Lile sakata la mkopo kati ya bodi ya mikopo na wanafunzi wa mwaka wa kwanza walioko mjini Constantine nchini Algeria linaendelea kuchukua sura mpya huku mambo yakiwa kitendawili ni lini fedha hizo zitatumwa kwa wanafunzi hao.

Habari kutoka chanzo chetu kilichopo huko nchini Algeria zinasema kuwa wanafunzi hao waliamua kuunda kamati yao ya kushughulikia jambo hili baada ya kuona wanazungushwa na kupigwa kalenda na umoja wa wanafunzi uliopo huko uitwao ATSA.Kamati hiyo ilipewa majukumu ya kupiga simu kwa mkurugenzi mtendaji wa bodi ambaye hakupokea simu hata moja kati ya zile zaidi ya 5 zilizopigwa.

Wakati taarifa zilizopo sasa ni kwamba bodi ya mikopo ilipokea akaunti hizo mnamo tarehe 25/5/2012 lakini kabla ya hapo vijana hao walishatumiwa e-mail na uongozi huo wakitaarifiwa juu ya akaunti zao kupokelewa bodi ya mkopo.

E-mail hiyo ambayo pia ilitumwa kwa wanafunzi wote walioko nchini huko. Chanzo chetu kilitufowadia e-mail hiyo na tukakopi baadhi ya maandishi ya e-mail hiyo ambayo inasadikiwa kutumwa na waziri mkuu wa chama hiko ambaye tusingependa kumtaja jina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nimeona malalamiko ya wanafunzi hawa wa Algeria. Nimeongea na Bodi ya Mikopo. Wamenieleza kuwa kabla ya kwenda huko Algeria walipewa fedha ya muhula wa kwanza. Kwa mujibu wa uongozi wa Bodi, tatizo lilikuwa masharti wa ufunguaji wa akaunti huko Algeria. Bodi imekiri kupokea akaunti zao.

    Bodi imenitaarifu kuwa leo kuwa kiasi cha TSh 247 millioni zimetumwa kwa ajili ya wanafunzi hao 56. Watarajie kupata fedha zao hivi karibuni. Ahsante.

    Dr Faustine Ndugulile (MB)
    Mbunge-Kigamboni
    Makamu Mwenyekiti-Kamati ya Bunge-Huduma za Jamii

    ReplyDelete
  2. naona sasa kuna vijana wanakosa kazi za kufanya,,,,sasa bodi ya mkopo na DINI zina mahusiano gani?MTU MZIMA NI FIKRA NA KUSOMA NI KUELIMIKA,,,HEBU VIJANA PIGENI SHULE MNA SAFARI NDEFU YA KWENDA,,naamini bodi itawasikiliza Lakini PIA TUHESHIMU VIONGOZI WETU,,nawakilisha hoja

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2012

    Kama walipewa taarifa tr 25/5 kuwa watapewa hizo hela mbona ni juzi tu? Kama leo tr 7/6 hata wiki 2 bado nadhani subira ni kitu muhimu sana hazijachelewa kiasi cha kumsumbua Michuzi na kutoa lawama ambazo hazina points,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...