Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam Octoba 30, 2012 mwaka huu itasoma hukumu ya washitakiwa wanaodaiwa kumuua Marehemu Swetu Fundikira. Washitakiwa hao ambao ni Rhoda Robart askari wa JKT, Ally Ngumbe wa JWTZ na Mohamed Rashid mtumishi wa JKT.
Upande wa mashitaka katika kesi hiyo uliwasilisha vielelezo viwili na mashahidi sita akiwemo daktari aliyechunguza mwili wa marehemu na Benedict Kinyaiya ambaye ni mtangazaji wa TBC.
Washitakiwa kwa upande wao hawakuwa na shahidi walitoa ushahidi wao wenyewe baada ya kukutwa na kesi ya kujibu katika kesi hiyo ya kuua kwa kukusudia.
Wazee wa baraza katika maamuzi yao yaliyotolewa leo, walisema kuwa wanaona washitakiwa hao watatu hawana hatia na hivyo waachiwe.
Majuto ni Mjukuu, naamini mnatamani kama ingewezekana kurudisha/reverse tukio mngefanya hivyo but it is too late. Najua mnasikitika kufupisha maisha ya mtanzania mwenzeni kwa titu ambacho mngeweza kutengeneza au kununua tena.
ReplyDeleteDunia tunapita tupendane wabongo japo kiduchu.
Hee wazee wa baraza wanaona waheshimiwa hawana hatia...
ReplyDeleteNdio maana kabla ya tendo lolote au kauli fikiria kwanza!
ReplyDeleteUsipofuata kanuni hii mara zote ndio utakuta watu wamesha kwama na hawan uwezo wa kujikwamua kama hawa wauaji!
Umwamba, mabavu na ubabe una hasara zake ndio kama hawa Maafande mambo yaliyowafika!
ReplyDeleteWaachwie? Ili baraza linamaana gani?
ReplyDelete