MARIA LOTI PHILLIPO DYAULI
Ni mwaka mmoja tangu Mama yetu mpenzi MARIA LOTI PHILLIPO DYAULI ulipoitwa na Bwana tarehe 26 Julai, 2011. Sisi wanao, wajukuu, shemeji zako, kaka na dada zako, wifi zako,Jirani zako, Marafiki zako na Wanakwaya wenzako wa Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front na Usharika wa Iambi Igyuli, Singida bado tunayo kumbukumbu ya mapenzi na tabasamu lako; huruma na wema wako, ujasiri na maono yako. Ulitufundisha kuimba, umeiacha familia yenye kipaji cha kuimba na kupiga kinanda, ukatulea katika kumjua na kumuabudu Mwenyezi Mungu. Hakika hakuna URITHI na ZAWADI zaidi ya hii uliotuachia. Hivyo hata kama macho yetu na mwili hayakuoni tena, wala mikono yetu haiwezi kukugusa tena Mama, lakini tunayo AMANI katika YESU KRISTO Bwana wetu na Roho Mtakatifu ambaye siku zote ameendelea kutufariji na kututia moyo.
Mama Maria Loti Phillipo Dyauli
Tutakukumbuka Daima.
Tunafarijika kwa maneno ya Mtume Paulo kwa Timotheo 2: 11 - 12
KAMA TUKIFA PAMOJA NAYE, TUTAISHI PAMOJA NAYE PIA.



Poleni sana kwa msiba mkubwa uliyowapata Mungu awatie nguvu na mzidi kumwombea mama yetu
ReplyDeletemary
Poleni sana Dagmary, Bertha Juliet, Edwin Mumbaiga, Ingrid Lois, Anne, Florence Alice na Richard. Muzidi kumcha Mungu wazazi wenu waliwalea katika kumuabudu Mungu. Talanta yenu ya uimbaji na kupiga piano, na vifaa vya muziki msiiache. Ingrid umekuwa muimbaji mzuri wa Kanisa alilokuwa anasali Mama na Baba yenu. Urithi mlioachiwa msiupoteze. Mungu awashike, awakumbatie na kuwatia moyo siku zote za maisha yenu. Ulale salama Mama Maria Loti Phillipo Dyauli, Asante
ReplyDelete