Askari wakilinda usalama jana wakati Dk. Ulimboka anafikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbi, kupata matibabu.
Mchana huu sakata limetokea kati ya ndugu wa Dk. Ulimboka na waandishi wa habari waliotakiwa na Ulimboka kufanya nao mkutano, kukukataliwa kuingia chumba cha ICU, WAKIHOFIA USALAMA WAKE.
Licha ya madaktari kuwakubalia wanahabari kuingia lakini ndugu, akiwemo dadake walikataa katakata. Ndipo Madakatari walipoamua kuchukua wao rekoda na kamera za wanahabari na kwenda kumpiga picha pamoja na kumrekodi
Nampongeza sana huyu dada yake Ulimboka, anaakili sana, mtu mgonjwaa yuko kwenye chumba cha watu mahututi mnaita wanahabari wa nini kama sio dili hiyo.
ReplyDeleteUlimboka katolewa muhanga na watu wanaotaka umaarufu sasa wanataka wampige mapicha yatandaze kwenye magazeti ili iwe nini?
Tumemuona yule mama wa haki za binadamu kafika yeye kabla ya ndugu za Ulimboka, kapigiwa yeye wakwanza usiku wa manane.............kama nani? Mama mtu mzima na familia yako unapigiwa usiku wa manane na vijana tu, unamahusiano gani na hawa viongozi wa migomo, kwa nini wasipige usalama wa taifa..........jamani kuna hiki kimetokea.
Safi kabisa wanasiasa wasitumia kabisa kitendo hiki kwa umaarufu, na hao wana haki za binadamu kama kweli ni watetea haki, basi wamuache Ulimboka apone, wamuombe apone atasema tu yaliomsibu na itabainika kweli utakapojitokeza.
mgonjwa mahututi madaktari nao wanampiga picha????? udaktari wetu kazi kweli kweli
ReplyDeletenakuunga mkono mdau juu, hongera sana dada kwa uamuzi wenye ujasiri na hekima ya kuzuia vyombo vya habari kumuhoji na kupiga picha mgonjwa, nashauri na hao madakitari wanaopewa kamera nao ungewazuia vile vile
ReplyDeleteMahesabu yamegongana. Manake naona tamko la serikali bungeni lili kuwa lina "assume" huyu bwana hayuko tena duniani.
ReplyDeleteSasa hesabu zimegoma imebidi Tamko nalo Lishindikane.
Hivi sasa Dr. Ulimboka amekuwa ni public figure hivyo ni haki kwa waandishi wa habari kupata taarifa kutoka kwake ikiwa ni pamoja na kupata hiyo picha yake.
ReplyDeleteDr. Ulimboka, next time make sure you have eye witness around and Berreta 10+ in your pocket, inaonekana walidhani umekufa kumbe ungali hali, nawe ndiwe shahidi wa kwanza kutuambia walikuwa wanasema nini wakati wanakupiga? ili tupate kujua waliokupiga siyo wale unao gombea nao wanawake, bali ni wale wanaozuia Mgomo wa Madakta (serikali).
ReplyDeleteWhere have you been all those days kumpa ulinzi huyu mtu mpaka anakumbwa na mkasa wa kupigwa na kuteswa kiasi hiki, ni maumivu makali aliyonayo, anastahili kupumzika sawa but wananchi nao wanataka kujua kuhusu afya yake. Ni public figure Dkt. Ulimboka.
ReplyDeleteDr.Ulimboka kweli amekombolewa na mwenyezi Mungu Kama jina lake alilopewa na mama yake.ukweli utasemwa nani aliyewatuma hao vijana kumpiga mtu anapodai haki zake. Madaktari wafaida kubwa sana nchini,walipwe haki zao wanazo zitaka,wa bunge kazi hawafanyi walipwa 10m,umewahi sikia wapi ulaya kwenyewe wanawatetemekea madaktari wao,kesi eyende kwa human rights Kama kweli kuna haki za binadamu Tanzania.Get well soon Dr.Ulimboka,
ReplyDeletealiyekuwa anakunywa nae mbona hatumsikii. hili ni tukiola kijambazi wala serikalihaina mkono, angetii madai yao asingeumizwa. LKN AMEJALI MALI KULIKO UHAI NDIO MAANA YUKO TAYARI KUBORESHA MIGOMO WATU WAFE. HAO MADAKTARI WENGI FAMILIA ZAO HAZIBIWI HUKO. WARUDI KAZINI WAKAFANYE KAZI.
ReplyDelete