Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama  ishara ya ufunguzi wa madrasat Nurullah Kitope Zanzibar,iliyopo Wilaya ya Kaskazini B Unguja,Mkoa wa  Kaskazini,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,jengo
hilo limejengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mohamed Raza 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akifuatana  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,pamoja na viongozi wengine alipowasili katika Jengo la Madrasat Nurullah Kitope,kwa ajili ya kulifungua rasmi,lililojengwa kwa
ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi  wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza. 
 Baadhi ya wanafunzi wa Kike wa Madrasat Nurullah ya Kitope wakiwa katika sherehe ya ufunguzi wa madrasa yao iliyojengwa kwa kiwangi kizuri ambacho kitwafanya kuwa na arizaidi ya kusoma kwa bidii,iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,iliyojengwa kwa ufadhili wa Abdalla Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi  wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akitembelea katika vyumba mbali mbali vya Madrasat Nurullah Iliyopo  Kitope Wilaya ya Kaskazini B,Unguja
 Baadhi ya wanafunzi wa Kiume wa Madrasat Nurullah ya Kitope wakiwa mbele ya uwanja wa jengo la Madrasa yao
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wapili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pembe Juma Pembe,(kushoto) wakati sherehe za ufunguzi wa Madrasat Nurullah ya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wapili kushoto) akipokea risala ya wananchi na wanamadrasat   Nurullah ya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,kutoka kwa Mwalimu Juma Mohamed,baada ya kuifungua Madrasa hiyo
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza,akitoa shukurani zake na kwa niaba ya wafadhili waliojenga Madrasat Nurullah. Picha zote na mdau Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2012

    Jamani wapendwa....naomba kuuliza hivi Zanzibar kuna askari polisi wa kike? Kama wapo huwa wanavaaje? Kwa mimi sijawahi kuona askari wa kike zanzibar amepigwa picha kwemye hafla kama hizi! kama zipo ziwekeni tuzione!

    ReplyDelete
  2. Askari wa kike Zanzibar wapo, tena wengi tu! Na isitoshe huvaa kama wavaavyo askari wengine wa kike nchini (Uniform), Ila tu inategemea na kitengo alichopo askari huyo/haoi, mana baadhi ya vitengo kwa mujibu wa kazi zao, hulazimika kuvaa kiraia. Hata hivyo mara nyingi hao wa kike unakuta wapo kwenye vituo vyao vya kazi na baadhi yao unaweza kuwakutia barabarani wakiwajibika katika doria zao za kila siku na baadhi yao ni wana usalama barabarani "Traffic police". Kadhalika hata kwenye hafla na misafara mbali mbali au shughuli zozote zenye mikusanyiko inayowajumuisha viongozi mbali mbali au wananchii kwa jumla, basi pia na wao huwemo kazini wakiwajibika katika suala zima la kulinda usalama wa raia, nchi na mali zao.

    Suala la wao kuwaona wamepigwa picha katika hafla mbali mbali au kama hizi, huwa lipo na wanapigwa picha nyingi tu! Ila inategemea na hiyo hafla yenyewe na mazingira yake kwa jumla na kama kuna ulazima huo wa kutolewa kwenye vyombo vya khabari kama vile Magazeti, Television, Mitandaoni n.k. Basi hakuna kizuwizi/pingamizi yeyote ya picha hzio kutolewa na zikawa viewed by the pulic.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2012

    Assalama Aleykum Masheikh Visiwani?

    Al kul hali Muungano unakwenda Ali jojo Mashikh mpo busy na ubwabwa wa Maulidi na Dufu,,,Kulikoni?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2012

    Anon. wa pili haopo juu, naomba kukusahihisha hilo neno ulilolitumia hapo, siyo Ali jojo bali ni "ARIJOJO". Ila kwa muonekano tu, huo hawendi arijojo hata siku moja! Uzi umekazwa khasa, tena ule wa utare madhubuti kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...