Mchuuzi maarufu wa korosho na njugu maarufu kwa jina la Bahanuzi akiwa kazini katika mitaa ya Lindi kama alivyonaswa na kamera ya Globu ya Jamii hivi karibuni. Kutokana na ubunifu wake wa mavazi na nidhamu ya kazi, Bahanuzi huuza korosho na njugu kwa wingi kila aendapo
 Msamaria mwema akimwelekeza Bahanuzi wapi pa kupeleka mashambulizi
Bahanuzi wa Lindi ni kivutio tosha kila apitapo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hakika dhana ya maisha bora kwa kila mtanzania imemuinua kimaisha!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Dah! anastaili sifa kwa ubunifu.

    ReplyDelete
  3. Pita msimbazi tukutengenze

    ReplyDelete
  4. Jangwani mpo?

    BAHANUZI WA LINDI!

    HIVI KWA KIWANGO HIKI CHA UPENZI SIKU ILE YA BAO 5-0 HUYU BWANA MKUBWA ALIKUWA NA HALI GANI?

    Hazina iliyofichika ipo huko Lindi.

    Watu kama hawa ndio muhimu Klabuni angalau awe anauzia korosho zake pale !!!

    ReplyDelete
  5. Kuna umuhimu jamaa akaribishwe Chama Tawala kama hayupo huko.

    Jamaa apewe na Kadi ya CCM ili akamilishe mzunguko kamili!

    ReplyDelete
  6. Yanga itabidi siku mkikutana na Simba 'Bahanuzi wa Lindi' apewe angalau Dk. 5 uwanjani acheze kidogo ili kama awasalimie Mashabiki na kuwachangamsha!

    ReplyDelete
  7. Nadhani siku ya 5-0 kutoka Msimbazi uliwaachia ngedere na kima kapu lote la Korosho!!!

    Asubuhi yake labda ulipiga simu Jangwani kuomba mtaji mwingine utumiwe kwa M-Pesa!

    ReplyDelete
  8. Bahanuzi wa Lindi,

    Huyu jamaa inaonyesha hata damu yake ni ya kijani na sio nyekundu kwa unazi wake!

    Angepewa angalau Penalti siku ya Simba na Yanga afunge bao kwa ajili ya Yanga !

    ReplyDelete
  9. Rangi za Vilabu vyetu vya Soka Yanga na Simba ni balaa.

    Nilishuhudia ktk Benchi la Mpiga rangi za viatu (Shoe shine) Dar waikutana wateja wawili wakiwa hawajuani.

    Mpiga rangi akafungua gunia la ndala za wateja za kuvaa kwa muda huku viatu viking'arishwa.

    Huku akiwa Mpiga rangi hajuiitikadi za kimichezo za wageni wake wateja, akamruhsia ndala za Kijani jamaa akiwa hajui ni Shabiki wa Simba na mwingine akatupiwa ndala rangi nyekundu.

    Kilichotokea yule Shabiki wa Simba akazitupa chini ndala za kijani na yule wa Yanga akazitupa chini ndala nyekundu, sisi watazamaji yetu macho,,,vitendo bila makosa wakabadilishana ndala hapo hapo wa Simba akachukua nyekundu na wa Yanga akachukua za Kijani!

    Jamani ushabiki huu hadi 'aleji' za rangi unafaa???

    ReplyDelete
  10. Said Bahanuzi wa Kusini Lindi,

    Duhhh, itokee jamaa apewe mpira uwanjani apige kumfunga Juma Kaseja wa Simba golini (puuu gooooooo!!!),,,,,ahhh huyu Bahanuzi inaonekana atakufa kwa furaha na mzuka wa wazimu!!!

    ReplyDelete
  11. Ehhh jamaa Yanga asilia inaonekana hadi jasho yake ni kijani na njano!

    ReplyDelete
  12. Mtu kama huyu akipewa namba akifika ktk 18 lazima iwe waya,,,maana akikosa atakufa kwa maumivu!

    ReplyDelete
  13. YANGA:

    Ktk upigaji wa penati muwe mnaweka watu kama huyu jamaa, hata akiwa kwa Mahsabiki kwenye Uwanja akiuza korosho zake aitwe anaambiwa aweke kapu chini ili atimize jukumu la Klabu.

    Inaonekana kwa uzito wa imani yake juu ya timu hawezi kukosa kufunga bao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...