Balozi Salome Sijaona, Mwansheria Mkuu Michael Mischin, Dr Tungaraza, na Dr Nzuki
 Dr Tungaraza na Profesa Eric Tan, Mwekezaji
 Meya Lisa Scafidi akimpa katiba Bwana Mahir Meghji
 Ugeni mzima na wenyeji wao
 Wadau katika hafla hiyo

huko Perth Australia kulikuwa na shughuli kubwa ya kuutangaza utalii wa Tanzania. Balozi wa Tanzania huko Japani anayesimamia Australia, Balozi Salome Sijaona alijiunga na kundi la viongozi wa mashirika kadhaa ya Utalli hapa Tanzania katika tafrija fupi iliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali wa Australia Magharibi.
\
Mwenyeji katika shughuli hii alikuwa Dr Casta Tungaraza ambaye ni Balozi wa Utalii wa Tanzania huko Australia. 
Viongozi hao  kutoka Tanzania walijiunga na viongozi wa Australia Magharibu wakiwemo  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bwana Michael Mischin pamoja na Meya wa Jiji la Perth Lisa Scafidi.
Wengineo walikuwa Wabunge Ian Britza, Janine Freeman na Ken Wyatt.

Katika shughuli hiyo mbali ya kuzindua Ofisi na kazi za kutangaza utalii Australia kulizinduliwa pia ofisi ya Baraza la Biashara la Australia na Tanzania ( Australia- Tanzania Business Council).  Kaimu Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw Meghji alikadhibiwa rasmi Katiba ya Baraza hilo kama ushuhuda wa kukubalika kwa Baraza hilo hapa Australia.

Wageni waliotoka Tanzania kuutangaza Utalii ni pamoja ba Dr Aloyce Nzuki Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii, Bi Halima Mamuya na Shaddy Kyambile kutoka Hifadhi ya Ngorongoro na Dr Ezekiel Dembe wa TANAPA.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...