Ankal habari za leo.
Naomba unipelekee shukrani zangu kwa wasomaji wetu wa blogs za wabongo, na hasa hii yako.
Asanteni sana watanzania wenzangu na hata wale wasio watanzania lakini wanafuatilia habari za blogu hii, na zile nyingine za kiswahili, labda kujifunza zaidi lugha yatu ya kiswahili au pia kufahamu nini wazungumza kiswahili "maridadi" watanzania wanaendelea vipi katika kujuzana hili na lile kupitia mitandao ya jamii.
Hakika inapendeza sana kuona maendeleo yetu kama watanzania na Taifa kwa ujumla. Lakini pia katika kukikuza na kukipenda kiswahili chetu.Picha ni sehamu inayonogesha pia habari hizi na mtandaoni.
Kuna mambo mengi najifunza kutoka katika habari za mtandaoni hasa kupitia blogu hii ya bwana Michuzi, mzee wa libeneke. Nimekuwa nikimwambia katika hali ya utani kuwa blogu yake inafanana kama vile ina"Operate" kama iko Washngton DC, au Pentagoni, kule US. Habari zinatufikia kupitia blogu hii kutoka pande karibu zoote za dunia hii na mabara yote. Bwana Michuzi nasema Bravooo!
Watanzania, hata sisi tupo na sasa watatuheshimu wale wanaodhani kuwa kiswahili hakikui, nafahamu sasa kuna habari nyingi tu kupitia mitandao yetu kutoka hapo nyumbani Tanzania. Haya ndiyo maendeleo nini tena cha zaidi? Ndiyooo!
Lakini kabla sijasahau kusema kilicho nisukuma kuwashirikisha wasomaji wa blogu hii ni kuwa, Leo hii pamoja na habari nyingine nimefurahishwa sana na kuguswa na SHAIRI la bwana Mroki Mroki maarufu kama "Father kidevu" mtanzania kutoka pale kinyenze, mji kasoro bahari, Morogoro.
Shairi lake ni kutoa jibu kwa shairi lililokuwa limetangulia kutolewa na mshairi mwingine aliyejitambulisha kama ndugu Mwamgongo akielezea dukuduku lake kuhusu watu wa takwimu kutoa nafasi kwa mambo ya dini katika sensa za mwaka huu.
Wakati nikisoma mashairi yote mawili kupitia blogu hii, nilikumbushwa mshari maarufu aliyevuma sana naniliye msoma nikiwa shuleni pale shule ya Bihawana, sio ile seminari, la hasha ni ile ya serikali. Miaka kadhaa sasa na bado hata sasa bado tungo zake za kishairi ni somo tosha.
Huyu si mwingine bali ni mzee Shaaban Robert. Ubeti wake ambao naukumbuka kuhusu "Mtanikuta Morogoro" umenifanya nimunganishe ndugu Mroki Mroki kama mtu anayeweza kutufundisha mengi kupitia mashairi. Kaka Mroki, Morogoro nikisima cha mambo mengi, Mbaraka Mwishekhe, alitokea hupo na hakika ukimsikiliza si tu katika tungo zake, bale pia katika beti zake zakimuziki utakubaliana nami kuwa alikuwa na busara zakutufundisha.
Sisi sote tuna busara lakini nivizuri kukubali kuwa kunawale wanaotuzidi kidogo. Je unakumbuka pia "diwani ya Mloka?"
Kaka Mroki Asante sana kwa jibu lako si tu kuwa limenifurahisha, lakini pia limenifunza nakunikumbusha mambo msingi katika kuuishi umoja na Amani kama taifa. Nimelichukua nakuliifadhi pamoja na lile la bwana Mwamgongo kwa ajili ya mradi wa kitabu ambacho kipo njiani, kitakacho beba jina la "Kwetu hatuna makabila tunakiswahili".
Hili ni kama jibu la maswali tata na nyeti. Usiogope msomaji. Tafadhali pia msomaji jina hili usilitumie. Usiogope kuwa na hisia juu ya nini kitakuwemo ndani yakitabu hiki. Ni katika kutia gundi zaidi katika Umoja wetu. Hata wale walio na wanajaribu kututenganisha wapite mbali na jicho lao la "husda"
Hakika nasema asanteni saaaana kwa mchango wenu huu. Mnanivutia kuwasoma pia watanzania woote wale wanaoandika na hata wale wasiopata bahati yakuandika katika blogu hii na nyingine. Nasema haya nikiifahamu fika hali ya nchi yangu katika idara ya mawasiliano ya "intaneti"mawasiliano. Nasemea hasa wale wanaoishi vijijini. SIMU za mkononi tupo juu.
Zaidi nitafurahi kama kunawengine wataendeleza huu "mdahalo" wakutoa au kutuelimisha kupitia mitanadao hii ili tuendelee kujuzana hili a lile hasa sisi tulio ughaibuni.Nimeona ndugu Mroka umetugusa ukiwataja wale wa ma"dipatimenti" Hakika hapo uko sawa.
Kaka vina na mizani ya shairi lako ni babu kubwa. Ujumbe ndiyo zaidi. Laweza tumika hata mashuleni. Nikiendelea kufuatilia habari za nchi na ndugu zangu watanzania kupitia blogu hii ambayo imeshakuwa kama dozi ya dawa vile, kumbuka enzi zile za Chloroquine dawa ya maleria.
Kwani naisoma walao mara tatu kwa siku, yaani asubuhi nikiamka, mchana baada ya chakula, na jioni, usiku kabla sijalala. Watanzania mwendo ni huu huu. Maendeleo yetu ni nguvu na juhudi zetu soote kama watanzania, na waafrika na hasa zaidi binadamu. Mambo mengine nikama "accident" tu ila asili yetu ni Ubinadamu au vipi.U-jamaa.
Through Blogs and other sources, let us promote the common good of, and for our country, Tanzania and continue living togehter for this common good as Mwalimu Nyerere wished us to do always. Mpoo! Na libeneke liendeleee.
Mdau
Frederick Meela.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...