Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua bidhaa ya mmoja wa Wajasiriamali Tatu Suleiman wa Chukwani Zaidat Oil ambaye ni Mjasiri wa mwanzo kutoka Zanzibar aliyefikia kiwango cha juu cha ushindi katika Mpango wa Faidika Kibiashara Nchini Tanzania.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Hundi ya Shilingi Milioni 697,000,000/- kwa Wajasiri Amali watano kwa   niaba ya wenzao 213 wa Mikoa Mitano ya Zanzibar walioshindia kwenye Mafunzo ya Faidika Kibiashara Tanzania. Sherehe hizo zilifanyika katika Viwanja vya Victoria Garden Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Taasisi zilizofadhili na Kuendesha Mafunzo ya Faidika Kibiasha Nchini Tanzania  kwenye Sherehe za utoaji zawadi kwa washindi wa mafunzo hayo hapo victoria Garden Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

Taasisi zinazowawezesha Wananchi Kiuchumi nchini zimehimizwa kuwatumia vyema Wajasiriamali wanaopata Mafunzo kwenye Mpango wa Faidika Kibiashara kwa lengo la kujenga mazingira bora zaidi ya ajira ndani ya Sekta Binafsi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  ametoa Himizo hilo katika sherehe ya utoaji zawadi kwa Wajasiriamali walioshiriki Mafunzo ya Mpango wa Faidika Kibiashara zilizofanyika kwenye Viwanja vya Victoria Garden Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif alisema mafanikio yaliyokusudiwa ndani ya Mpango huo yataweza kupatikana pindipo Taasisi hizo zitatumia ujuzi wa Wajasiri Amali hao na hatimae kukuza Uchumi wa Taifa.
Aliziomba Taasisi zilizopo kwenye Sekta Binafsi kufikiria kuwa na Umoja imara kupitia Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar utakaoiwezesha Sekta hiyo kufikia malengo ya Taifa ya kukuza Uchumi Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba Serikali itajitahidi kusaidia Sekta Binafsi  ili ikue na kuchangia kwa kiasi kikubwa Maendeleo ya Nchi.
Alieleza kuwa Mpango mzima wa Faidika Kibiashara umedhihirisha namna ya mafanikio baina ya  Serikali na Sekta Binafsi yanavyowezekana pindipo itakuwepo mikakati imara.
Mpango huo ni chem Chem ya Elimu ya Biashara ambayo Wafanyabiashara walengwa ni wale wadogo wadogo ambapo pia aliwaomba kutumia vyema fursa hiyo.
“ Biashara bila ya Elimu, jawabu lake ni kufilisika. Nani kati yenu anataka kufilisika? Kama jawabu hapana maana yake tujitokeze kwa wingi kila fursa za mafunzo zinapotokea kwani Biashara ukiijumlisha na Mafunzo jawabu yake ni Mafanikio”. Alisisitiza Balozi Seif.
Balozi Seif alilikubali ombi la Wajasiri Amali hao la Nchi kuwa na Wafanyabiashara wengi ambao wataliwezesha Taifa kuwa na Rasilmali na Hakiba ya kutosha ya Pato la Nchi.
Alisena uimarikaji wa Sekta hiyo sambamba na Mafunzo ya Uwezeshaji kwa Umma utajenga hatma njema hasa kwa wafanyakazi wanaomaliza muda wao wa Utumishi Serikalini kuweza kujiendeleza Kibiashara.
Alisema Wastaafu wengi hivi sasa wamekuwa wakibabaika kwa kukosa mtaji wa kuendeleza Maisha yao ya Uzeeni kutokana na ukosefu wa mafunzo ya Ujasiri amali.
Katika Risala yao Wajasiriamali hao wa Faidika Kibiashara wamezishukuru Taasisi za Benki ya Watu wa Zanzibar, Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka pamoja na 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...