Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiwafnya mahojiano na mwanahabari Jena Fox kutoka jarida la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni.Katika mahojiano hayo Balozi Kagasheki alipata fursa ya kuelezea furdsa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini kwa soko la Marekani.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Sued Kagasheki akimkabidhi tuzo ya kinyago Bi. Jena Fox, mwanahabari kutoka Jarida maarufu la nchini Marekani la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni. Tuzo hii ilitolewa na Bodi ya Utalii nchini kufuatia uandishi mzuri wa makala mbalimbali za kutangaza ukanda wa utalii wa kusini katika soko la Marekani.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini Dk. Sloyce Nzuki akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Wageni cha Marekani (USTOA) Bi. Peggy Murphy mara baada ya kufanya nae mazungumzo juu ya namna ya kuongeza idadi ya wageni nchini kutoka Marekani jijini new York hivi karibuni.





WIZARA HUSIKA NA BODI YA UTALII IMEFANYA JITIHADA ZIPI KWANZA ZA KUSAFISHA JINA LA NCHI INAYOJULIKANA KWA RUSHWA, WIZI, TABU YA USAFIRI, MSONGAMANO WA MAGARI MIJINI HASA DAR ES SALAAM KABLA YA KUFUNGA SAFARI KWENDA KUUZA KISICHOUZIKA.
ReplyDeleteUKIINGIA KWENYE MITANDAO KAMA TRIP ADVISOR, KNOW BEFORE YOU TRAVEL, NA WEB NYINGINE ZENYE DETAILS KIBAO KUHUSU UTALII WA TANZANIA, KITU CHA KWANZA WATAKACHOKUONYA NI "UKITAKA JAMBO LOLOTE HATA VISA AIRPORT, LAZIMA UTOE RUSHWA". JE BODI NA WIZARA HUSIKA MNATAKA KUTUELEZA HAMNA TAARIFA HIZO?
SIYO KUPITA KILA KONA KUTEMBEZA BAKULI LA MSAADA HUKU MKIVINJARI KWA FEDHA ZA SERIKALI KWA KILE KINACHOITWA "TANGAZA NCHI KITALII". WENZETU WA KENYA WAPO MBALI KWA HILO NA SASA RWANDA WANAFUATIA. MKIFUTA RUSHWA TU, NDIPO MTAKAPOFANIKIWA. RUSHWA MPAKA KWA MKEO/MUMEO ILI UPATE PENZI. NCHI GANI HII.
HATA WATOTO SIKU HIZI NAO WANATAKA RUSHWA ILI WAENDE SHULE. USIPOWAPA WANAISHIA FERRY KUCHEZA KWENYE MV KIGAMBONI/MAGOGONI.
Mdau hopo juu umenena!
ReplyDeleteMdau wa kwanza mm nahisi ww ni Kenya Kenya..mtakufa na kiroho cha juba..nyinyi kaeni tu kujisifu oo ss matajili huku mwafa na njaa..na kwenye nonino eti tushilikiane mpaka rand subutu kamwe..msituletee hadith za jongoo na nyoka...nyoka alipo mwambia jongoo naomba uniazime macho coz naenda kwenye mnuso wa watu wenye macho ila ntakuludishia...masikini ya mungu jongoo kwa huluma yake amempa basi toka siku ile joka bila ya aibu limeingia minitini...kwa hiyo nyinyi mtajibana kwenye mastore mpaka mwisho wenu...go go tz.
ReplyDeleteMi sidhani kama alichofanya Kagasheki ni kibaya....nampongeza sana kwa nguvu hiyo aliyoanza nayo ila ahakikishe urasimu,rushwa na ufisadi anaondoa katika wizara yake.Naamini utalii pekee unaweza kuwalipia ada wanafunzi wote wa vyuo vikuu,kununua madawa hospitalini na kuboresha shule zetu za msingi na sekondari ila tu kama mtadhibiti hayo niliandika hapo juu.
ReplyDeleteUtalii unatangazwa kwa ziara ya waziri? Kwa nini hatujifunzi nchi kama Malaysia wanavotangaza utalii wao kwa mafanikio? Wanatumia mawaziri? Posho za safari zitatumaliza jamani,mawaziri wetu kaeni ofisini mfanye kazi,wizara zenu hazina vitengo vya masoko vyenye wataalamu?
ReplyDeleteHivi hakuna utamaduni au sanaa nyingine Tanzania? Zawadi ni vinyago tu kila siku? Shame!
ReplyDelete