Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Bwana Raymond Chambers mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika vita dhidi ya Malaria wakati wa kikao maalum cha African Leaders Malaria Alliance(ALMA) kilichofanyika jijini Addis Ababa leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati wa kikao maalum kilicojadili masuala ya Maziwa Makuu kilichofanyika jana jijini Addis Ababa Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Rais mpya wa Misri Bwana Mohamed Mursi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais mpya wa Misri Bwana Mohamed Mursi wakati wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU) uliofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akifanya mazungumzo na Rais mpya wa Misri Bwana Mohamed Mursi (wa pili kushoto) pamoja na viongozi waandamizi wa Misri wakati wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU) uliofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Rais wa Malawi Bwana Khumbo Kachali jijini Addis Ababa Ethiopia wakati wa mkutano wa 19 wa Wakuu wan chi za Umoja wa Afrika leo.(picha na Freddy Maro).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2012

    Picha ya juu kabisa inakuwaje pale, wanatunishiana misuli / wanapigana mikwala ama?!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2012

    Michu mbona hupendi ku you tube speech za Mkuu wetu.Tafadhari jitahidi kwa hilo angalau watu wawe wanapata jumbe zake mbalimbali nadhani zinasaidia sana si tu kusubiri mwisho wa mwezi.mbona kagame zinatoka kila dakika angalia kama ya hii summit ya family planning kagame wameshamyoutube

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2012

    Bwana Khombo Kachali Makamu wa Raisi wa Malawi kazi anayo!,,,chini ya Raisi Mwanamke Joyce Banda mamaa wa jazba.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2012

    Banda hana jazba.Ana uwezo wa kufanya maamuzi ambayo wanaume wenu wameshindwa kuyafanya. Big up mamaaa Banda!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...