Lile sakata la mkopo kati ya bodi ya mikopo na wanafunzi wa mwaka wa kwanza walioko mjini Constantine nchini Algeria linaendelea kuchukua sura mpya huku mambo yakiwa kitendawili ni lini fedha hizo zitatumwa kwa wanafunzi hao.
Habari kutoka chanzo chetu kilichopo huko nchini Algeria zinasema kuwa wanafunzi hao waliamua kuunda kamati yao ya kushughulikia jambo hili baada ya kuona wanazungushwa na kupigwa kalenda na umoja wa wanafunzi uliopo huko uitwao ATSA.Kamati hiyo ilipewa majukumu ya kupiga simu kwa mkurugenzi mtendaji wa bodi ambaye hakupokea simu hata moja kati ya zile zaidi ya 5 zilizopigwa.
Wakati taarifa zilizopo sasa ni kwamba bodi ya mikopo ilipokea akaunti hizo mnamo tarehe 25/5/2012 lakini kabla ya hapo vijana hao walishatumiwa e-mail na uongozi huo wakitaarifiwa juu ya akaunti zao kupokelewa bodi ya mkopo.
E-mail hiyo ambayo pia ilitumwa kwa wanafunzi wote walioko nchini huko. Chanzo chetu kilitufowadia e-mail hiyo na tukakopi baadhi ya maandishi ya e-mail hiyo ambayo inasadikiwa kutumwa na waziri mkuu wa chama hiko ambaye tusingependa kumtaja jina.
Nimeona malalamiko ya wanafunzi hawa wa Algeria. Nimeongea na Bodi ya Mikopo. Wamenieleza kuwa kabla ya kwenda huko Algeria walipewa fedha ya muhula wa kwanza. Kwa mujibu wa uongozi wa Bodi, tatizo lilikuwa masharti wa ufunguaji wa akaunti huko Algeria. Bodi imekiri kupokea akaunti zao.
ReplyDeleteBodi imenitaarifu kuwa leo kuwa kiasi cha TSh 247 millioni zimetumwa kwa ajili ya wanafunzi hao 56. Watarajie kupata fedha zao hivi karibuni. Ahsante.
Dr Faustine Ndugulile (MB)
Mbunge-Kigamboni
Makamu Mwenyekiti-Kamati ya Bunge-Huduma za Jamii
naona sasa kuna vijana wanakosa kazi za kufanya,,,,sasa bodi ya mkopo na DINI zina mahusiano gani?MTU MZIMA NI FIKRA NA KUSOMA NI KUELIMIKA,,,HEBU VIJANA PIGENI SHULE MNA SAFARI NDEFU YA KWENDA,,naamini bodi itawasikiliza Lakini PIA TUHESHIMU VIONGOZI WETU,,nawakilisha hoja
ReplyDeleteKama walipewa taarifa tr 25/5 kuwa watapewa hizo hela mbona ni juzi tu? Kama leo tr 7/6 hata wiki 2 bado nadhani subira ni kitu muhimu sana hazijachelewa kiasi cha kumsumbua Michuzi na kutoa lawama ambazo hazina points,
ReplyDelete