Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Uganda, Joseph Mayanja 'Jose Chameleone' usiku wa kuamkia leo amefunika vilivyo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini lililofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Chameleone aliwarusha mashabiki kwa baadhi ya nyimbo zake za zamani kama Mambo bado, Kipepeo na ile mpya iitwayo Valu Valu inayopendwa na watu wengi hapa Bongo.
Home
Unlabelled
JOSE CHAMELEONE AFUNIKA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI UWANJA WA TAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hivi ni kwa nini katika mikusanyiko kama hii akina dada huwa wachache mno? angalia picha zote hizo halafu ona ni akina dada wangapi wapo humo.
ReplyDeleteJee ni nini sababu hasa? wanaogopa kwa sababu za usalama wao? hawapendi aina hii ya muziki? hawawezi bei za kiingilio? wazazi na wapenzi wao hawawaruhusu? au ni nini hasa?
Jose Chameleone wewe ni king wa muziki Haki ya mama!
ReplyDeleteSiku zote kimaumbile wanawake na wanaume ni tofauti,kwa hiyo na hisia zao ni tofauti,,vitu kama hivi vijana wengi wa kiume ndo washabiki,na ukilinganisha kuwa watumbwizaji ni wavulana,,hapo kama angekuja Beyonce au Nyota Njema sijui nyota njema yule dada wa Kenya,,wewe ungeona wasichana kibao hapo
ReplyDeleteNa pia jambo jingine,,sana sana show za uwazi hivyo kama uwanjani kina dada huwa hawapendi,,wewe angalia kama katika maharusi au clubs ndo kuna msanii yeyote awe hata mvulana utawaona kina dada maana huwa wanapenda sana sehemu za heshima,,hapo wapo,ila sio wengi,,waliokuwepo wamekubuu
Ahlam,,London
Kina dada wanaogopa kubakwa. Si unajua jamii yetu bado ustaraabu mdogo kidogo.
ReplyDeleteVALU VALU(Walu walu?)
ReplyDeleteDavid V
naomba nikujibu anonymous wa Sun Jul 08, 01:48:00 PM 2012 ni kwamba sio kwamba wadada wengi hatupendi ila bado kuna mfumo dume kwenye jamii zetu...ya kwamba hata ruhusa ya kwenda huko hatupati..wazazi wetu,wapenzi wetu wamekuwa na ugumu wa kutupa ruhusa za kwenda maeneo kama hayo kwa sababu tofauti tofauti..na sababu nyingine ni kuhofia usalama! bado hakuna usalama mzuri pale uwanjani..
ReplyDeletewakina dada hawapendi kudhalilishwa na hata hivyo mzazi gani amruhusu binti yake usiku kama wanabakwa mchan kweupe je usiku itakuwaje
ReplyDelete