Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. Zelothe Stephen akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) vyeti feki vya watuhumiwa wa kundi la Matapeli la LAMBA LAMBA vyeti hivyo ni vya (UMAWATI )– vya mtuhumiwa DK. Shabani R Kisoma ambacho kirefu chake ni UMOJA WA WAGANGA WATAFITI WA MAGONJWA SUGU UKIMWI NA TIBA ASILIA TANZANIA, na (CHAUMUTA) – Cha mtuhumiwa anayejiita DK. Hussein Shomari Mabogo, ambaye amekamatwa , kirefu chake ni CHAMA CHA UTAFITI WA MAGONJWA SUGU NA UKIMWI KWA TIBA ASILIA.
Baadhi ya watuhumiwa wa utapeli wa kufanya waganga wa kienyeji wa Kundi la Lamba Lamba wakiwa wameshika dhana za kazi wakiwaonyesha waandishi wa habari pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen (hawapo pichani). Kutoka kushoto waliovaa kawaida ni Mkude S/O Mwenda 32 yrs, Mkulima, na Joseph S/O John miaka 27, Mkulima, wote wakazi wa Mkoka – Kongwa na SALEHE S/O OMARI, mwenye umri wa miaka26, mkulima wa Songe Kilindi Mkoani Tanga aliyevaa lubega nyekundu kwa nyeusi na ndani ana fulana mistari.Picha na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2012

    Kwani hawakusema wameoteshwa?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2012

    polisi mmeanza tena yale mambo yenu ya kuwahukumu watu kabla ya mahakama. iweje mtuhumiwa alazimishwe kushika 'kithibitisho' mradi tu mpate picha ya kujikosha kwamba mnafanya kazi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2012

    hamuwakamati wanao fisidi mafisaji kwa kweli kweli wanaofisidi uchumi wa nchi na mnawajua mnakula nao sahani mmoja kila leo, eti leo mnawakamata watu hawa, upuzi mtupu katika nchi yetu ya wadanganyika

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2012

    Vidagaa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2012

    Lamba lamba ndio nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...