Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam tayari kutoa heshima kwa mashujaa wetu waliopigana vita mbalimbali nchini.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amirijeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumatano, Julai 25, 2012, amewaongoza Watanzania kuadhimisha Siku ya Mashujaa nchini katika shughuli iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amewasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja saa tatu na dakika 10 kujiunga na wananchi na viongozi wengine wa kitaifa akiwamo Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Pandu A. Kificho na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Viongozi wengine walikuwa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Saidi Mecky Sadiq, Meya wa jiji la Dar es Salaam Mheshimiwa Dkt. Didas Masaburi Jaji Kiongozi Mheshimiwa Fakhi Jundu.
Kabla ya kusomwa kwa dua kutoka madhehebu mbali mbali ya dini, Rais Kikwete na Amirijeshi Mkuu aliweka ngao na mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange ambaye aliweka sime, akifuatiwa na Mkuu wa Mabalozi Balozi Khalfan Mpango nchini ambaye aliweka shada la maua. Naye Meya Dkt. Masaburi aliweka mshale.
Kwenye dua zao, viongozi wote watatu wa dini ya Kiislamu na madhehebu ya kikristo waliiombea Tanzania iendelee kuwa nchi ya utulivu na amani na kuombea michakato mitatu muhimu ambayo inaendelea ama inaandaliwa kufanyika nchini iweze kwenda vizuri na kwa utulivu. Michakato hiyo ni Maandalizi ya Katiba Mpya, Sensa ya Watu na Makazi na Vitambulisho vya Taifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...