Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 12 kwa ajili ya Manispaa ya Ilala, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mushi (kushoto) na Steve Kilindo wa TBL wakifagia ikiwa ni ishara ya kuzindua rfasmi maadhimisho hayo karibu na Soko la Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiungana na watumishi wa Manispaa ya Ilala kufanya usafi wa mazingira katika makutano Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Muheza, Karikaoo, Dar es Salaam jana. TBL ilitoa msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. mil. 12 kwa Manispaa ya Ilala wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira, Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2012

    jamani waende soko la Ilala linanuka uongozi umelala wanachojua wao ni kula pesa tu hasahasa magari yanayoingia usiku sokoni hakuna usimamizi wowote ule yale maeneo ya pakini sokoni ndani ni uchafu mtupu. wachuuzi wanalipizwa pesa lakini hakuna kitu chochote kinachofanyika zinaingia mifukoni mwa wachache kama mnabisha fanyeni uchunguzi muwaulize wachuuzi. hakuna hata taa za kutosha kwa ajili ya usalama. Jamani aibu tupu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2012

    Hongera TBL kuwa mstari wa mbele kwenye kusafisha na kulinda mazingira.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...