Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma  hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika  kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi ya tarehe 23 Juni 2012.

Baada ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:
(i)                   Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;
(ii)                  Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.
(iii)                Madaktari waliopo likizo  warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa. 
(iv)                Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;
(v)                 Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations’ za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na
(vi)                Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo

Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na  waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.  

_________________
Dkt. Gabriel Upunda
KAIMU MWENYEKITI
BODI YA WADHAMINI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2012

    Huko tunakokwenda siyo kuzuri.
    sasa ni kawaida tu kwa maprofesa ,walimu na madr. kukimbilia kwenye siasa.
    Serikali inapaswa kuwasikiliza hawa watu na sio kutumia mabavu,ubabena na vitisho.
    Nchi hii ina haribika sasa .
    Madaktari ,walimu na wanavyuo ni viungo nyeti ktk kujenga taifa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2012

    We always use the same approach! It doesn't matter what level of the leadership the person is!

    Let as be creative and tolerance in solving our national problems and our misunderstanding!

    God bless us!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2012

    A Doctor to strike is a death sentence to a patient!. As a nurse, before I strike I think about "if it was myself,my mother,Sister,brother,child,husband and the list goes on would I have loved me or them to lay in the hospital without service?" Hospital personnel especially who provide direct patient care please think twice before you strike!! You took an Oath!! I am underpaid for the services I do but I took an Oath! PROBLEM SOLVING is the answer " ROOT CAUSE ANALYSIS"
    Concerned Nurse!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2012

    Albert Einsten liapata kusema ''Maana ya upumbavu ni kurudia kufanya jambo lile lile kwa kutumia mbinu ile ile na kutarajia matokeo tofauti''.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2012

    HIVI NYIE BODI MNUJUA SHERIA ZA AJIRA ?
    UNAWAOMBA AU WAO NDIO WAMEMBA KAZI
    CHUKUA HATUA ZA KISHERIA SIO KUOMBANA HAWA WANALIPWA NA ATAKAE RUDI AKATWE SIKU ALIZOGOMA NA KAMA ATALIPWA SIKU ZOTE WANANCHI TUTAIISHTAKI BODI, KWA KUWALIPA WATU BILA KUFANYA KAZI

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 02, 2012

    Mi nilijua Udaktari ni Wito, Kumbe Commercial daa..Wajitolee wamalizie hii ungwe ya JK..People have opened their eyes now, Tukiwachagua tena wanaoleta haya yote Tutakuwa tumelogwa na Tusilalamike bali Tufuate sytem tu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2012

    Matokeo ya Maprofesa,Wahandisi na Madakitari kushiriki Siasa ndio haya sasa!

    Mara zote Sayansi ianegemea kwenye uhalisia na ukweli wakati Siasa inaelemea kwenye kufikia malengo hata kama kwa njia ya udanganyifu na kupindisha ukweli halisi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...