Kikosa cha Yanga kilichoifunga APR ya Rwanda kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Kagame.
Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa APR.
Kipa wa APR, Ndoli Jean Claude akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake. Kusho ni mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza.
Mfungaji wa bao pekee la Yanga, Hamisi Kiiza, akimtoka beki wa APR, Ngabo Albert katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame, uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga imeshinda 1-0. 
Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi akimtoka beki wa APR.
Mashabiki wa Yanga.
Wanazi wa Yanga wakishangilia ushindi wa timu yao.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuingia fainali ya kombe la Kagame
Kocha wa APR, Ernest Brandy (kushoto) akiwa na kocha wa Yanga, Tom Saintfiet kabla ya mchezo wa nusu fainali ya kagame ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mrisho Ngasa akimtoka beki wa AS Vita
Godfrey Taita akitafuta mbinu za kumtoka beki wa APR, Iranzi Jean Claude
Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet akikumbatiana na baadhi ya viongozi wa Yanga waliokuwa katika benchi la ufundi
Mshambuliaji wa Azam, Kipre Tchetche akimtoka beki wa AS Vita.
Mashabiki wa Azam wakiishangilia timu yao baada ya kuingia fainali ya kagame
Mshabiliaji wa Azam, Mrisho Ngasa akimtoka beki wa AS Vita, Pambani Makiadi katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ambapo Azam imeshinda kwa mabao 2-1 na kuingia fainali ya michuano ya kombe la Kagame kwa kupambana na Yanga Julai 28.
Kikosi cha APR.
Kikosio cha Azam.
Kikosi cha AS Vita. Picha zote na Francis Dande

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2012

    Hongera sana Yanga na Azam kwa kubakisha kombe nyumbani.Pia pongezi kubwa kwa kocha wa yanga Tom ,kwani amekaa na timu muda mchache sana na kuibadilisha kiufundi na sasa tunaona soka la kuvutia.Pia pongezi nyingi kwa Azam kwani ni mara ya kwanza kushiriki mashindano haya na wametinga hatua ya fainali.Kwa kiwango kilichoonyeshwa na timu za Tansania ktk mashindano haya hasa Yanga na Azam ,inaleta matumaini ktk timu ya taifa,hivyo kocha awe makini ktk zoezi la kuchagua wachezaji wa taifa kuna vipaji kibao tu bongo.Natabiri kombe linaenda jangwani kwa mara ya pili mfululizo,kila la kheri yanga.Mdau wa ughaibuni ,big Joe

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2012

    Asante Francis,asante blog ya Jamii kwa picha.TFF punguzeni viingilio,attendance siyo nzuri..Pongezi kwa Yanga na Azam.

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2012

    Michuzi, tutaweza kuangalia fainali live mkubwa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2012

    Mashabiki mnaojiita wa AZZAM:

    Muwe mashabiki wa kweli kwa timu hiyo na msije kuwa 'nyoka wmenye vichwa viwili' yaani huku muwe AZZAM na kichini chini muwe 'MSIMBAZI' msije mkavuna mawe maana safafri hii Yanga ni Demu hasa, hizo ndio zenu na kama hamuamini hapo mlipo mmo wa Msimbazi,,,uongo?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2012

    Hi Ankal!

    Timu ni kama taasisi fulani hivi yenye nia ya kuleta faida na furaha kwa wadau wake, basi Young Africans tuwe makini na kuendesha timu yetu, mimi nimeangalia mbali zaidi siyo ushindi na mafanikio tu bali pia uendeshaji wa timu, unahitaji watu wenye muono wa kimataifa katika mambo hata madogo madogo lakini pia yanachangia mafanikio! Nimegundua Shirt (Jersey) za David Luhende na Godfrey Taita hazifanani na Shirt za wachezaji wenzao walizochezea Semi Final ya jana na APR! Je Young Africans hatuna kits manager na pia kuna mechi ya kwanza kabisa golikipa Yaw Berko alivaa jersey ya juu ya timu ya taifa ya Ghana! tujaribu kurekebisha mambo madogo madogo ili tuwe uniformity! mengineyo tutaendelea kukumbushana kama kuwapeleka Jerry Tegete, Ladislaus Mbogo na Shamte Ally kwa mkopo kwa timu nyinginezo za Premier ili waweze kurudisha viwango, hili litatusaidia kuwa na wachezaji wenye uchu na uwezo wa kuisaidia Timu yetu. Naomba kutoa hoja!

    shark_ham@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2012

    yanga huyooo!!!! kesha.....wa!!!
    mahariii!!! kesha......waaa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...