KOCHA wa Riadha wa Timu ya Tanzania inayotarajiwa kushiriki mashindano ya Olimpiki London, Julai 27 hadi Agosti 12 mwaka huu, Zakaria Gwandu, ameelezea kusikitishwa na kushangazwa kwa mchezaji Faustine Mussa kutojiunga na wenzake kambini, Mkuza Kibaha.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi leo, Gwandu, alisema, wakati timu ikitarajiwa kuondoka nchini Julai 8 mwaka huu, Mussa ambaye ni mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ndiye pekee hawajatia mguu kambini hapo, jambo linalomweka katika wakati mgumu wa kutekeleza programu zake.

“Kwa kweli sielewi kinachoendelea kuhusiana na mchezaji huyu Faustine Mussa, sijui tatizo ni kwa mchezaji au mwajiriwa wake, kwani barua ya kuombewa ruhusa Chama cha Riadha (RT), kilikwisha ituma kwa mwajiri wake muda mrefu, lakini mchezaji hadi sasa hajatokea kambini,” alilalamika Kocha huyo.

Timu ya riadha itakayoshiriki michezo ya Olimpiki London nchini Uingereza, inaundwa na wachezaji wanne, Zakia Mrisho, Samson Ramadhani, Msenduki Mohamed na Faustine Mussa, ambaye bado hajaripoti kambini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2012

    Huyo kocha wa taifa katika enzi hizi mawasiliano mazuri hawazi hata kujua ni kwa nini Nusa hajafika kambini. Wakati ambao anautumia kumlalamikia musa kwa mwandishi wa habari anaweza kumpigia simu Musa mwenyewe au Mwajiri wake kujua kwa nini hajafika kambini. Ikiwa hapa nyumbani hawezi kufuatilia na kuwa na contacts na wachezaji wake wote, je kule aendako anaweza kufuatilia mambo ya huko? au itakuwa malalamishi kamaya Musa tu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2012

    Wenzetu walianza maandalizi miaka 4 iliyopita kambi ndio inaendwa saa hizi? Wanaenda kutembea tu hao

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2012

    bongo hatupo serious na michezo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2012

    Wanariadha wanne(4)? Yaani hao ni wanne bora au ni Bajeti?Jamani wacheni maskhala. Nashangaa sana na waratibu wa michezo. Utaona kuna idadi kubwa ya msafara kwenda kufanya shopping. Hii aibu jamani na pia karne hii Kocha hajui ni jinsi gani ya kuwasiliana na muhusika! Jamani tubadilike.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...