Waziri wa miundombinu na mawasiliano (Zanzibar) Mhe. Hamad Masoud Hamad (CUF) -pichani-  amejiuzulu kufuatia ajali ya boti ya Mv Skagit. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, ameridhia kujiuzulu kwa Waziri huyo na amemteua Mhe. Rashid Seif Suleiman (Ziwani, CUF) kushika nafasi hiyo. 

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Iddi amesema uamuzi wa kujiuzulu kwa Mhe Hamad ni wake binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2012

    Hongera zako,lakini na Registrar wa meli Zanzibar na Bara wote wajiuzulu.

    Walijua specific conditions za meli ile kwamba hairuhusiwi kutembea kwenye open sea lakini wakairegister na kuiruhusu ichukue abiria.

    Uzembe wa aina hii ni mbaya sana wa kusababisha maisha ya watu kupotea bure.

    Mwenyezi Mungu awalaze pema peponi wote waliopoteza roho zao. Amiiin

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2012

    The biggest problem here is the logic to rescue people, we don't have that in place, the rescue team should not take longer than 20mins to arrive at the accident scene. Also with working equipment, sometimes our rescue team shows up without rescuing equipment s. That is what is needed in place, the 100 People died shouldn't have died.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2012

    Hongera sana umeonesha mfano wa kuigwa. Umeipaisha Zanzibar kwenye medani za utawala bora na uwajibikaji. Ingekuwa ni waziri kutoka bara asingekubali kujiuzulu. Angejitetea weeeee wakati ni kweli anahusika. Safi sana, BIG UP Seif.

    Sasa kaungane na wenzako tukadai Zanzibar yetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2012

    kajiuzuru lakin atatiwa kwenye serikalini kificho ficho ndo inavyokuwa usisikiye aisee so msifurahiye sana kujiuzuru kwake kumbukeni kwamba alikuwa hataki kujiuzuru

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2012

    nawashangaa mnaomsifia kujiuzulu, huyu si alikuwa anagoma kujiuzulu? alitakiwa ajiuzulu toka ajali ya kwanza naona kalazimishwa kujiuzulu aka kaonyeshwa mlango kidiplomasia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2012

    Mimi bado nawalaumu Mamlaka ya hali ya hewa kwa sababu hali ya hewa ilibadilika kulikuwa na upepo mkali hadi nchi kavu. Wao ndio walipaswa kutoa tahadhari mapema lkn hawakufanya hivyo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2012

    You are absolutely correct the 5th commenter, I hat off for you!! The Hon Minister was supposed to have stepped down long ago unconditionally immediately after the MV Spice Islanders' tragedy. Now I witness from ZBC Television, the members of Zanzibar House of Representatives congratulating him for what they claim to be 'clean responsibility'!! What a nonsense thought!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2012

    APELEKWE MAHAKAMANI KWA KUUA ABIRIA WASIO NA HATIA

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2012

    mnaona choyo kwa kuwa ni mzanzibari Hii nchi ina mawaziri wawili husika lakini cha kushangaza hii meli imetoka bara na imepakia watu zaidi ya hao 230 na wamekiri wenye meli kuna watu wamepitishwa kificho ficho HIVI PALE DOKI kuna wazanzibari wa TRA NA POLISI walioruhusu hiliii?

    hao mawaziri wanakuwa tu mawazirilakini hawajawahi kutembelea hata bandarini ? na hakuna miundo mbinu ya kujikinga na majanga wala utaalam wa hali ya hewa-POLISI TRA WAMILIKIWA MELI WOTE WAMO HATIANI PAMOJA NA WAZIRI WA MUUNGANO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...