Hali ya USAFIRI kati ya Nangurukuru- Lindi  katika kipande cha km 165 imekuwa ni safari ndefu inayochukua takriban masaa 4 baada ya kampuni ya CICO kuweka njia ya mchepuo kwa km nyingi kupisha matengenezo ya marudio kufuatia 
matengenezo yake ya awali kwa kiwango cha lami kukataliwa na kulazimishwa arudie. Hivyo hali ya  kupishana huwa tete na Wengi huomba dua mvua isinyeshe maana hali itakuwa mbaya zaidi. Wakala wa Barabara inaombwa na watumiaji wa barabara hiyo kusimamia mkandarasi huyo kupunguza urefu wa mchepuo kwa kuwa hajauimarisha kwa ubora njia hiyo ya muda kati ya 
Lingaula na Mavuji..Picha na Abdulaziz Video, Lindi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2012

    CICO:

    1.Hoja ya msingi ni kupanua hiyo michepuo ili kutoa nafasi ya upana wa barabara.

    2.Mpaka lini Kandarasi zitakuwa zinafanya madudu miradi ya barabara za lami nchini na kulazikima kushinikizwa kurudia ujenzi?

    Sioni sababu kwa nini hizi tenda zisiwekwe kupita ICB (International Competitive Bidding)?

    Ama kushirikisha taasisi kama WORLD BANK na TRADE MARK INTERNATIONAL katika kusimamia kuchagua Wazabuni Makandarasi wenye sifa na kuweza kumudu kufuata taratibu kanuni na vigezo vya ubora wa kazi zao?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2012

    Jamhuri ya walalamishi. Saa nne kwa km 165 si muda mkubwa sana kwa vile ni shughuli ya muda ili njia itengenezwe mwende kwa saa mbili. mvumilivu hula mbivu. Wakumbukwe na wakulima ktk swala la pembejeo na elimu kwani naona mmkalia barabara za lami tu kama vile huo ndio utii wa mgongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...