Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. MATANGALUJuly 25, 2012

    Nimeangalia mpaka dakika ya 5 na sekunde 33 hapa huyu mwanadada alipoanza kupayuka "you rich maaaan...." nikaacha kuangalia. Hashimu ni wazi akawa embarrassed na tabia pori za huyu mwanadada. Hii ukijumuisha na swali lake la kwanza kwamba "eti wewe unaweza kukojoa hadharani" imenifanya nione kumbe hii mkasi yenu ni Comedy show.
    Hashimu ni NBA star na amezoea kufanya interviews katika profesional level; sasa huyu dada anapayuka utadhania mwehu, mambo gani haya? Kisha mtu kama Hashimu siku nyingine akikataa kuhojiwa na watu kama hawa watamwambia anaringa na kujiona bab kubwa, au anasahau alikotoka.

    Hivi anatoka familia ya aina gani huyu classless twat?.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2012

    Strange kipindi,kama hivyo ndivyo vipindi vya TV huko Bongo,poleni sana

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2012

    Salama,hao vijana wako wanajuwa kweli kweli kuuliza maswali,hasa huyo miwani myeusi,,wanajitahidi sana,,,Ila tu Salama nilishasema mwanzo.sijui kama huwa unasoma comments za hapa kwa Michuzi,,Jaribu kuuliza vitu vya kiheshima heshima,,maana hicho kipindi chako nahisi watu wazima na watoto wao huwa wanaangalia,,ya leo hii cha mtoto!kuhusu kukojoa!Siku moja niliona unauliza habari zingine kabisa mpaka mwenyewe nikawa naona aibu,wakati niko peke yangu,,Je wenye kuangalia na watoto wao?
    La pili Salama punguza kuharibu kiswahili,au tutakuitia mzee kifimbo akuchape viboko,,Eti unasema 'MCHIZI ALIPOFARIKI',,ulikuwa unazungumzia marehemu Kanumba,,Ee jamani,,marehem nae anaitwa mchizi..
    Hashimu unaongea vizuri,huna Kiswanglish,ila tu Salama ndo anakuuliza kiuswanglish,,sasa na wewe anakuchanganya kabisa mpaka unaamua kutwanga KIINGLISWAHILI moja kwa moja,mpaka mwisho wa Reli Kigoma!
    Ahlam,,,London

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2012

    Yeah y'know no one cares to hire real professionals who know their job and who respect boundaries. I saw it and was like yo why am I watching this?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2012

    Huyu Salama nabidi hawe makini sana sana,hii mkasi tunaipenda sana sisi tulio nje ya nchi,lakini wakati mwingine ina utoto na ukomedi sana,
    kingine ni matumizi ya lugha,kama mahojiano ni ya kiswahili basi yae kiswahili,na kama ya English basi yawe english,kuliko kuchanganya mseto

    ReplyDelete
  6. Mdau.coventry.UKJuly 25, 2012

    Uandishi wa habari una maadili yake na heshima yake.nashindwa kuelewa huyu salama kutukana katika mahojiano wakati wote kama ndio hayo maadili ya uandishi.kumbuka hii ni taaluma ya watu wenye heshima ambao wanafunza jamii.kama umeona ni uhuni nenda katafute taaluma nyingine badala kupaka matope uandishi.umedhihirisha hauna adabu na nina wasiwasi kama kweli ulifudhu hii taaluma

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2012

    sasa hao sindio wanaitwa point 5...mbona kwangu point 0...sasa naona huu ndio wakati muuafaka wakuutumia kwenye kutoa maoni yetu ya maana na yenye maadiri mema kwenye jamii yetu...ili tukomeshe kabisa utoto utoto kama huu...hebu wadau nisaidieni jamani na tuwe wakweli hivi kipindi kama hiki tena hatari yenyewe kipindi chenyewe kinaonyeshwa muda ambao hata watoto wetu hawaja lala...sasa swari kwenu wadau wote je watoto wetu wakiangalia kipindi kama hiki watajifunza nini hasa..tena cha ajabu wengi wao wanaoitwa kwenda kuhojiwa ni hao hao mama zetu kaka zetu baba zetu dada zetu na wao bila ya woga kabisa au hata kuona aibu ili mradi auze sura au eti anaogopa asipo enda ataambiwa analinga aibu kwenu...mm kama mm..kamwe bora unambie nalinga kulikoni kutia sura yangu kwenye vipindi kama hivi...na ukitaka ushauli wa bule kwa jambo lililo kushindwa kwa mtu yoyote yule...nitafuteni..KWA JINA NAITWA....SITUMII facebook twita wala simu..bali natumia pesa na maisha yanakwenda kama kawaida..aksanteni wadau wote mungu awabariki.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2012

    Na nyie mliokuja na hoja zenu za taaluma acheni ushamba wenu hapa. Walioanzisha kipindi hiki ni wajasiliamali na ujasiliamali hausomewi. Ni sifa tuu "inherent character" ambayo mtu anazaliwa nayo, kama ambavyo mtu husomei kujua kuchora au kuwa na mbio. Kama mnaona kila kitu kinahitaji shule basi waambieni hao wasomi wenu waanzishe mkasi yao kisha muone wataishia wapi.

    Kuhusu huyu dada Salama Jabir ni kweli ana vitabia vya kupayuka lakini akiwa kama kijana anatakiwa aelekezwe tuu na afahamishwe umuhimu wa kipindi hiki katika jamii. Hakuna sababu yoyote ya kumkatisha tamaa, bali aelimishwe. Inawezekana anadhania kwamba kuleta "usela nondo" mwingi ni kivutio kwenye kipindi chake. Dada kaza buti, isipokuwa kipindi chako kama zamani kilikuwa cha kuchekesha, basi unatakiwa utambue kwamba kinakuwa kikubwa na kinaangaliwa na watu wazima na watoto wenye heshima zao. Kwa watoto wadogo ambao wanamuona Hashimu kama "role model" wao; siyo vyema kuangalia kipindi kama hiki huku kikiwa na usela nondo huu na lugha za hovyohovyo.
    Kwa ufupi rekebisha makosa hayo machache kisha kaza buti dada yangu na usikatishwe tamaa. Kipindi chenu tunakipenda, na hasa sisi wa ughaibuni.

    Shukrani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2012

    Bibie Salama,pole sana na shughuli,na haya tunayoyatoa hapa usiyatupie kisogo,Mkasi ni kipindi kifupi wa timu yako ni nzuri sana,lakini wewe mwenyewe Salama punguza utoto na kuwa
    mtaalamu na jaribu sana kujali na kujivunia kazi hii ya uwana habari,sio kuivunjia adhi,baadhi ya mbwe mbwe zako ni za kitoto,badilika Dada unategemewa na taifa na Mkasi inaangaliwa na wengi

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2012

    Si na uhakika na wachangiaji Wazamunda wa Bongo na Comment zao hapa maana hawana exposure, Lakini kwa Waliokua ugaibuni naona kama wanafiki tu na Fitina. Salama analeta revolution katika TV industries mnataka mambo ya 1947 ya Mchonga?! Big Up Salama, Kizazi cha Bongo cha sasa Tunataka Program kama hizo Chekini Ma Interviews ya wasanii ya states ambapo ndio tunaiga muziki wao ndio utasema salama hana adabu. Keep rolling salama and remember usitake kumridhisha kila mtu hutafanikiwa. Watanzania ni Fitina tu zimetujaa

    ReplyDelete
  11. Salama kwa ujumla kipindi chako kizuri, lakini kadri kinavyoendelea kupata umaarufu, umeanza kufanya baadhi ya wapenzi wake kukereka, khasa kwa huo uulizaji wako wa masuali usio na mpangilio maalumu wala kujali hadhi na heshma ya unaemfanyia mahojiano hayo. Umekuwa ukifyatuwa fyatuwa tuu! Almuradi wewe limekujia kinywani mwako, namna hiyo usaili wako unaonekana kuwa 'informal', huonekani kabisa kama umejiandaa nao, wakati mwingine unashindwa hata na hao vijana wako hapo katika kuuliza masuali. Tafadhali maintain your personality na khasa kama hiyo kazi ni mojawapo ya 'professional' zako. Otherwise, haipendezi kuwaona watu na heshma zao, wanakuja hapo wakiwa wamejiandaa vizuri kwa mahojiano, halafu wewe unaanza kuleta 'uchepe' wako, shame!

    Hata hivyo, kwa ujumla unastahili pongezi kwa kuweza kwenda nacho vizuri kipindi chako cha MKASI. Hakuna mkamilifu na makosa madogo madogo hayakosekani na ndio chachu ya kuweza kubaini wapi panataka marekebisho au kuboreshwa zaidi, hata hivyo bado hujachelewa, jirekebishe, unapokuwa kwenye kipindi, pia jaribu kuipa hadhi na heshma yake fani hii ya utangazaji na uandishi wa khabari kwa jumla. Kila la kheri na ufanisi zaidi katika kazi zako.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 26, 2012

    people are so uptight and serious on everything . what is Salama doing got some degree of journalism but the main concept is comedy, it is all over the world and people are making career out of it and taking up to $10 million a year.. If we decide to embrace globalism we shouldn't be so selective.I can honestly say its a good concept and bring our so called celebrity close to the community on the personal level. and Well at age of 25 Hasheem showing a lot of maturity ,thats lot of class from him.
    peace

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...