Mkurugenzi wa Kampuni ya SONGAS Limited,Bw. Christopher Ford (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, Mh. Edward Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam,,iliyofanyika jana usiku kwenye hoteli ya Hyatt Regency.Kushoto ni Meneja Rasilimali wa Songas,Bi Agatha Keenja.
Mgeni rasmi wa Harambee hiyo,Mh. Edward Lowassa akimpa mkono wa asante mwakilishi wa kampuni ya Home Shopping Centre,Bi Madiha Al Harthy (kushoto) baada ya kuchangia sh. milioni 22.
Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh. Bonah Kaluwa akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Mgeni rasmi wa harambee hiyo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa (wa pili kulia), akiwa amesimama na viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Manispaa ya Ilala wakati wimbo wa taifa ukipigwa kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendelea kuwa mstari wa mbele katika harakati zake za kuchangisha fedha baada ya kuchangisha zaidi ya Sh. Milioni 421.8 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katika harambee hiyo iliyofanyika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski Dar es Salaam, Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli alichangia Sh.milioni 10.
Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa ni Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22, African Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja alichangia milioni Sh.10.
Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh. milioni 12.
Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu.
Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa jitihada zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani wengine kuiga mfano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, alisema shule saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na changamotonyingi zikiwemo za upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja huku wakiwa wamekaa chini.
.“Shule nyingi katika kata yangu zinakabiliwa na changamoto nyingi, kwa mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane wakati wanafunzi waliopo ni 2,200, Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa.
Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15 kilichangwa na wadau mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3 zilitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group ambao walitoa shilingi milioni moja na wanafunzi kadhaa wa shule za msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga alisema katika jimbo hilo shule nyingi zinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo alitoa mwito kwa wananchi na madiwani wa eneo hilo kuunga mkono jitihada za kuchangia elimu ili kuwaondolea wanafunzi adha wanayopata ya kukosa mazingira bora ya kuopata elimu.
Well done diwani wa Dar es Salaam! Ndio wa Dar es Salaam, kwani wengine wako wapi?
ReplyDeleteMIMI NI MMWANANCHI WA KIPAWA B (KIWALANI), NAMSHANGAA SANA MBUNGE WETU MAKONGORO MAHANGA KWANI TANGU ACHAGULIWE HATUJAWAHI KUMWONA HATA SIKU MOAJA KUJA KUTATUA MATATIZO YETU HASA SISI WA KIWALANI. BARABARA NI MBAYA SANA, WAKATI WA MVUA NI MATATIZO MATUPU.HAKUNA MIFEREJI. TAKA ZIMEZAGAA HOVYO KILA MAHALI. AKIITWA HAJI, NADHANI WAMESHATOSHEKA YEYE NA DIWANI WETU. PESA ZINAZOTOLEWA KWA AJILI YA MAENDELEO HATUJAWAHI KUONA MAENDELEO YEYOTE. ZAIDI YA WAO KUTANUA. NA HIVI KASHINDA KESI KWA WIZI, MAANA HATUKUMCHAGUA NDIO MAANA NASEMA HIVYO, NDO BASI YEYE YUKO KIVULINI, WANANCHI WAKE WANATESEKA.TUMEMCHOKA SANA WALA HATUNA HAMU NAYE KABISA.
ReplyDeleteSafi sana, harambee kama hizi ndo zinahitajika siyo michango ya harusi..big up madiwani wa Ilala.
ReplyDeletemlishindwa nini kumpitisha mpendazoe.....?????? sasa diwani huyu ndio agombee ubunge wa ubungo huyu mahanga kashakua mhanga
ReplyDelete