Na Woinde Shizza,Arusha.

Viongozi 2000 wa makanisa mbalimbali kutoka katika nchi 5 wanatarajia kukutana jijini Arusha na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia za nchi,pamoja na mapigano ya kidini yalioibuka zanzibar

Askofu wa makanisa ya Intenational Evangelism Centre ya hapa nchini Eliud Isangya (pichani) alisema hayo wakati akifanya mahojiano na libeneke la kaskazini ofisini kwake ambapo alisema kuwa viongozi hao watakutana jijini hapa wiki ijayo.

"kwa sasa zipo changamoto kubwa sana ikiwemo changamoto ya mabadiliko ya tabia za nchi ambayo inawaasumbua wananchi wengi sana hasa wa vijijini lakini kama taasisi mbalimbali zikiwemo za dini zitawahamasisha hata waumini wake ni wazi kuwa jamii haitaweza kukumbwa na baa la ukame kwa maana hiyo tutajadili masuala kama hayo ambayo yanazitesa jamii za watanzania walio wengi."

Aidha alibainisha kuwa wanasayansi wanabuni vitu vipya na vina uwezo wa kuwasaidia jamii kwanini sisi kama wadau wa nchi hii tusiwe wabunifu wa kusadia hata kuombea taifa katika majanga mbalimbali ambayo ni kikwazo cha maendeleo,tunataka tufanye hivyo ili kurudisha hata vitu ambavyo vimepotea kwenye nchi hii ya Tanzania

Mbali na hayo Eliud alizitaka Taasisi nyingine za dini kuhakikisha kuwa kila mara zinayafanyia maombi changamoto ambazo zipo kwenye jamii kwa kuwa wao ndio wana nafasi kubwa sana ya kuweza kulikomboa taifa la Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2012

    Nadhani kuombea nchi umasikini utokomee mtakuwa mmeijali saana nchi hii.

    Na pia umasikini ni kipimo kizuri kama mnajibiwa au laa. Ambacho pia ni kipimo cha mahubiri yenu.

    Nafikiri watu wanataka kuponywa umasikini zaidi kuliko matatizo mengine kama majini n.k.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2012

    Bado waandishi mnaojukumu kubwa kwa kutenda kazi zenu kwa haki na wajibu sahihi.

    Mkuu wa makanisa nawe unajukumu kwa kutosema ukweli juu ya hayo mapigano ya kidini Zanzibar hakika utawajibila kwa muumba wako.

    Changamoto ya mapigano ya kidini haina nafasi Zanzibar na haijatokea na wala haitatokea kwa uwezo wa Allah.Nakutakieni kheri ya maombi salama.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2012

    Nani alikwambia Znz kuna mapigano ya kidini???! Acha propaganda hizo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2012

    sasa hao wa Rwanda ,Burundi ,Congo ,Uganda na mocambique wasemeje kuhusu mapigano wakati kwao ndilo chimbuko na mbali na hayo znz hakuna mapigano ya dini.kwasababu nzn ASILIMIA 98 ni wa dini moja mapigano na nani.... wandishi wa habari wa tz mnatupeleka wapi jamani kuwa makin.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2012

    Vurugu za Zanzibar umeshakuwa mtaji wa wajanja! Iacheni nchi yetu, kwa maovu yenu maombi mtakayofanya yanaweza yakatuletea mabalaa ya kila namna!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...