Hapa ni Askari wa Usalama Barabarani wakitokea katika sehemu waliyokuwa wamejificha ili kuangalia mwendo kasi wa magari yanayopita katika njia hiyo kwa kutumia kifaa maalumu (kwa jina maarufu Tochi) na kuingia ghafla barabarani kwa lengo la kuikamata Basi hii ambayo ilionekana ikienda kwa mwendo ambao hautakiwi katika eneo hilo.
 Basi hiyo ililazimika kumkwepa askari yule ambaye alikuwa akielekea barabarani kwa kukimbia,jambo ambalo linaweza sababisha ajali kwani sehemu hiyo sio salama kwani ni kwenye mwinuko na pia hakuna nafasi ya maegesho,vile vile kama dereva wa basi hili angekuwa na spidi kubwa zaidi ya hii aliyonayo hapa na kwa namna alivyokuwa akimkwepa askari huyo,labda sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine.
 Basi ile haikuweza kusimama pale pale hivyo ilisogea mbele zaidi na sehemu ambayo ni salama (kituo cha Mlandizi) na kusimama.ambapo askari huyo alilazimika kwenda mpaka ilipo basi.(kilichoendelea huko sijui).
Afande akiingalia kwa makini Basi hiyo ili aone kama itaweza kusimama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2012

    Hao matrafic wana hiyo tabia sana hasa barabara ya dar -iringa wanajificha vichakani halafu wanakurupuka ghafla na kusimamisha gari kisha wanakwambia uwape hela ili uondoke.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2012

    lazima wafanye hivyo kwasababu wakisimama pemben ya barabara c wanawona kwa mbali wanapunguza mwendo,lazma askar wawe wabunifu so thy can achv smthng

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2012

    Hawa jamaa ni kero.

    Wanacho kera ni pale wanapojificha.

    Hii inakua kama vile ni lazima wakamate gari kwa hyo tochi.

    Utawaona wanatoka kichakani ghafla na wanaweza kusababisha ajali.

    Mdau - znz

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2012

    Tunaomba maelezo kutoka kwa wahusika vipima mwendo kasi vinavyotakiwa kufanya kazi.Ukiweka sehemu maalum ya kupimia mwendo kasi,ni 'obvious'kwamba madereva watafika maeneo yale watapunguza mwendo, baada ya hapo wataongeza mwendo.Hizi 'random' checks' nakubaliana nazo kabisa 100%,ninachopingana nacho ni kusimamisha gari papo hapo.Angalia hapo Askari anaweza kusababisha ajali kweli.

    Kwani Askari hawezi kumulika hicho "kitochi"(Samahani Wachagga) halafu akachukua namba za gari tu ,zikatumwa huko linakoenda faini kali ikalipwa huko huko?Tuwe na utaratibu mzuri.Twende na wakati,lazima vyombo husika vilete teknolojia ya database,makosa yatunzwe kwenye database.Bila hivi rushwa barabarani haitaisha.

    David V

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2012

    wapuuzi sana hawa askari na ipo siku watagongwa kwa kupenda kuingia barabarani hovyo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2012

    Tatizo ni rushwa bongo sio utendaji.Nakumbuka sana huwa nikiwa bongo unakuta madereva wanavunja sheria kibao na trafki akiwaona anaomba kudakishwa then anaendelea na safari.Utakuta hata hawa wanaoonekana hapa wakilisimamisha hili basi ,huenda wameishia kupena mkono na konda na kudakishwa ,then safari inaendelea.Hakuna lolote .Ndiyo maana kila kukicha ajli kibao na wananchi wanapoteza maisha yao na kuacha watoto yatima kibao au kuwa vilema.Serikali na polisi ingekuwa serious ktk utendaji mambo mengi ,ajali nyingi zingezuiwa na zisingetokea.Mdau big Joe wa Ughaibuni

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2012

    Hii ni hatari sana. Hawa ni maofisa wa usalama au ajali barabarani.
    Nauliza hivyo kwa sababu cku zote wao wanakimbilia makosa kuliko kulinda na kusaidia..

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2012

    Hawa waliwahi kusababisha ajali mbaya sana Tegeta. Sitasahau. Wanafanya uzembe na makusudi mbovu kwa kuwa hawawajibishwi kwa haki.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2012

    Big up sana mdau uliepata picha hii. kweli bongo tambarale. hapo ukisimama anakuletea tochi yake na kukuonesha km alizorekodi. unajiuliza amerekodi namna gani wizi mtupu!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2012

    Kwa style yao hii nahisi harufu ya damu muda si mrefu.Wacha wao wanaenda kichwa kichwa barabarani

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2012

    Mdau naomba nitumie hzi picha please please kwenye gmassawe2001@yahoo.com

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2012

    Hakuna barabara ya Dar-Iringa

    ReplyDelete
  13. Jana tarehe 26/7/2012 nilikuwa nasafiri kutoka Mbeya.
    Gari nililopanda linaitwa Green Star Express, namba T 525 BVP . Dereva wa gari lile si mzuri na hakuwa anajali kama amebeba watu. mlima Kitonga na mabonde ya Uduzungwa alikuwa akiendesha rafu sana mpaka mabegi yanadondokea watu, mbugani Mikumi alikuwa anapita kwa kasi kubwa bila kuzingatia ishara zilizowekwa. kisa anaenda na muda. Unaendaje na muda? Una mkataba na magurudumu wewe?kosa lako unataka kuwapa vilema au vilio wenzako? Acha tena Acha...samahani kama mliyotuomba haisaidii lolote kwa mchezo wa hatari kama huu. Msije mkapoteza Image ya kampuni yenu bure kwa mambo ya kijinga.Mmiliki kama unajali biashara yako ondoa mtu huyu.Atakuharibia..na Polisi waachwe wafanye kazi yao lakini kwa njia ya kisasa siyo hii.

    Maeda, F
    Mdau aliyesafiri.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2012

    Askari maisha kuendekeza msemo wa maisha magumu mtatumaliza. USITOE WALA KUPOKEA RUSHWA, RUSHWA INAPOFUSHA MACHO. unakuwa huoni hata kitu mbadala cha kufanya zaidi ya kusubiri kudakishwa vihela vya njiani vya kula tu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2012

    Saidi Mwema should sack these corrupt idiots. Hawa wangesababisha ajali mbaya sana.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 27, 2012

    Waacheni wafanye kazi yao. Kama staili hii inakukera basi tuwanunulie magari ya kasi yafukuzane na hao waendesha kasi na kusababisha vifo kila siku. Tembea dunia hii na utakuta wanafanya hivyo hivyo kuwakamata wanaoendesha kasi zaidi ya sheria. Duhh!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 27, 2012

    Nilipo mimi ughaibuni wanajificha hivyo hivyo, of course siyo vichakani kwa kuwa havipo ila wanakuwa na unmarked cars, and motorcycles wamezitega mahali wanakupiga tochim tofauti yao wakikubaini wanamwarifu mwenzao aliye mbele kwa radio call au simu ili akusimamishe.Nisichokielewa hapo ni kuwa jamaa amekataa amri halali ya polisi na anapeta tu huku thubutu!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 27, 2012

    Jamani ehe, hiyo ndiyo technology impya na itafanya kazi sana kama hawa askari watapewa magari au pikipiki. Huku tunakoishi kwa muda Marekani hivi ndivyo watu wanavyokamatwa nakisha kutozwa faini nakupewa points kwenye driver license yako. ukifikisha amount fulani ya points has 10, unanyanganywa license yako kwa muda mpaka points zishuke. Speeding tickets ni point tatu na accident point tano. Speeding ticket inakwaa kwenye record yako kwa miaka mitatu na accident ticket kwa miaka mitano. Halafu insurance yako ipo determined na points zako, hivyo more points high insurance premium.

    Serikali inabidi imtume mtu huku apate huu ujuzi.

    Thanks

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 27, 2012

    Jamani ehe, hiyo ndiyo technology impya na itafanya kazi sana kama hawa askari watapewa magari au pikipiki. Huku tunakoishi kwa muda Marekani hivi ndivyo watu wanavyokamatwa nakisha kutozwa faini nakupewa points kwenye driver license yako. ukifikisha amount fulani ya points has 10, unanyanganywa license yako kwa muda mpaka points zishuke. Speeding tickets ni point tatu na accident point tano. Speeding ticket inakwaa kwenye record yako kwa miaka mitatu na accident ticket kwa miaka mitano. Halafu insurance yako ipo determined na points zako, hivyo more points high insurance premium.

    Serikali inabidi imtume mtu huku apate huu ujuzi.

    Thanks

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 27, 2012

    Hamna kitu hapo, kuanzia wakubwa wao mpaka chini wote kitu kimoja. Hao wanatumwa kila siku kuleta fungu usione wanjiamini hivyo. Mtapiga kelel bure tu. Cha muhimu hapa wadau tuanzishe kampeni maalum yakuwanasisha pesa za moto. Mimi walinipiga faini 30,000 Kibaha Mail moja kwa speed ya 55 wakati inatakiwa 50. Wakakataa kunipa risiti hadi leo nina fomu tu. wanadai niiende nirudi mpaka Kibaha Ofisi kwao nipewe risti. Nilipokuwa narudi nikafanya makusudi wakanikamata tena nikawapa 5,000 wakashshangilia sana. JHata namba ya huyo askari ninayo. Waziri mhusika angalia sana kibarua chako.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 27, 2012

    Sir Richard Mayne (1829) wrote:

    "The primary object of an efficient police is the prevention of crime: the next that of detection and punishment of offenders if crime is committed. To these ends all the efforts of police must be directed. The protection of life and property, the preservation of public tranquillity, and the absence of crime, will alone prove whether those efforts have been successful and whether the objects for which the police were appointed have been attained."


    Kazi ya police wa Tanzania si kuzuia bali kuomba crime ifanyike ili wapate mwanya wa kuombea rushwa, na hii ni kinyume kabisa cha malengo ya wao kuwapo. Wangekuwa wanavizia hivyo na kisha kuwakamata madereva na kuwafungulia charges na kisha wanaadhibiwa ili wasirudie tena ningesema huenda wanataka kuwafanya madereva wawe makini bila hata ya kuona police mbele yao.

    Kuna wakati niliwahi kushangaa eti police wanalalamika kuwa wenye mabasi yenye radio call wanaambiana kuhusu uwepo wa polisi na hivyo kuendesha polepole ili kukacha mitego yao, this is bullshit!, badala ya kujisifia kuwa uwepo wao unapunguza crime wao wanalalamika kuwa unapunguza crime ili wasiwashike.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 27, 2012

    Awali ya yote hiyo teknolojia ipo tangu zamani, kama ulikuwa hujui ni wewe tu, utata hapo upo kwenye eneo ambao Askali wapo kama unavyoona hapo kuna Solid White line upande wa hilo bus maana yake hakuna ku-overtake sasa hilo bus likisimama gari zinazotoka nyuma zitapita vipi, ni vizuri maafande wakijificha sehema salama zaidi.

    Mdau UK

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 27, 2012

    Wakati mwingine huwa wanawabambikia madereva kwa kuwaonyesha wamekwenda speed kumbe ile record aliyokuonyesha hawakuifuta inakuwa ya gari nyingine, usipoangalia speed meter yako unakuwa umekwisha

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 28, 2012

    Mijizi mitupu na njaa ndiyo inayowasumbua matrafik wa bongo,kazi kushibisha matumbo yao tu,lakini hawafanyi kazi zao kwa uadilifu,matrafiki na polisi wananuka RUSHWA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...