Wakazi wa eneo ya Manzese jijini Dar wakikatisha barabara ya Morogoro rodi kwa taabu kwenda ng'ambo ya pili kutokana na kuchimbwa kwa eneo la katikati ya barabara hiyo ambayo ipo katika mpango wa Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya kisasa na yaendayo kasi,kama walivyokutwa na kamera man wa Globu ya Jamii mchana wa leo.
Home
Unlabelled
hali ilivyo eneo la Manzese leo hii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Sijui ni mtindio wa ubongo? Ishu za kuwadharau waenda kwa miguu ni ishu chafu sana jamani, unless hawapaswi kuvukia hapo, and if only that is practically implementable.
ReplyDeletemanzese kuna daraja bwana watu wabishi tu
ReplyDeleteNadhani hata kama kulikuwa na huo uchimbwaji wa eneo hilo la katikati ya barabara, but still wangewafikiria na hao 'pedestrians' (wenda kwa miguu), angalau wangetengenezea japo kwa muda tu sehem maalum ya kupitia , while other parts of the road zikiendelea na hiyo construction yao, kuliko hiyo adhabu ya kuchupa wakichupa na tena, mara nguo inakurarukia hapo hapo, pia inaweza kupelekea mtu kuchupa vibaya akateguka au kuvunjika kiungo, kwani humo mna kina mama, wazee na hata watoto na kina ndo hicho kama kinavyoonekana hapo.
ReplyDeleteMtaka cha uvunguni, sharti ainame. Maendeleo yoyote yanahitaji uvumilivu once you in process, ila nafikiri wanaweza kutumia daraja linaloonekana kwa mbele kidogo kwenye hiyo picha.
ReplyDeleteNdo gharama za maendeleo jamani, tuwe wapole mambo mazuri yaja wajameni
ReplyDeleteMdau wa kwanza, bongo kuna ubabe mwingi sana na kutokujaliana. Hata majengo yetu mengi ya ghorofa yanajengwa bila lift. Halafu unakuta ofisi inahusika na huduma hata kwa walemavu na wazee lakini iko ghorofani na hamna lift. Najua umeme wetu una matatizo lakini kama tungekuwa tunajali mahitaji ya kila mtu tusingeshindwa kuweka standby jenereta kwenye maghorofa yetu.
ReplyDeleteBinadamu wengine kama ng'ombe, kwa mtazamo tu sio lazima kuvukia hapo walipo kwani ukiangalia hapo mbele kiogo kama mita kumi (hatua 10) utaona pamekaa vizuri na unaweza kuvuka bila matatizo.
ReplyDeleteHilo moja lakini zaidi ya hapo kwa kuangalia tu hapo sio mahali salama kwa kuvuka, kwani msongamano wa magari ni mkubwa na zaidi hakuna hata vivukio (Zebra crossing)
Hata hivyo mkandarasi alitakiwa kuweka alama za usalama kama hakuna njia au ujenzi unaendelea ni hatari ikiwa ni pamoja na vizuio kama Warning tape na kadhalika
Mdau Engineer
Tatizo hawataki kuvuka maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kuvuka sasa badala yake wanavuka hovyo hivyo kusababisha ajali na foleni. Inasikitisha sana jamani tubadilike. Na hizi njia zinazo ongezeka watagongwa wengi
ReplyDeleteishu ni wabongo ni watu wavivu kuzunguka kwenye sehemu ya kuvukia wanaona tabu.Hio ipo kwa watu wa magari na waenda kwa miguu.Na ndio waaribifua wakuu wa barabara zetu.
ReplyDeleteThanks
Mdau wa Dar
huko uliko,wanafanya je wanapojenga mabarabara. Umelaani na hapo hapo ukajijibu mwenyewe,yes hapo si pahala pa kuvukia,na kila sehemu hapa duniani ziko nyakati za dharura,tatizo lako wewe ni fala tu.Zebedayo.
ReplyDeleteNakukumbusheni kutumia "barabara ya morogoro au morogoro road" na sio barabara ya morogoro rodi
ReplyDeleteNdugu yangu wa hapo juu mimi ni mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo sema kasumba zetu ukizoea kuvukia hapo hapo hata kama kunatengenezwa unang'ang'ania. Sehemu za kuvuka kwa miguu zipo sema mazoea yao yana taabu. Mtu hatua kama tano au kumi kutoka kivuko alichozoea kikibadilishwa analalamika na kuanza kujipitisha pale pale
ReplyDeleteJana niliona mama kabeba mtoto mgongoni akipanda kutoka kwenye hili 'korongo' la manzese.
ReplyDeleteKwani mdau namba 1 hujui kuwa manzese wana daraja la kuvukia juu, au ww lile unaona ni pambo la mji...hao wananchi wenyewe wamewekewa sehemu za kuvukia (ZEBRA LINE) lkn ni wangapi wanazitumia,? Ni barabara ngapi umeshuhudia ktk sehemu ambazo si za kuvukia kuna vichochoro vya waenda kwa miguu walivyobuni wenyewe?
ReplyDeleteWajinga ni sisi wananchi wala hakuna anayetudharau kama tutafuta sheria za barabarani zilizowekwa...
Nchi zilizoendelea construction site ni eneo la hatari na wanaweka bango "Danger men at work"!!!
ReplyDeleteWanaotakiwa kuwa eneo hilo lazima wawe wamevaa "safety first" equipment. Na hairuhusiwi kipita karibu.
Hapa kwetu kuna utamaduni wa kijifanyia mambo kienyejienyeji, maeneo ya kazi hayaheshimiwi, mtu anapita chini ya Crane bila wasiwasi, au mtu anaenda sambamba na bulldozer.
Bila shaka hawaruhusiwi kupita maeneo hayo, hakuna ufuatiliaji, ukiwazuia hawatasikia, utaonekana wewe ndio wa ajabu.
Anon hapo juu, mbona waenda kwa miguu wamewekewa flyover, kwa nini hawaitumii katika hali hii ambayo barabara inatengenezwa? Ni kutumia akili ya kuzaliwa tu wala hamna haja ya kulaumu wanaotaka kuleta maendeleo.
ReplyDelete