Ndugu Michuzi, heshima yako.

Ninaomba msaada unirushie mtandaoni kwako ombi hili kwa wadau wanaofanya au waliowahi kufanya masomo ya masters mchepuo wa biashara (MBA Genaral, Master of Finance,Accounting, Human Resourses, Management n.k) kwenye vyuo hasa vya USA, Canada, Australia, New Zealand na kwingineko. 

Admission ya vyuo hivi inahitaji pamoja na mambo mengine kufaulu mtihani wa GMAT. Nimekuwa na nia ya kufanya mtihani huu lakini nimekutana na changamoto kadhaa kama kutoeleweka kwa vituo vya kufanyia au kuwaandaa watahiniwa wa kufanya mtihani huu hapa bongo, kutopatikana kwa materials kwa ajili ya maandalizi, ugumu wa namna ya kujisajili na kulipia kupitia mtandao n.k. 

Ninahitaji kupata uzoefu wa watu waliowahi kufanya mtihani huu hapa TZ, walikabiliana vipi na changamoto hizi? Kwa mfano mimi niko Mbeya, ni lazima nije kufanyia Dar, ni kweli kama nilivyoona kwenye mtandao kwamba Tanzania nzima ni chuo kimoja tu kinausimamia?

 Nimeomba materials chuo hiki wanasema hawafundishi wala hawatoi materials, mpaka ununue kupitia mtandao kwa credit card...Gharama za mtihani nimeona kwenye web yao ni $ 250 lakini hiki chuo kimoja kinatoza zaidi ya hapo, kuna namna naweza kujisajili bila kupitia jamaa hawa na nikishajisajili nitafanyia wapi? 

Naomba msaada tafadhali.

Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2012

    Ni kweli sehemu ya kufanyia ni moja. ila hakuna longo longo hapa huwezi kukwepa fee ya mtihani.

    Inabidi uende kwenye mtandao wao ulipe hiyo $250 register kufanya UD.

    Kama unataka materials; ongea na rafiki yako aliye USA atakutafutia vitabu na CD easily arafu akutumie. Hela kadhaa itahitajika

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2012

    hello, kuna chuo kipo uk , ila wanaofisi bongo sio agency ni ofisi ya chuo (market office) wasiliana na huyu mtu anaitwa ally abdallah, email yake ni ally.abdallah@lsclondon.co.uk

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2012

    The Institute for Information Technology (IIT) is the only centre in Tanzania that offers GMAT exams. However, they are only a testing centre and so they do not offer any study material or tuitions related to GMAT. GMAT registration can be done online by logging in to http://www.mba.com/ . The cost of registering GMAT online is $250. Another option is that of registering with the centre whereby the candidate will be required to go to the center and fill in the required form and make payment of $300. Exams can be scheduled any day from Monday to Friday, starting from 9am to 5pm. Contact address: Institute for Information Technology, 1st Floor, Kelvin House, Samora Avenue, and P.O. Box 964, Dar es Salaam. Tel: +255 22 2114801/2, Fax: +255 22 2119506 Website: http://www.iit-tz.com/, Contact Person is Shezmin Kassam, Program Manager.
    Preparation materials for all the standardized tests are available at the U.S. Embassy Dar es Salaam’s Information and Resource Center Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2012

    mdau nimekuwekea information kwenye comment ya kwanza kwa maelezo zaidi piga simu uongee na Shezmin Kassam ndie program manager simu yake iko hapo kwenye maelezo wameeleza waweza kwenda kuregister pale kwa $300 ukapewa na tarehe ya exam bado naangalie material utayapata vipi. hope imekusaidia

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2012

    Going to an American College this Year?


    Image: Education USA
    This center belongs to the EducationUSA network of educational advising centers affiliated with the U.S. Department of State's Bureau of Educational and Cultural Affairs. EducationUSA advisers strive to provide accurate, comprehensive, current, and unbiased information on educational opportunities in the United States. We do not endorse or rank any college or university, nor do we endorse services provided by any company or organization in areas of test preparation, admissions, placement, language training, or visa procurement.

    Educational Advising Assistance for Tanzania Students Wishing to Study in the USA

    Answers to Frequently asked questions

    Useful tips to Teachers on Writing Letter of Recommendation

    Services Available

    Undergraduate group sessions, which provide an introduction to the structure of American higher education as well as information on the application process. These sessions are offered each Wednesday, at 2:00. All undergraduate applicants must attend a group session before seeing the advisor individually. Undergraduate and graduate applicants should review admission procedures on the computers in the library. The librarian on duty will assist you.

    Individual advising sessions, which help students to implement their educational plans; are available by appointment on Monday and Wednesday afternoon from 2:00 p.m. to 4:00 p.m.

    Information on a variety standardized tests (e.g., TOEFL, SAT, GRE, GMAT) is available to students who have attended introductory advising sessions and selected their schools

    We offer a well equipped library of up-to-date materials on education in the U.S. You are welcome to use these materials for researching and planning your U.S. education Monday -Thursday from 9:00 a.m. to 5:00 p.m. and Friday from 9:00 - 11:00 a.m.

    You may also wish to consult these sites for additional information about higher education in the United States

    College Board Online (http://www.collegeboard.com/)
    Educational Testing Service Online (http://www.ets.org/)
    University and College (http://www.utexas.edu/world/univ)
    Our primary website is http://www.educationusa.state.gov/, where you will find a wealth of information designed for international students.

    Print
    Email
    PRE-DEPARTURE ANNOUNCEMENT
    Pre-Depature Orientation - Study in the U.S. June 21, 2012 at 12:00 noon (PDF 59 KB)
    Download Adobe Reader »
    CONTACT INFORMATION
    Office Hours
    Individual sessions
    (by appointment):
    Mon. & Wed. 2:00 - 4:00 p.m.

    Address
    Educational Advisor
    American Embassy
    PO Box 9123
    Dar es Salaam
    Tanzania
    Tel: (255-22)229-4192
    Fax: (255-22)229-4722
    Email: eadar@state.gov

    This site is managed by the U.S. Department of State. External links to other Inte

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 13, 2012

    mdau material kwa nilivyoelewa unazipata kwenye hiyo center niliyocopy paste iko ubalozini na simu zao ziko hapo wapigie simu kwa maelezo zaidi au kama utakuja Dar nakushauri uende mwenyewe ukaulize zaidi, nimejaribu kusaidia mengine utamalizia mwenyewe. kumbuka hii imefocus zaidi Marekani sijaangalia nchi zingine ulizotaja. Good luck

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 13, 2012

    Ok haya information unaweza kupata hapa chini kwenye link hii

    http://tanzania.usembassy.gov/test-centers-info.html

    na ndio inabidi utumie credit card, visa and the like!!!

    Mdau

    John

    ReplyDelete
  8. Bahati mbaya mdau ajasema yupo wapi hivyo inawezeakana ikampa shida konda kujua ampe msaada tuta la wapi.

    Ila ukifungua official website ya GMAT ambayo ni www.mba.com kuna sehemu ya kutafuta test location ambayo itafufahamisha kituo kilicho karibu yako. kwa Dar uwa test kama hizi zinafanyikia University of Dar Commputing center ila malipo unalipa moja kwa moja.
    Bahati nzuri sikuhizi hata Bongo yuna Debit Card (Visa au mastercard) hivyo hata kama uko hapa nyumbani waweza kulipia kupitia online.

    Uki google GMAT utapata free GMAT practice test na ukishalipia jamaa uwa wanatuma practice materials. Inabidi ucheck na chuo unachotaka uone wanataka score ngapi ila ni vizuri kupata za juu otherwise unaweza kurudia zaidi ya mara moja na kila mara lazima ulipe

    Natumaini tuta ili laweza kusaidia

    Styden

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 13, 2012

    Nenda UCC-UDSM wanafanyisha TOEFL na GRE, sina hakika na GMAT, ila nadhani wanaweza kukushauri. Kila la kheri.

    Eddy
    Van.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 13, 2012

    Mdau wa Masters,

    Lipo tatizo la Vituo vya hizo College Testings hapa Bongo ila pana Centre moja ya mtu ambaye yeye ni Appointed College testings administrator yupo hapa Dar.

    Ukiwa Dar fika jengo la Bakwata ipo THE ICON CENTRE, 2nd Floor ni ya Mrs. Kapasi ipo makutano ya Bibi Titi na Morogoro Road.

    Yeye anatoa Preparatory Classes na hata materials anatoa na ana simamia Testings kama GRE, GMAT, TSE, MELAB,SAT-I,SAT-II, IELTS, Toefl and so on.

    Kazi kwako!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 13, 2012

    IT IS NOT TRUE THAT ARE NOT GETTING PLACE TO DO A EXAMINATIONS BECAUSE YOU WAS SAID IT HAS ONE PLACE IN DAR TO DO IT.HOWEVER YOU WAS SAID IT IS ONLY $250 THEREFORE IT LOOK LIKES YOU KNEW IT ALREADY AND YOU WAS ALREDAY TO DO IT EXAMINATION. I LIVED IN COLUMBUS OHIO AND I JUST GRADUATED IN MY MASTERS OF SCIENCE ON FINANCE AND MINORS ON INTERNATION RELATIONSHIPS MY GMAT WERE VERY EASY 150 QUESTIONS ALL MALTIPLE CHOICES AND TRUE AND FALSE. VERY FEW MATCHINGS ITEMS AND FEEL THE BRANKS. YOU CAN PASS YOU JUST HAD TO STUDY VERY VERY HARD AND THERE EXAMINATIONS IS VERY TOUGH IF YOU WERE NOT STUDY ALL TOPICS IN AND OUT. I URGUE YOU TO CONTINUED TO PUSH THEM TO TAKE $250 FEES AND DO EXAMS. MY NANE IS KARUME JAMALIWA FROM COLUMBAS OHIO LET ME KNOWS IF THIS HAVE HELP YOU IN YOUR ENDOVOURS OF SERCHING SCHOOL IN UNITED STATES, IT IS VERY SIMPLE AND NO CONSUMER TIME IS WESTED.
    KARUME JAMALIWA. COLUMBAS OHIO

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 13, 2012

    Mi nachojua british council wanatoa kwa gharama ya sh 350,000 kama nimekosea ni kidogo sana; na ukishalipa unapewa materials yote; google british council Tanzania then wapigie wakupe maelezo zaid

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 13, 2012

    Ukienda katika book store iliyopo Mlimani City wanavyovitabu kwa ajili ya mtihani huo bahati mbaya sikumbuki jina la hiyo bookstore ila hapo utafanikiwa kupata vitabu kwa ajili ya mitihani hiyo. Aidha, kuhusu sehemu ya kufanya mtihani wa GMAT ni Institute of Information Technology, Dar es Salaam jaribu goggle ili uweze kupata contacts zao.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 13, 2012

    mbona umebania comment? michu vipi hutaki maendeleo ya watu sio vizuri kaka mdau nimetuma maelekezo yote ya GMAT test comment zote zimebanwa sielewi lengo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...