Timu ya soka ya wanawake ya wenye umri chini ya miaka 17 ya Temeke, imeifunga wenzao wa Lindi 4-0 kwenye muendelezo wa michuano ya Airtel Rising Stars uliochezwa jana asubuhi, Jumanne Juni 12.

Magoli ya Temeke yaliwekwa kimiani na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Fatuma Iddi kwenye dakika ya 13 na 19. Arafa Abdul waliwafungia Temeke goli la tatu huku Niewel Halafan akimalizia kazi kwenye dakika ya 58.

Wakati huo huo, timu ya Mpira wa Miguu ya Mbeya iliifunga timu ya Arusha mabao 2-1 katika pazia la kufungua mchezo wa fainali Ngazi ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa 17 yanayojulikana kama Airtel Raising Stars uliofanyika Jumatatu, Juni 11 ya wiki hii kwenye Uwanja wa Karume  jijini Dar es Salaam.

Huku michuano hiyo ikiwa imetanguliwa na mechi ya wasichana baina ya Mikoa hiyo miwili huku Mbeya wakisinda 3-2, Timu ya Arusha ya wavulana walifungua mechi hiyo kwa kasi lakini nguvu zao hazikuweza kuzaa matunda kabla ya vijana wa Mbeya kufunga goli dakika ya tisa kupitia mchezaji wake Mussa Msape.

Goli hilo la timu ya Arusha liliwafanya wachezaji hao kufikiria kutimiza ndoto zao kuwa za kweli ambapo dakika ya 24 mchezaji Shabaaan Jabir wa Arusha aliwatoka walinda mlango wa Mbeya na kupachika goli hilo.

Ndoto zao zilizimwa kwa goli la ushindi la timu ya Mbeya liliweka kinywani na mshambuliaji Stanley Kaduma aliyokuwa ni pasi nzuri kutoka kwa washambuliaji wa mbele. Huku kipindi cha pili kikiwa kimetawaliwa
na pasi na kukosa magoli.

Mbeya wasichana walipata goli lao kwa kwanza dakika ya saba kupitia mchezaji wake Lucia Venance huku dakika ya 25 Vaileth Mcholuosi akipachika goli la pili huko la mwisho likiwekwa kinywani na Naomi
Lucas dakika ya 40 huku timu ya Arusha magoli yale yalifungwa dakika ya 12 kupitia Irine Venance na Venance huyo huyo kupachika goli la pili dakika ya 27.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...