Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania maarufu kama Bongo Movie linalodhaminiwa na Kinywaji cha Grand Malt,Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini,Mh. Halima Dendego (katikati) akijiandaa kubonyeza kitufe chenye kuashiria uzinduzi Rasmi wa Tamasha hilo kwenye Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania maarufu kama Bongo Movie,Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini,Mh. Halima Dendego akiwahutubia wapenzi wa Bongo Movie waliofurika kwa Wingi kwenye Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga kushuhudia Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie).Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah na kulia ni Meneja wa Kinywaji hicho cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo,Consolata Adam.
Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Habari kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Godfrey Mngereza akizungumza machache kwenye Uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Butallah akizungumza machache na wapenzi wa Bongo Movie waliokuja kwa wingi kwenye uzinduzi wa Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) katika Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Mh. Halima Dendego na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,Mh. Mboni Mgaza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...