Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati ya utambulisho kutika kwa Balozi wa Eritrea Mhe. Beyene Russom Habtai leo Ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete leo amepokea hati za mabalozi watano wanaoziwakilisha nchi zao hapa pamoja na kupokea wajumbe wawili maalum waliotumwa na marais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Mabalozi waliowasilisha hati za utambulisho ikulu ni pamoja na Mhe.Domingo Lucenario wa Phillippines, Mhe.Volodymyr Butiaha wa Ukraine,Mhe.Beyene Russom Habtai wa Eritrea, Mhe.Kingsley Saka Karimu wa Ghana pamoja na Mhe.Gil Haskel wa Israel.
Wajumbe walioleta salamu maalum kutoka kwa marais wao ni pamoja namhe.Raymond Tschibanda ambaye ni Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa DRC na Mhe.Nhial Deng Nhial ambaye ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Sudan ya Kusini. (picha zote na Freddy Maro)
Balozi wa Ghana Mhe.Kingsley Saka Karimu akiwasilisha hati za utambulisho.
Balozi wa Israel mhe. Gil Haskel akiwasilisha hati za utambulisho.
Balozi wa Philippines Mhe. Domingo Lucenario akiwasilisha hati za utambulisho.
Balozi wa Ukraine Volodymyr Butiaha akiwasilisha hati za Utambulisho.
Mhe.Nhial Deng Nhial akiwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais Salva Kiir.
Mhe.Raymond Tschibanda akiwasilisha ujumbe kutoka kwa Rais Joseph kabila.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...