Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Heshima msanii mstaafu wa muziki wa Taarab, Mwanacha Hassan Kijole (65) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana Julai 6, 2012 katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Mohamed Baucha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Heshima msanii mstaafu wa muziki wa Taarab, Mwanacha Hassan Kijole (65) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji Fm, Mohamed Seif Khatib (kushoto) ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Mohamed Baucha.
 Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji Fm, Mohamed Seif Khatib, akimkabidhi Tuzo msanii, Rukia Ramadhan, aliyeibuka mshindi kwa kuwa mwimbaji bora wa mwaka wa Taarab Aslia, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za  Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana Julai 6, 2012 katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Mkuu, akimkabidhi Tuzo mwanamuziki wa kundi la Taarab la Zanzibar One Modern Taarab, Saada Nassor, baada ya kuibuka mshindi kwa kuwa Msanii bora wa Kike wa mwaka wa muziki wa Taarab ya Kisasa, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2012

    Bi Mwanaacha Hassan kweli wa zamani sana. pamoja na Bi Rukia, Ramadhan, sasa mbona Bi Mwanahawa Ally mmemuacha? Japokuwa sometimes anaimbia vikundi vya Bara, lakini ingependeza na yeye kama angeweza kutunikiwa TUZO yake mithili ya hao wenzake, mana katika muziki wa taarab na yeye ni miongoni mwa hao waliotunukiwa hapo. Pia kwa namna moja au nyingine wametokea mbali sana wakiwa pamoja enzi hizo tangu ikiwa ile taarab 'asilia' mpaka ya leo hii tuliyoibatiza 'Modern' Bi Mwanahawa yeye angalipo. Tungejaribu kuliangalia na hilo na yeye ingependeza sana kama angepata kutunukiwa TUZO yake katika hafla hiyo, matokeo yake hakutiwa japo hesabuni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2012

    kweli mdau hata Zuhura shaaban nae ni mwimbaji mzuri na wa zamani kidogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...