Lori la Mchanga likipiga overtake huku gari nyingine ikiwa inakuja kwa mbele,uendeshaji huu umekuwa ukiendelea siku hadi siku katika barabara mbali mbali hapa nchini.
 Basi la Aboud nalo likiyakata magari mengine.
 hilo nalo ni hivyo hivyooo
 Yaani imekuwa ni kama kamchezo vulee.
 Huyu nafikiri anawahisha mgonjwa.
Hawa nao kwenye mlima Kitonga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2012

    kwa uendeshaji huu ajali hazitaisha tz. mama N. dsm

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2012

    Hii ni evidence tosha kwa trafiki kuwa-arrest madereva wa magari haya kwa kuhatarisha maisha yao na ya wapita njia wengine. Ndio hivi hivi ajali zinazoua watu wengi zinavyotokea. Huwa tunajiuliza inakuwaje.. kumbe jibu tumelipata sasa. Ushauri wangu kwa wahusika wa trafiki ni kuwa wawafungulie mashtaka mara moja hawa madereva. Na kwa wamiliki wa mabasi haya wawafukuze kazi mara moja hawa madereva wazembe wasiojali maisha ya watu. Ni uwajibikaji tu ndio unatakiwa sasa, kila mtu afanye kazi yake. Wenzetu Ulaya picha na video kama hivi ndio vinatumika kuwachukulia hatua watu kama hawa. Wahusika fanyeni kazi yenu sasa!!

    Exception yaweza kuwa gari la wagonjwa. In absence of maelezo zaidi ni ngumu kumuhukumu dereva. Lakini dereva wa gari ya mbele alitakiwa apishe ili gari ya wagonjwa lipite kama kulikuwa na mgonjwa ndani na limepiga king'ora.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2012

    oh my God hayo hilo basi linakata basi lingine na mbele kabisa anaona kuna kona? non this is not acceptable jamani.

    polisi wa barabarani wako wapi? wachukue reg no za haya magari wawachukulie hatu labda itasaidia.

    SAD

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2012

    Huyo dereva wa Bus la Sumry ni jambazi wa barabarani kabisa. Haiingii akilini ku-overtake kwenye kona kali tena sehemu hatari kama hiyo ya mlima Kitonga. Kuna haja ya kuwa na Patrol na madereva kama hawa wanyang'anywe leseni zao mara moja.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2012

    Naomba Mungu Serikali ilione hili na kuchukua hatua mara moja ili liwe somo kwa wengine. Sidhani kama kuna kiongozi yeyote ambaye ndugu yake angukuwepo kwenye gari lolote angefurahishwa, achilia mbali viongozi ni wa wananchi wote.
    1. Madereva wa magari washitakiwa sawasawa na kosa la anayetaka kujiua au kuua wenzake,,hakuna cha bahati mbaya hapa basi ni uzembe na kiburi au jeuri kuwa hakuna cha kuwazuia
    2. kwa tafsiri nyingine nachelea kusema ni kuitukana serikali na zaidi ya yote kukosa hofu ya MUNGU. mpiga picha Mungu akubariki sana maana hivi ni kama kina jerry walivyofanya kufichua uhalifu

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2012

    Hapa sio Issue ya askari wa usalama Barabarani ni issue ya Abiria wenyewe Ndani ya Gari wanakuwa Mazezeta Hadi wanashindwa Kukemea Uzembe Huu!! Kwani Trafic Police always atakuwepo Kwenye Uzembe Huu wa Kupindukia??

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2012

    hii inatokana na sheria ifuatwi maana hapo kuna alama zinazozuia kufanya tendo mojawapo na kama sio alama ata na hao madreva wanaofanya hivyo na abiria wanaona nakufurahia huo mchezo nashindwa kujua ikishatokea ajari nani atalaumiwa? sheria ifanye kazi yake madereva wa aina hii ni kukamata na kufunga mwezi na faini juu akitoka likuwa fundisho kwa wenye tabia za aina hiyo

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2012

    Huyo dereva wa hilo basi anaye ovetake kwenye kona kali kitonga anatakiwa afungwe kwa kuhatarisha usalama wa abiria na watumiaje mengine wa barabara. Imagine kuna gari nyingine inatokea upande mwingine ghafla itakuwaje?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2012

    Kilio changu zaidi ni kwa hilo gari la wagonjwa. Yaani nalo linatafuta majeruhi wa kubeba au na wao wabebwe!!!!. Kam alikuwa na mgonjwa au haraka si, alipaswa aombe apishwe na huyo wa mbele yake? Yaani watuogopi kifo wala kuwasababishia wengine mauti!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2012

    YAANI MACHOZI YANANITOKA HASA MADEREVA MAGARI HASA MABASI WANAVYOCHEZEA MAISHA YA WATANZANIA.

    HAKUNA ATAKAYEPONA KWA HAWA MADEREVA VICHAA NA WAVUTA BANGI.

    MUNGU TUHURUMIE WATANZANIA MAANA TUPO KWENYE FOLENI YA MACHINJONI, TUNASUBIRI KUCHINJWA MUDA WOTEWOTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...