matundu saba ya Risasi kwenye sehemu ya kiuno na tumbo ya Ng'ombe Dume mwenye uzito wa kilo 700 ambaye amepigwa Risasi na Maskari wa wanyama Pori wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, dhamani ya Dume Huyu inafikia shilingi Tsh: 900,000/=
 michirizi ya Damu juu ya paja la Ng'ombe baada ya kupigwa Risasi na maaskari wa hifadhi ya Mikumi jana.
Ng'ombe Jike akionekana na matundu 4 ya Risasi baada ya kupigwa jana na maaskari wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Ng'ombe huyu alirudi nyumbani usiku kwa mwendo wa kuchechemea na baadae akawa amekufa.Kwakweli unyama huu umekuwa ni huzuni sana kwa wafugaji wanaokaa maeneo ya jirani na hifadhi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2012

    Watafutwe wafungwe kabisa hata Simba porini angemuacha Ng'Ombe leo Maaskari wanauwa wanyama bila sababu hii kesi awshikwe wafungwe au wasimamishwe kazi. MZ

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2012

    Call it unyama or anything, cha msingi hapa ni hawa wafugaji.
    Inabidi waiangalie mifugo yao kikamilifu isiingie mbugani kwenda kuchanganyika na wanyama pori kwani kwa kufanya hivyo kuna uwezekano wa kupeleka magonjwa ambukizi kwa wanyama wa porini kitu ambacho kitahatarisha maisha ya wale wanyama wa porini pia.

    Wafugaji wanaokaa karibu na maeneo ya hifadhi, hakikisheni mifugo yenu haiendi mbali na makazi yenu. Inaelekea hawa wafugaji hawasikii halafu wanakuja hapa kutaka sympathy, wasitake kuleta siasa hapa, sheria ipo ambayo inasema marufuku kuingiza mifugo ndani ya hifadhi kwa sababu zinazoeleweka.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2012

    Elimu ya Ubinaadamu ni muhimu itolewe kwa Askari wote badala ya kuegemea kufundishwa Sheria peke yake.

    Matokeo ya muegemeo huo ni kitendo cha hawa Askari wa Wanyama Pori!

    Hivi ng'ombe wa kawaida na Wanyama Pori kama tuseme Nyati wana tofauti gani?

    Wote si ndio viumbe wenyewe?

    Hivi unapolinda Mpakani tuseme kati ya Kenya na Tanzania halafu wewe ukawa Mlinzi wa mpaka wa Tanzania ina maana mtu wa Kenya akiingia Tanzania itakuwa ni jukumu lako kumchapa risasi badala ya kumuuliza kwanza ni vipi ameingia upande wa Tanzania?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2012

    Ndugu Hili jambo linasikitisha sana. Si haki hata kidogo kumpiga Ng'ombe risasi hata kama ameonekanika kwenye hifadhi. Ni ukatili usiokifani, Ni ukatili usiokubalika kwa jamii hata kidogo. Ngombe ukimfuata hakupigi, hakung'ati, ukimfukuza anaondoka..Ni kipi kinamfanya mtu ampige ngombe risasi? tena mlo wetu? Hii ni hatari sana.. kuna uwezekano mkubwa sana kukaribisha njaa ya hatari kwa kutokuheshimu viumbe wanaotupa chakula. Haistahili na haitakubalika hata kidogo kumwadhibu ngombe kwa makosa ya mwanadamu. Imeniuma sana.
    Emmanuel

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2012

    Wote mku sahihi,Mawazo yenu nyote ni mazuri. Mimi nadhani hao maaskari wwngewakamata ng'ombe wakawafungia kwenye yard maalumu (naamini yard hizo zipo).Kisha mkawachukulia hatua za kisheria wamiliki wa Ng'ombe hao.Tena wangetoa adhabu kali kwelikweli kwa wamiliki wa ng'ombe hao. Jamani ng'ombe hawana akili yakujua hii ni hifadhi. Wao wanachotaka ni majani mazuri yaliyo stawi wapate msosi. SO BAD....!!!!

    ReplyDelete
  6. Hakuna lolote acha wapigwe risasi ndiyo hao jamaa watapata somo hao wafugaji ni wabishi sana na mara nyingi wanafanya makusudi hua , Hata mashamba ya wanachungia tu , wakifanyiwa kama hivyo inakua fundisho, kwangu naona wanasitahili, ngawa hata mimi natokea familia ya wafugaji , wafugaji wabishi sana.

    Mkurya mimi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2012

    so sad..binadamu wengine hawana utu kabisa.

    Mtu anamfanyia kiumbe asiye na uelewa mabaya kama haya ni hatari hata kwa binadamu mwenzake.

    Wafungwe!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2012

    Tuache ''huruma'' za upande mmoja!
    Kwani simba akiingia kijijini anafanywa nini? anashikwa sharubu anabembelezwa arudi hifadhini?
    Tembo je?
    Nyati je? Au kwa sababu hawa ni ''wanyama wa porini''?

    Kama hawa wanapigwa risasi basi na hao ng'ombe wacha wapigwe risasi maana wote ni viumbe hai.

    Tembo, nyati wanakuwa shot nyama zao zinagaiwa kijiji husika. Simba, chui wanakuwa shot ngozi zao zinapelekwa sehemu husika.

    Basi na hao ng'ombe wachinjeni mgawe nyama na mwenye ng'ombe alimwe faini pia. Tuache kupelekwa na hisia zaidi, la sivyo kanuni zimewekwa hatutakuwa tunazizingatia.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2012

    Hawa askari wa wanyama pori wamekosa hata chembe ya busara. Hivi wao katika maisha hawajawahi kuingia eneo lililozuiliwa? Hawa ng'ombe hata kama kungekuwa na tangazo la kuwazuia kuingia humo bado wangeingia tu kwa sababu wao hawawezi kutofautisha sehemu ya hifadhi na malisho mengine. Wenye kosa hapa ni wafugaji/wachungaji. Hivi kweli wale ng'ombe wangekuwa ni wao (askari) wangewapiga risasi? Hapo ndiyo tungeona ule usemi wa mkuki kwa.......kwa binadamu..... Hatua waliyochukua ni ya kukomaza chuki na si kumaliza tatizo. Usimwadhibu mnyama kwa kosa la binadamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...