Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa madrasat Nurullah Kitope Zanzibar,iliyopo Wilaya ya Kaskazini B Unguja,Mkoa wa Kaskazini,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,jengo
hilo limejengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mohamed Raza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akifuatana Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,pamoja na viongozi wengine alipowasili katika Jengo la Madrasat Nurullah Kitope,kwa ajili ya kulifungua rasmi,lililojengwa kwa
ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.
Baadhi ya wanafunzi wa Kike wa Madrasat Nurullah ya Kitope wakiwa katika sherehe ya ufunguzi wa madrasa yao iliyojengwa kwa kiwangi kizuri ambacho kitwafanya kuwa na arizaidi ya kusoma kwa bidii,iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,iliyojengwa kwa ufadhili wa Abdalla Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akitembelea katika vyumba mbali mbali vya Madrasat Nurullah Iliyopo Kitope Wilaya ya Kaskazini B,Unguja
Baadhi ya wanafunzi wa Kiume wa Madrasat Nurullah ya Kitope wakiwa mbele ya uwanja wa jengo la Madrasa yao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wapili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pembe Juma Pembe,(kushoto) wakati sherehe za ufunguzi wa Madrasat Nurullah ya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wapili kushoto) akipokea risala ya wananchi na wanamadrasat Nurullah ya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,kutoka kwa Mwalimu Juma Mohamed,baada ya kuifungua Madrasa hiyo
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza,akitoa shukurani zake na kwa niaba ya wafadhili waliojenga Madrasat Nurullah. Picha zote na mdau Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar
Jamani wapendwa....naomba kuuliza hivi Zanzibar kuna askari polisi wa kike? Kama wapo huwa wanavaaje? Kwa mimi sijawahi kuona askari wa kike zanzibar amepigwa picha kwemye hafla kama hizi! kama zipo ziwekeni tuzione!
ReplyDeleteAskari wa kike Zanzibar wapo, tena wengi tu! Na isitoshe huvaa kama wavaavyo askari wengine wa kike nchini (Uniform), Ila tu inategemea na kitengo alichopo askari huyo/haoi, mana baadhi ya vitengo kwa mujibu wa kazi zao, hulazimika kuvaa kiraia. Hata hivyo mara nyingi hao wa kike unakuta wapo kwenye vituo vyao vya kazi na baadhi yao unaweza kuwakutia barabarani wakiwajibika katika doria zao za kila siku na baadhi yao ni wana usalama barabarani "Traffic police". Kadhalika hata kwenye hafla na misafara mbali mbali au shughuli zozote zenye mikusanyiko inayowajumuisha viongozi mbali mbali au wananchii kwa jumla, basi pia na wao huwemo kazini wakiwajibika katika suala zima la kulinda usalama wa raia, nchi na mali zao.
ReplyDeleteSuala la wao kuwaona wamepigwa picha katika hafla mbali mbali au kama hizi, huwa lipo na wanapigwa picha nyingi tu! Ila inategemea na hiyo hafla yenyewe na mazingira yake kwa jumla na kama kuna ulazima huo wa kutolewa kwenye vyombo vya khabari kama vile Magazeti, Television, Mitandaoni n.k. Basi hakuna kizuwizi/pingamizi yeyote ya picha hzio kutolewa na zikawa viewed by the pulic.
Assalama Aleykum Masheikh Visiwani?
ReplyDeleteAl kul hali Muungano unakwenda Ali jojo Mashikh mpo busy na ubwabwa wa Maulidi na Dufu,,,Kulikoni?
Anon. wa pili haopo juu, naomba kukusahihisha hilo neno ulilolitumia hapo, siyo Ali jojo bali ni "ARIJOJO". Ila kwa muonekano tu, huo hawendi arijojo hata siku moja! Uzi umekazwa khasa, tena ule wa utare madhubuti kabisa.
ReplyDelete