Ankal Habari..!

Katika harakati za kuimarisha zoezi la ukataji tiketi za treni ya abiria Menejimenti ya Kampuni ya Reli Tanzania _TRL imetoa
Mwongozo ufuatao:

TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA WATEJA WETU KWAMBA, KUANZIA JUMATATU JULAI 16, 2012 MTEJA YEYOTE ANAYETAKA KUNUNUA TIKETI YA TRENI LAZIMA AONESHE KITAMBULISHO CHAKE KWA KARANI MUUZA TIKETI BILA HIVYO HATUTAWEZA KUMHUDUMIA.

VITAMBULISHO VINAVYOTAMBULIKA NI VIFUATAVYO; KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA, LESENI MPYA YA UDEREVA, KITAMBULISHO CHA MUAJIRI, HATI YA KUSAFIRIA, KITAMBULISHO CHA SHULE, BARUA KUITOKA KWA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MITAA NAKADHALIKA UTARATIBU HUU MPYA NI KWA AJILI YA KUONGEZA UFANISI NA KUBORESHA HUDUMA ZETU KWA WATEJA WETU!

IMETOLEWA NA MENEJA UHUSIANO ( MIDLADJY MAEZ) KWA NIABA YA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL MHANDISI KIPALLO AMAN KISAMFU

DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2012

    Hapa ni ukiritimba tu unaongezwa hakuna kuboresha chochote wakati inatambulika kwamba ni wananchi wachache sana wenye vitambulisho maana usafiri huu unatumiwa na watu masikini mno wa vijijini kwa kuwa ni wa bei rahisi, sidhani kama itasaidia au itaongeza adha tu.

    ReplyDelete
  2. Kweli hili shirika limeishiwa sera,sasa kitambulisho cha nini mimi nataka kusafiri ndani ya nchi?kwahiyo kama sina kitambulisho sisafiri na hizo treni zenu?halafu inasaidia nini au inapunguza nini?sioni maana yake kabisa, ma vitambulisho ya kutengenezesha hapo mjini kibao, mnamashine yoyote ya ku scan hivyo vitambulisho kujua kipi ni halali kipi ni feki?kupotezeana muda tu na kujifanya muonekane mnafanya kazi, mwakyembe hebu dili nao hao, sisi zamani tulikua tunapanda treni bila masharti natulikua tunaenjoy safari ya kigoma. jipangeni upya,mmechemsha kwa hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...