Ilikuwa ni mpira wa krosi iliyopigwa na Mchezaji wa Yanga,Juma Abdul kuelekea langoni mwa timu ya Mafunzo na ndipo Mchezaji wa Timu ya hiyo ya Mafunzo kutoka Zanzibar,Juma Mmanga (13) aliruka juu Sambamba na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Hamis Kiiza na kugongana kwa bahati mbaya wakiwa katika harakati hiyo ya kuwania mpira wa juu,hali iliyopelekea Mchezaji huyo wa Mafunzo ya Zanzibar,Juma Mmanga kupoteza fahamu na kufanya mchezo huo kusimama kwa muda.Mchezo huo uliendelea baadae na kumalizika kwa hatua ya Penati ambao timu ya Yanga iliweza kuibuka mshindi baada ya kushinda mabao 5-4.
 Wachezaji wa Timu zote mbili za Mafunzo na Yanga wakisaidiana kumpepea Mchezaji Juma Mmanga wa Mafinzo baada ya kupoteza Fahamu kutoka na kugongana kwa bahati mbaya na mchezaji mwenzie wa Yanga,Hamis Kiiza.
 Wachezaji wa Timu ya Mafunzo wakiwa wamechanganyikiwa baada ya mwenzao kupoteza fahamu wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame dhidi ya Timu ya Yanga uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Wafanyakazi wa Chama cha Msalaba Mwekundu wakimtoa mchezaji huyo uwanjani chini ya Uangalizi wa Madaktari wa Timu zote mbili kwa ajili ya kumpatia huduma ya kwanza.
 Wafanyakazi wa Chama cha Msalaba Mwekundu wakimpeleka katika chumba ya huduma ya kwanza Mchezaji wa timu ya Mafunzo,Juma Mmanga baada ya kupoteza fahamu.
 Baadae alizinduka lakini hali yake haikuwa nzuri hivyo,ililazimika mchezaji huyo apelekwe hospitali kwa matibabu zaidi.
Mchezaji Juma Mmanga akiagana na Mmoja wa wachezaji wenzake aliekuwa nae wakati akiingizwa kwenye gari la Wagonjwa Mahututi tayari kwa safari ya hospitalini.
Penati ya mwisho ya timu ya Yanga iliyopigwa na Athuman Iddy ndiyo iliyowatoa Mafunzo katika Mashindano ya Cecafa Kagame Cup jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2012

    RAMADHANI hii ilikuwa michezo isitishwe na waislam wafunge tu sio kucheza mpira

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2012

    Wadau nielewesheni endapo nimepotoka. Nilisoma sehemu kuwa mtu akiwa katika hali ya kutojitambua anapaswa kuegemezwa upande wake wa kushoto kwa vile mirija ya hewa hufunguka zaidi katika upande huo na si kumlaza chali au kumuegeshea upande mwingine wowote.

    Ninachokiona hapa na tofauti na kinafanywa na wataalam wenyewe. Bora mnifumbue macho mapema nisije nikafanya kosa endapo nitapaswa kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyekumbwa na janga kama hili.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2012

    Wewe anon wa kwanza hapo juu. Kwa mawazo yako kwamba kila kitu kinasimama wakati wa mfungo? Nadhani mawazo yako ni potofu....watu waendelee kuchapa kazi kama hawawezi basi waache. Na hiyo timu yenu mbona imeshiriki wakati wa mfungo? Mbaki huko kwenu Zenjibar.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2012

    Yanga ina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa ,ingawa kiwango siyo cha kutisha ,ila ikumbukwe kocha Tom hajakaa na timu muda mrefu.
    N.B Ama kweli Zanzibar pia kuna vipaji sana tu ,hivyo kocha wa taifa stars asiishie tu bara ,pia ajaribu kuchukua wachezaji zaidi au kuangalia vipaji huko Sansibar pia kwa manufaa ya taifa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2012

    Tanzania kwa ujumla hakuna vipaji vya michezo wala nini ndugu yangu. Hakuna lolote tunalofanikiwa katika anga za kimataifa. Na timu zinazofanikiwa, japo kwa kidogo sana, ndani yake kuna wachezaji wa kigeni.Mimi napingana kwa nguvu kabisa na wanaosema Tanzania kuna vipaji vya michezo, hasa soka. Vingekuwepo wala tusingengoja watu watamke, tungeyaona wenyewe. Ila nothing, zilch, period!

    Leo hii kwa mfano Simba hawana Patrick Mafisango (R.I.P) na Emanue Okwi (wote wachezaji wa ng'ambo) tayari madudu uwanjani, hadi kocha anakiri kutokuwepo kwao ndio sababu. Sasa wamebaki wangapi humo wazawa lakini watu wawili tu kutokuwepo ghafla basi tayari ni ishu?

    Wote hao Yanga, Simba na timu zingine wanacheza mpira usio na kiwango cha umri na umaarufu wao. Wakija ndugu zetu kutoka nchi ambazo zimekumbwa na vita kwa muda mrefu wanatota kama panzi aliyefungwa fungwa masharubu na miguu. Hakuna lolote, hakuna vipaji wala nini. Ni sawa na mwanafunzi ambaye hata akipewa majibu ya mitihani bado kuna uwezekano mkubwa akafeli. Taifa stars (sijui hata kwa nini wanajiita hivyo) si unawaona, au huwa unawasikia tu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2012

    anon wa tue 24 01:35 am maoni yako yanakutambulisha kwamba wewe ni shabiki wa michezo (mwanasiasa wa michezo) na si mwanamichezo kabisa. Kama hapa wanaotoa maoni ni wanasiasa wa michezo basi uko sahihi lakini kama hapa wanaotoa maoni ni wanamichezo basi tafuta njia ufute maoni yako, yanatapisha aaakhhh!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2012

    hakuna kulazwa ubavu ni sahihi kabisa kuwa chali kwakuwa atakapolala chali ndio airways zinaclear na anapoanguka mtu awachwe hivi hiv hadi watu wa hudumaya kwanza wafike.Ama kuhusu TAIFA STAR ni kweli ZNZ kuna vipaji lakini ni mambo ya upambe watu wanaupambe kwakocha na wanamchagulia kablahata hajachagua mwenyewe sifkiri kama kila siku Nizar halfani ni mchezaji mzuri kilakocha amchague MFANO TU.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2012

    @ Mdau Mon Jul 23, 10.20 PM 2012.

    Ni kweli kabisa, mtu akizimia na kama bado anapumua inabidi awekwe kwenye "left lateral position" aka recovery position, sababu kubwa ni mbili.
    1, Mtu akizimia mara kwa mara anaweza kutapika pia, hivyo akiwa amelala chali, matapishi yanaweza kuingia kwenye mfumo wa hewa na kufanya ashindwe kupumua,ie he/she can be choked.

    2, Mshipa mkuu a damu wa vena kava (inferior vena cava), unaweza kuminywa na kusababisha damu chache kurudi kwenye Moyo, kama mtu aliyezimia atalazwa upande wa kulia(Zuia hili kwa kumlaza upande wa kushoto).

    kama mtu amezimia na hapumui, hivyo anza CPR, look, listen and feel, do thirty chest compressions followed by two mouth to mouth breaths.
    Kama hutaki kumpa mgonjwa the so called "kiss of life", basi haidhuru fanya hizo 30 chest compressions, mpaka apate nafuu, au Daktari akifika.
    Dr Gangwe Bitozi- Ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...