Cables:            "MUHIMBILI"                                                                       Postal Address:
Telephones:   255-22-2151367-9                                                      P.O. Box 65000          
FAX:                255-22-2150534                                                          DAR ES SALAAM
Web:               www.mnh.or.tz                                                                Tanzania

Taarifa niliyopata kutoka kwenye Kurugenzi ya Tiba, Kurugenzi ya Upasuaji, Kurugenzi ya Tiba Shirikishi na Kurugenzi ya Uuguzi ni kama ifuatavyo;

Kurugenzi ya Tiba:
Huduma zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kati wagonjwa ni wachache wanaokuja kutibiwa.

Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa wote na Registrar wote wamefika kazini na wanafanya kazi. Interns 11 wamefanya kazi. Major ward round zimefanyika. Kliniki zote za leo zimeendelea kufanya kazi  pia cliniki za mchana zitafanyika.

Idara ya watoto, Madaktari Bingwa wote wapo na wanafanya kazi wapo wadini wanaona wagonjwa. Changamoto ni kwamba inabidi pia wafanye kliniki za wagonjwa wa nje na wanajitahidi kufanya hivyo.

Idara ya magonjwa ya nje.
Registrars na Daktari Bingwa wote wapo na wanafanya kazi.

Idara ya magonjwa ya afya ya akili, Madaktari Bingwa wote wamefika kazini . Bada ya wagonjwa wote kupelekwa wodini, walionwa na madaktari. Wagonjwa katika kitengo hiki ni wengi ukilinganisha na idadi ya madaktari bingwa, lakini kliniki zimeendelea kufanyika kwa kiwango cha kati. Kiliniki ya wagonjwa wajidunga imefanyika.

Idara ya magonjwa ya dharura, Registrar wote wamesaini lakini wliofanya kazi ni wawili tu. Daktari Bingwa yupo na anafanya kazi.

Idara ya mazoezi ya viungo, Wafanyakazi wote wapo na wanafanya kazi.

Kurugenzi ya Upasuaji:
Huduma za upasuaji zinafanyika lakini siyo sawa na jinsi zilivyokuwa zinafanyika kabla ya mgomo kwani wagonjwa ni wachache kwenye baadhi ya kliniki na baadhi ya kliniki wagonjwa wanakuwa wengi. Wagonjwa wa upasuaji walioko wodini wanaonwa japo ni wachache ukilinganisha na hali ilivyokuwa. Baadhi ya huduma za upasuaji (operations) zimefanyika ingawa wagonjwa ni wachache kwa vile idadi ya wagonjwa wanaokuja kliniki au waliolazwa kwa ajili ya upasuaji ni wachache.

Huduma za Tiba Shirikishi:
Vipimo vya maabara na vile vya uchunguzi wa radiolojia vinaendelea kufanyika kama kawaida ingawa idadi ya vipimo vimepungua ukilinganisha na kabla ya mgomo. Idara ya famasia pia inafanya kazi kama kawaida. Idadi ya wagonjwa wanaoandikiwa dawa ilipungua ukilinganisha na kabla ya mgomo.

Kurugenzi ya Uuguzi
Huduma za uuguzi zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kawaida.

Imetolewa na;

Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 3, 2012



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2012

    Mungu atawajaalia ubinadamu madaktari wetu. Binadamu ameumbwa na roho ya huruma.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2012

    Ni vizuri ukitufahamisha idadi ya madaktari waliopo na wanaoendelea kugoma ili tuweze kupima huduma zinafanyika kwa kiwango gani ? Haitoshi kusema wagonjwa ni wengi kuliko madaktari bila ya kutaja kitengo kina madaktari wangapi, wangapi wapo na wangapi wanakosekana

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2012

    Ningependa kujua hali ya wagonjwa hawa baada ya wiki moja.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2012

    Wamerudi na sote tunafurahi kwa kuwa watu wetu watapata matibabu. Lakini serikali inatakiwa iangalie upya namna inavyotoa maslahi kwa watumishi wake. Haiingii akilini kusikia eti waziri analipwa milioni 15 kwa mwezi wakati kuna mtu analipwa laki moja na sabini na tano. Kama nchi haina pesa hao wanaolipwa nyingi wanalipwa kutoka mfuko wa nani kama sio kodi za watanzania wote? Haki iko wapi? Huenda mgomo huo ulizidishwa na mambo kama haya.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2012

    Jamani mnatuchanganya, sasa huyo Catherine Mng'ong'o anazungumzia madaktari bingwa gani waliogoma? Mbona hatuelewi, tunaomba maelezo ikiwezekana kwenye vyombo vya habari vya taifa mtutoe hofru wananchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...