Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari zikiihusisha Idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi. Kati ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Gazeti moja la kila wiki limekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa madai kwamba ni habari za uchunguzi na kuihusisha Idara.
Idara inataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni za UZUSHI NA UONGO ambazo zina nia ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha vipande vya taarifa mbalimbali ili kukidhi malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumia gazeti hilo. Idara haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katika tuhuma hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.
Matukio yaliyotajwa katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho ndicho Chombo Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia upotoshaji huo uendelee.
Aidha, tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Idara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azma yetu ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana na wanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,
Makao Makuu,
DAR ES SALAAM
26 Julai, 2012.


Safi sana, msikatishwe tamaa na wasio na nia njema. Wala hawana shukrani kwa utulivu, amani na uhuru wanavyo chezea. Kaza buti songa mbele. Hongereni.
ReplyDeletehivi bongo kuna sheria gani, idara ya taifa inashindwa kuwapeleka mahakamani gazeti kama inaona inaandika uongo badala yake inawaamia wananchi wapuuzie habari????????
ReplyDeleteGazeti la mwanahalisi ni mojawapo limejaa propaganda na umbea mtupu. Inawezekana ndiyo maana Mhariri/mmiliki wake aliwahi kumwagiwa tindi kali kwa kujifanya anajua kufanya uchunguzi kumbe anapenda tuu kuunganisha uongo wenye mtazamo wa kusadikika ili auze Gazeti lake. MBAYA SANA. Toa hii Michuzi usimlinde kwa kuwa NI MWANDISHI MWENZENU.ISIPOTOKA HII COMENT NITAJUA UMEMLINDA MTU MUOVU
ReplyDeleteIdara ya Usalama ingekuwa ina nia mbaya ya kuwashughulikia hao viongozi wa CHADEMA wala wasingepata nafasi ya kueleza waliokwisha yaeleza. Waache siasa chafu hizo za kuupakazia Usalama wa Taifa ambao ndiyo unaifanya nchi yetu kuwa ya amani mpaka hii leo. Msitake kuwakatisha tamaa watu wanofanya kazi usiku na mchana kulinda usalama wetu.
ReplyDeleteKupeleka kesi mahakamani kuna gharama zake. Ikiwa kila mpuuzi utaamua kumpeleka mahakamani unaweza kujikuta bajeti yote inaishia mahakamani na maadui wanaotaka kukudhoofisha wanaweza kuibua tu uzushi mara kwa mara ili kuexhaust bajeti na mipango.
ReplyDeleteWananchi hawawaelewi watanzania wenzetu wa usalama wa taifa kwa tuhuma hizo na kama mnaona yaliyoandikwa siyo sahihi mpeleke mwandishi wa habari hizo au gazeti linalohusika mahakamani ili ukweli ukajulikane huko huko. Ndicho wanachosubiri wananchi wajue mkweli ni nani.Kutoa tu ufafanuzi bado mtabaki kuwa na mawaa.
ReplyDeleteMdau wa Fri Jul 27, 12:05:00 AM 2012 nakuunga mkono,ili kukomesha vyombo vya habari vinavyoandika uongo inabidi wasilumbane,waende mahakamani na ikithibitika kwamba habari ni za uongo vyombo hivyo vifungiwe maisha ili visiendelee kupotosha umma
ReplyDeleteIdara ya Usalama wa Taifa,
ReplyDeleteHeko kwa kazi kubwa na jukumu mnalolitekeleza kwa maslahi ya nchi na Raia.
Isipikuwa kazi kubwa iliyopo mbele yenu ni KULIFYEKA GENGE LA WATU WANAOHATARISHA USTAWI WA NCHI YETU LINALOSHIRIKISHA WATU KAMA:
1.MAFISADI,
2.WALA RUSHWA PAPA,
3.WAHUJUMU,
4.WACHOCHEZI (kama hao watoa taarifa za upotoshaji kwa umma)
Haiwezekani,
Hivi kuna sababu watu wasiozidi 1 Milioni (hao hapo No.1 hadi No.4 juu) wakasumbua Ustawi wa Nchi na mustakabali wa maisha ya watu 45 Milioni?
Habari! Inasikitisha kama watanzania wa leo wanaelezwa maneno ya JUMLA*2 (ni imani yangu ENZI HIZI tunaweza kusoma habari between lines (tumeelimika mno),miaka ya enzi za ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CHAMA ZIMEPITA, KWA SASA kuna MAENDELEO YA TECHNOHAMA YA JUU SANA, nadhani hata Mkongo wa TAIFA, setelaiti vizadhidi KUIIMALISHA habari.
ReplyDeleteIdara ya usalama wa taifa hawana haja ya kuwapeleka hao watu mahakamani, wana njia zao za taratibu lakini za uhakika za kuwamaliza. Tuombe uhai tuu. Usifanye mchezo na hawa jamaa na haswa ukizingatia kua kidunia wako kwenye top 10... Salute.
ReplyDeleteMichuzi nachukia sana hii blog yako kwa sababu tukiandika vitu vyeney kukosoa unabana. Wewe unataka watu wasifie tu wakati taifa linateketea. Toa comments zote. Don't be biased. Kama una ndugu zako huko usalama wa taifa utuambie ili tujue blog yako ni kwa ajili ya watu hao.
ReplyDeleteendeleeni kufanya kazi yenu tena zaidi, msamini kabisa petty talk to to fullfell petty needs. Jamani its interlligence kama wange panga siamini kama wasinge timiza.
ReplyDeleteYAAANI WANGESHINDWA KUFICHA no way ...just do your part