Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe Abdallah Ulega

Na Abdulaziz Video, Lindi


Kaya 256 Wilayani Kilwa Mkoani Lindi  zimetia dosari zoezi  la sensa na makazi kufuatia kaya hizo zilizo katika Kata ya kata ya Tingi, Kilwa Masoko na Kivinje na Njinjo wilayani himo kukataa kuhesabiwa  kwa madai ya kutokuwapo kipengere cha dini katika zoezi hilo
Akitoa taarifa hiyo  katika kikao cha Baraza la Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Ulega alieleza kuwa kwa asilimia kubwa ya kaya zilizo katika wilaya zimejitokeza na kutoa takwimu zao kwa makarani waliopita katika maeneo yao huku baadhi ya Kaya zikikataa kutoa taarifa zao
Kufuatia hatua hiyo,Ulega aliwataka Madiwani wa wilaya hiyo kuendelea kuhamasisha jamii zilizo katika zao  kujitokeza kujiandikisha katika siku zilizobaki sheria isichukue mkondo wake kufuatia ukiukwaji huo uliopo Kisheria.
Akifunga kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri Hiyo,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Ally Mohamed Mtopa aliwasihi Madiwani hao kwenda jamii zao kutoa hamasa zaidi katika siku zilizobaki huku akitupia
lawama kwa baadhi ya Kaya zilizogoma kuhesabiwa kwa madai ya dini huku wakidharau maagizo ya Viongozi wao wa Dini.
Awali kikao hicho  pia kilipitishaa Sheria ndogo ndogo za kutunza rasilimali za msitu wa hifadhi wa kijiji cha Nanjirinji  Baada ya Sheria hizo kukubaliwa na kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji na baraza la maendeleo ya kata na kuwasilishwa katika kikao hicho na Mratibu  wa Shirika la  Utunzaji wa Mpingo wilayani humo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...