Mkurugenzi Mkuu na CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi wa safari za Shirika hilo la ndege jana kutoka Dar es Salaam hadi Lusaka Zambia kupitia Lubumbash.Hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz. SOURCE:FATHER KIDEVU BLOG
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi, John Thomas James Mngodo akizungumza kaatika hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz.
Mgeni Rasmi, Naibu Wazizi wa Usafirishaji, Kazi, Usambazaji na mawasiliano wa Zambia, Samuel Mukupa akizungumza jana katika tafrija maalum ya uzinduzi wa safari za Ndege za Kampuni ya Precision Air kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka kupitia Lubumbashi. Mukupa alisema mbali ya kuzidisha mahusionao baina ya Tanzania na Zambia lakini pia itawasaidia sana wafanya biashara wa Zambia katika safari zao za kibiashara Tanzania.
Wageni mbalimbali wakifuatilia tafrija
Meneja Mkazi wa Afrika ya Kati wa Kampuni ya Precision Air, Emmanuel Mathias Ng'andu akiwa na Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo Anneth Nkini wakati wa tafrija hiyo.
Viongozi wakishangilia jambo.
Wageni mbalimbali wakiwepo na wafanyakazi wa Precision Air wakifuatilia matukio.
CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko (kulia) akiwaongoza wafanyakazi wake kucheza edudha...
Mkurugenzi wa Masoko, Patriki Ndekana , (kushoto), Meneja Mauzo, Tuntufye Mwambusi, Hilda Lema, Mariam Ismail na Meneja Mkazi wa Afrika ya Kati wa Kampuni ya Precision Air, Emmanuel Mathias Ng'andu wakipamba moto katika EDUDHA.
Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Afrika, Timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' Honor Janza nae alikuwepo. Picha na mpiganaji Mroki Mroki
Hongereni Precition Air kwa kukuza biashara. Shida yangu ni kwamba mbona jina la ndege yenu/shirika lenu haliitangazi nchi? Ningependekeza mufanye rejeo(review) la jina lenu ili angalau liitangaze nchi. Mfano mngeiita PRECISSION TANZANIA au "PRECISSION, the pride of Tanzania". Tunajua ATCL walipaswa kuitangaza nchi kwa kutumia ndege zao lakini wameshashindwa kufanya hivyo.
ReplyDeleteNathani kulikuwa na Tanzania finest slogan ambayo nathani tayari inatangaza Tanzania
ReplyDeletePrecisely that is the point, Air Tanzania imechafua sifa ya Tanzania katika uwezo wetu wa biashara ya anga. Kuna kazi kweli kweli. So, Precision wasije wakajikuta wanafukuza wateja. Inauma, lakini huu ndiyo ukweli wa nchi yetu katika anga. Wacha ATC(L) wenyewe waendelee kujisafisha na kuisafisha nchi.
ReplyDeleteWadau hapo juu mkumbuke pia kwamba Precision Air sio100% Tanzanian. Kuna share na Wakenya.
ReplyDeleteHuduma zao nzuri ukifanya booking kutoka Tanzania ila bookings za kutoka nje bado zina watesa.