGALIA UNUNUZI AU MATUMII YA MAGARI YA KIFAHARI TUNGEWEZA KUSAVE SANA KAMA KILA MBUNGE ANGEPEWA GARI JIPYA KABISA LA BEI NZURI NA LITUMIKE KWA MIAKA 8 NDIO LIRUDISHWE SERIKALINI LIUZWE FEDHA ZIONGEZEWE APEWE LINGINE JIPYA, WATANZANIA WENZANGU TUIMBEE SANA NCHI YETU NA TUWAOMBEE SANA VIONGOZI WETU WALITUMIKIE TAIFA KWA MOYO WA UPENDO NA UZALENDO.

    KIPEPEO

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 19, 2012

    John Mnyika uwe kidogo na Heshima hata kama unagombania uhuru wa maneno ila kuwa na Heshima alafu hawa Chadema wanaharibiwa sana na HAMAD RASHID MOHAMED huyu jamaa anawaharibu Chadema wanamuiga sana mawazo yake ndomana Seif Hemed hakuwa anafuata upuuzi wake.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 19, 2012

    Alichosema ni sahihi, kwani raisi wetu ni dhaifu asingekuwa dhaifu tusingeweza kumsema hadharani. Hata mawaziri wake wanajua kuwa nibonge la dhaifu ndo maana wakurugenzi, mawaziri n.k wanatafuna pesa zetu harafu anawachekea au wanamrushia kidogo. Hongera mnyika umesema kweli. Wabongo bwana akiambiwa ukweli eti hana nidhamu, kwani haya kasemea marekani si ni humuhumu bongo?sasa aibu iko wapi? Aache udhaiifu aone kama atasemwa. Hongera dogo,,,,, wachane

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 19, 2012

    deni lataifa linakua hali yamaisha inazid kua mbaya halafu mnataka watu wanyamaze eeh! Tatizo lenu mkiambiwa ukweli mnaona mmetukwana, kipi kibaya alichosema mhe. Mnyika? Natumaini hili Jk atalichukulia kama changamoto,huyo ni mnyika tuu aliyeonyesha hisia zake ogopa sana waTz nawao wakiinuka kuonesha hisia zao.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 19, 2012

    Hmm! kazi kweli! ndo mana watu wanachagua watu wenye heshima zao bungeni wanaojua kuongea vzuri mbele za watu!! mlienda kuchagua wahuni hawajaelimika hata kdogo wanaanza kurusha matusi hadharani!!!!!!!!mpeni heshima zake RAIS!!!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 19, 2012

    Kama Rais ni dhaifu ni dhaifu kwa sababu yeye ni Rais asiambiwe matatizo yake..na nyie kuweni na busara....Rais ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote anavyoweza kukosolewa..angalieni wenzetu majuu ndio maana wanaendelea kwa kupeana ukweli no matter wewe ni Rais au Spika

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 19, 2012

    That is the true color of chadema. wenye macho muone.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 19, 2012

    Nadhani ni vyema na haki kwa hili kwa kuwa hao hapo juu wanaolaumu na ndio hao hao wanazidisha umaskini kwa mtanzania. Mtu kasema kitu cha ukweli kwa kuwa mafisadi ni wengi basi wanaona ni vyema kusapport na zaidi wanapiga piga makofi bungeni, inakuja siku hata hizi lawama mnazitoa hapa juu mtashindwa kuziandika kwenye pc zenu mtakavyoona mambo yanaanzia bungeni hadi huku mtaani. NAWAPA WARNING HIYO

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 19, 2012

    MTASEMA SANA, ACHENI WATU TULE NCHI, NYIE MAGARI YANAWAHUSU NINI BWANA, LANDCRUISER MOJA BOSI MMOJA NA DEREVA WAKE, ACHENI KABISA, CHA MSINGI OMBENI NANYI MUWE MABOSS, KAMA UKILIKATAA SHANGINGI, TUTAJUA KWELI WEWE MPENDA NCHI.

    wANAAJIRIWA VIJANA WADOGO, WANAPOFIKA TU MAKAZINI, WAKIPANDISHWA VYEO NA KUWA MABOSS, WANAPEWA MASHANGINGI NA HAWASEMI LOLOTE, SEMA WEWE AMBAYE NI MGANGA NJAA, MANENO MENGI YA NINI

    UKIPATA TESA, UKIKOSA JUTIA, MTACHONGA SANA, BAJETI NDIO HIYO NA ITAPITA, POSHO POSHO, MAGARI MAGARI, HAISAIDII, NYIE WADANGANYIKA FUNIKENI MWANA HARAMU APITE.

    PIA KIJANA ANAJAZIBA, NDIO ANA UCHUNGU NA NCHI YAKE, ILA RAIS NI RAIS, LAZIMA IWEPO HESHIMA, HATA BIBLIA INASEMA WAHESHIMU BABA NA MAMA YAKO, KAULI MBOVU AU YA KUSHUSHA HADHI NI TABIA MBAYA

    fIKIRIA ANGEKUWA BABA YAKO RAIS HALAFU ANAUDHAIFU JE UNGEMWAMBIA BABA WEWE NI DHAIFU?

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 19, 2012

    Ndio maana Wazungu wanasema waafrika hatuna akili. Udhaifu kila mtu anao.

    Manake mlitaka asema Rais ni "Almighty?" Yaani Mwenye enzi? hiyo ndiyo ingekuwa ni kufuru.

    Hakuna mtu asiyekuwa na udhaifu. Sema udhaifu unatofautiana.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 19, 2012

    NILIJUA TU KUWA VIBARAKA WA CHADEMA WATALITETEA HILI LA MNYIKA LAKINI KUMBUKENI KUWA BUNGE SIO SEHEMU YA MIKUTANO YA SIASA PALE PANA KANUNI ZA UENDESHAJI WA BUNGE NDIO MAANA MNYIKA AMEPATIKANA NA HATIA YA UVUNJAJI KANUNI HIZO WALA SIO SWALA LA KUSHABIKIA KAMA ANGELIKUWA KTK MKUTANO ANGEWEZA KUKASHIFU ANAVYO WEZA AU KAMA ALIVYO SEMA EBU WABONGO TUPANUKE KISIASA NA KUTOFAUTISHA NA SHUGHULI ZA BUNGE- mdau bongo

    ReplyDelete
  30. Nina maswali mawili ya msingi kuhusu hili,1.Mnyika anawakilisha nani bungeni 2.uwakilishi wake unalenga nini.

    1.uwakilishi wa mnyika unakusudiwa uwe wa wananchi na hasa wa jimbo lake la ubungo..tunayo matatizo mengi ubungo ambayo hayajafanyiwa kazi...barabara mbovu,hudma za afya maji,na mengine mengi hayaendi...Tulitarajia ajue au awe na utambuzi uwakilishi wake unaweza usiwe na tija pale anapokaidi amri ya Spika...ili awsilishe alichotaka kukiwakilisha...kwa mwenye uelewa wa haraka hapa unasemnaje juu ya busara ya huyu kijana?

    malengo ya uwakilishi.
    Ukiwa mpinzani haina maana uwe na lugha chafu matusi au kutafuta sababu za kuandikwa kwenye magazeti....au kuyateka mawazo ya wengi wetu tunaofuata mkumbo bila kuangalia mambo kwa kina.Uwakilishi unaangalia tatizo pendekeza suluhishi na fuatilia katika yale mapendekezo,,,omba kuhusishwa.
    Walio na nchi ni hawa jamaa wa CCM hakuna namna ya kwenda nao kihuni kwani hekima inaweza kuwaondoa.
    Mnyika amekosa heshima mbele ya baba yake na anashindwa kukiri...huu naita uhuni.Vijana wenzangu tujiepushe na tabia kama hizi.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 19, 2012

    mimi naunga mkono kikwete ni dhaifu. Najua michuzi kwa kuwa wewe ni mtu wa CCM utaichunia hii message yangu kwa kuwa unaogopa kumwaga unga..

    ReplyDelete
  32. "mtu mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu harafu anajua unajua ni ya kipumbavu ukiyakubali anakudharau, ukayakubali anakudharau" J.K Nyerere...

    Still I won't change my altitude due to what you write, Mnyika you are Jembe! Your the best man! Keep it up!

    Can't wait to see you again talking with confidence in explaining the strong/hard/difficult stuffs of this nation...

    Now I believe the formula of 1 from CHADEMA=200 in CCM, need a prouf? Few days passed a member of parliament spoke the same thing in different language!

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 20, 2012

    Tutakwepa kusema ukweli mpaka lini jamani? Neno "udhaifu" limekuwa tusi tena?! Kwa maoni yangu, suala la "kudhalilisha bunge" au "kudhalilisha kiongozi fulani" linatumipa kupitiliza. Wengine husema it is being overplayed!
    ZAma za nidhamu ya woga zimekwisha. Huu ni wakati wa kukubali kusikia ukweli wa mapungufu ili kuweza kuyakabili. Ni UKWELI kwamba Mheshimiwa Raisi anao udhaifu. Mkisema tusiuzungumzie mnatukosea haki ya kujirekebisha kwa maendeleo ya nchi. Mheshimiwa Mbunge Mnyika hajamtusi rais!

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 20, 2012

    Anonymous said...
    Unafiki ndio unatusumbua. sasa hapo tusi likowapi? TZ tunataka kufanya watu fulani kuwa miungu watu. Bila kuwa wakweli na kusema moja kwa moja nchi haitapata maendeleo hata kidogo.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 20, 2012

    mnyika kwa mtazamo wangu namuona ni mtu anayetafuta umaarufu kwa nguvu,mwangalie zitto huwa anajipanga kwa kauli zake na hoja zinazoconvice pande zote chama tawala ata upinzani,hana tofauti na mbunge mpya wa arusha wa chadema,PAPARA,SIFA ZA KIJINGA NA VIHEREHERE VINAWAHARIBI

    ReplyDelete
  36. Alichokisema mnyika ni sahihi kabisa, kwani hatuelewi maana ya neno dhaifu jamani? hapo nayetakiwa kuwemwa na ndugai na lukuvi, kozi wanashabiakia mamabo ya ajabu yanayozungumzwa na ccm ila ya upinzani wanadai yako na matusi? hivi mnayajua matusi? Nendeni shule mkasome kiswahili vizuri

    Nawaomba haki za binadamu kama wanalifatilia bunge vizuri nao watusaidie kwakweli namshukuru mungu ili bunge nimelifatia vizuri sana, Mnyika uko sahihi kabisa.

    Ndugai 2015 ndio mwisho kwako, na utakuja kuniambia sisi wanaichi wako wa kongwa hatunaimani na wewe kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...