Mkaguzi wa ndege,Makhiid Towillo (kushoto) akitoa mada katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya usafiri salama wa anga jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Fadhili Manongi (aliesimama) akifungua mkutano wa siku moja wa maboresho wa wadau wa sekta ya usalama wa Anga jijini Dar es Salaam leo.(kushoto) ni Mkurugenzi wa Sheria za Usalama wa mambo ya Anga kutoka Mamalaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).
Mkaguzi Mkuu anaeshughulikia masuala ya ajali za usafiri wa ndege kutoka Wizara ya Uchukuzi John Nyamwihura akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu masuala mbalimbali ya usalama na ajali za ndege nchini katika mkutano huo wa siku moja wa wadau wa usafiri salama wa sekta ya anga.
Baadhi ya wadau wa mkutano wa maboresho wa mambo ya usalama wa sekta ya usafiri wa Anga nchini wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano wa siku moja uliofanyika leo  jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) uliofunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Fadhili Manongi (hayupo pichani) Mkutano huo umezungumzia masuala mbalimbali jinsi ya kuboresha usalama wa usafiri wa anga pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wa sekta hiyo.
Sehemu ya muonekano wa ukumbi wa mkutano wa Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ulikofanyika mkutano wa maboresho wa wadau wa mambo ya usalama wa sekta ya usafiri wa anga leo jijini Dar es Salaam .(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...