Wachezaji wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea London, Uingereza katika michezo ya Olimpiki.
Wachezaji wa timu ya Tanzania inayokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuondoka majira ya saa kumi jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda London, Uingereza.
Muogeleaji wa mita 100 wa Tanzania Magdalena Moshi akiwa na kaka yake (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuelekea London, Uingereza katika michezo ya Olimpiki.
Kocha wa Riadhaa, Zakaria Ngwandu muda mfupoi kabla ya kuondoka
Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Leonard Thadeo, akiwaasa wachezaji kujituma katika michezo hiyo huku akisisitza kuwa na nidhamu kwa muda wote wa kambi na mashindano
Picha/Habari na Francis Dande,DAR ES SALAAM- Tanzania
TIMU ya Tanzania inayokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki imeondoka leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda London, Uingereza, huku ikiwa na matumaini ya kurudi na medali.
Timu hiyo ya Tanzania yenye wanamichezo sita ambao ni wa Kuogelea, Ngumi za Riadhaa na Riadha imeondoka jana majira ya jioni kushiriki michuano hiyo inayoanza Julai 27 hadi Agosti 12 mwaka huu, yakishirikisha nchi 205.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kupanda ndege, mmoja wa wachezaji hao, bondia wa ngumi za ridhaa, Seleman Kidunda, amejinasibu kufanya maandalizi ya kutosha kumuwezesha kurudi na medali, ingawa pia aliomba dua za Watanzania.
“Naenda kulipigania taifa kuhamasisha mabondia ambao wanadhani kuwa Tanzania haiwezi. Lengo ni kuitangaza nchi na Afrika, hasa ukizingatia kuwa haya ni mashindano makubwa duniani. Muhimu kwa Watanzania kutuombea dua,” alisema Kidunda.
Kwa upande wake, Kocha wa ngumi, Mrakibu wa Magereza, (SP), Remmy Ngabo, alisema amempa Kidunda mazoezi ya kutosha na anaamini yatamsaidia kwenye mashindano hayo yanayoanza kuanza
Mwanariadha wa Marathon, Zakia Mrisho alisema kwa upande wake anaenda London kwa nia moja tu ya kurudi na ushindi na kwamba hakutakuwa na kisingizo cha maandalizi, kwania amefanya ya kutosha kumpa medali.
Aidha akizungumza wakati wa kuiaga timu hiyo, Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Leonard Thadeo, amewaasa wachezaji hao kujituma katika michezo hiyo huku akisisitza kuwa na nidhamu kwa muda wote wa kambi na wa mashindano.
Aliongeza kuwa, mashindano hayo yatakuwa na ushindani mkubwa, hivyo wanapaswa kujituma zaidi ili waweze kurejea na medali.
Wanamichezo waliondoka jana ni Zakia Mrisho, ambaye ni mwanariadha anayekimbia mita 5000, Selemani Kidunda ngumi za Ridhaa, Samson Ramadhan, Riadha, Msenduki
Mohmed na Faustine Mussa ambaye anakimbia marathon.
Aliongeza kuwa, mashindano hayo yatakuwa na ushindani mkubwa, hivyo wanapaswa kujituma zaidi ili waweze kurejea na medali.
Wanamichezo waliondoka jana ni Zakia Mrisho, ambaye ni mwanariadha anayekimbia mita 5000, Selemani Kidunda ngumi za Ridhaa, Samson Ramadhan, Riadha, Msenduki
Mohmed na Faustine Mussa ambaye anakimbia marathon.
Hakuna mwanamichezo hata mmoja hapo hata medali ya shaba hawawaletei,njooni tu mtalii mda ukifika mgeuze zenu
ReplyDeleteTunawatakia kila la heri wachezaji wote!
ReplyDeleteHiyo timu ya riadha ni aibu tuu !!! Hawatapata medali hata moja hapo maana maandalizi yalikuwa finyu.
ReplyDeleteMzee Thadeo unajua kabisa kuwa hapo mnapeleka HEWA, ukwlei unaeleweka kuwa maabadalizi yalikuwa hakuna kabisa, TOC, RT, na wizara hakuna ilichokifanya.
Lakni kwa sababu ni utaratibu acha tuende tuu tukawashangilie wenzetu kutoka Kenya na Ethipoia wapate medali.
Sioni nafasi ya TANZANIA kupata medali huko BRAZIL mwaka 2016 kama shughuli za kuandaa timu na kupigiana DANADANA.
Wakimbiaji wetu wa marathon hawatamaliza, ngoja nikupe mfano;
Mda mzuri wa marathoni (maili 26 yadi 385) mwaka 2012 duniani
ni masaa 2 dakika 4 sekunde 55. Mkimbiaji wetu mwaka huu amekimbia masaa 2 dakika 15 sekende 40. sasa wewe fanya mahesabu uone mwenyewe.
Kwa wanawake kuna Wakenya 3 Ethiopia 3 na Waganda 2 ambao wana mda mkali kuliko mchezaji wetu, kwa hiyo medali ni ndoto za ABUNUWAS tuu.
Wakina Bayi, Nyambui, kocha Gwandu hili wanajua lakini kwenda Olimpiki ni utaratibu wa serikali kwa hiyo TWENDENI tukatembee tuu>
Wasindikizaji wakielekea London !!
ReplyDeleteHaya nendeni mkatembee uko msafishe macho. Safari njema wasindikizaji.
ReplyDeletewasipo rudi na medali basi tusishiriki tena olimpiki mpaka tujivue vya kutosha
ReplyDelete